Nini cha kufanya ili kuepukana na Sumu Kuvu kwenye nafaka?

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,305
3,327
Juzi iliripotiwa kuibuka kwa ugonjwa wa ajabu huko dodoma na watu kadhaa walipoteza maisha.

Leo kupitia magazeti imebainika kwamba ule ni ugonjwa ambao chanzo chake ni sumu kuvu ambayo hupatikana kwenye vyakula aina ya nafaka.

Kwa mujibu wa wataalamu sumu kuvu ni jamii ya fangasi ambao hutokea kwenye nafaka na hudhuru binadamu pale anapokula nafaka hio kwani sumu hii haishi kwa moto nikimaanisha kupikwa kwa vyakula.

Kimsingi ni ngumu kuanza kuchambua nafaka uweke pembeni zile zenye fangasi ndopo ule.Na sio rahisi kuitambua sumu kuvu kwa macho hii inahitaji vipimo vyakimaabara.

Ni maandalizi gani yafanyike kwenye vyakula vya nafaka ili kuondoa sumu hii kabla ya kupika hizi nafaka?
 
Mzizi Mkavu na wengineo njooni huku muokoe jahazi.Maana sasa sidhani kama hili Dona humu madukani litakua salama.Plz hata kwakuwaita wataalamu waombeni waje watoe elimu kuokoa maisha ya watz
 
Mzizi Mkavu na wengineo njooni huku muokoe jahazi.Maana sasa sidhani kama hili Dona humu madukani litakua salama.Plz hata kwakuwaita wataalamu waombeni waje watoe elimu kuokoa maisha ya watz

Ni kweli sumu kuvu (aflatoxin) ni tatizo kubwa kwa nchi za kitropiki hususani ambako mahindi na karanga ni vyakula muhimu.

Acute exposure (kula sumu nyingi kwa wakati mmoja) ndio inaweza kusababisha madhara ya vifo vya ghafla kama ilivyotokea Dodoma. Hata hivyo chronic exposure (kula vyakula vyenye kiwango kisichoua papo kwa hapo) ndio tatizo kubwa zaidi kwani hupelekea madhara mengi kama saratani ya ini, kudumaa mwili na akili, udhaifu wa kinga mwilini na kadhalika

Cha kufanya
1. Safisha na koboa mahindi kabla ya kula (hupunguza hadi 60% ya sumu). Ugali wa dona tunaupenda sana, lakini ni hatari
2. Usile mahindi yenye dalili ya kuoza (pamoja na aflatoxin, mahindi ya namna hii huwa na kiwango kikubwa cha fumonisin ambayo nia aina nyingine ya sumu kuvu yenye madhara kiafya)
3. Madhara ya chronic exposure ya sumu kuvu ni makubwa zaidi kwa watoto wanaokua. Epuka kumlisha mwanao vyakula vivyoandaliwa na nafaka usizokuwa na uhakika wa hali yake. Katika hili ni vizuri ukaanda mwenyewe unga wa uji wa mtoto na epuka kutumia karanga na mahindi mengi kwenye huo unga. Nafaka kama ngano na mchele ni salama zaidi.
4. Vyakula vinavyopikwa kwa kuchemshwa na magadi ni salama zaidi

Pamoja na hatua zinazoweza kuchukuliwa na mtu mmoja mmoja, lakini hatua za kitaasisi na kiserikali ni muhimu kama vile kupima unga unaosindikwa viw3andani, hasa wa chakula cha watoto.

Mikoa yote yenye mvua kidogo na joto jingi huwa na mazao yenye maambukizi makubwa ya fangasi na sumu-kuvu.
 
Wakulima wakauushe nafaka vizuri kabla kuhifadhi. Benchmark below 13 % moisture content. Vile wet basis au dry basis?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom