Najua fika haitafanyika hivyo. Ila si vibaya kutoa ushauri kwa vile yaelekea wenye kazi hiyo aidha wanaogopa, wanaona ni kazi bure au hawamtakii mema rais wetu. Si kwamba hawajui.
Hata saa hii, saa kumi na mbili kasorobo, bado kuna wakati kwa rais Samia kuokoa kilichobaki katika heshima na utu wake. Lakini akiishinda ego.
Ego, ( nafsi, kiburi, kuonekana, kutoambilika), ndiyo ilimfanya Shetani akosane na MMungu hadi akamfukuza milele, ingawaje Yeye Allah ni Mwingi mno wa kusamehe na wa huruma.
Ego, ndiyo sifa mbaya zaidi katika nafsi ya binadamu, na ndiyo sababu ya msingi ya majanga na kila maovu. Mtu ataiba mabilioni, atachukua rushwa, atakusanya vito vya fahari......si kwa sababu anavihitajia vyote hivyo! Ego.
Ego yaweza kumrubuni rais kwamba akiondoka yeye hakuna mwingine atayeweza kuongoza nchi. Au kumpotosha kuwa haya yatapita tu, au yote yaliyotokea ni njama za nje au Dini fulani!
Maoni yangu ni kuwa kuachia madaraka hivi sasa kungemrejeshea baadhi ya heshima na hata pengine huruma. Actually, watu huwa wanamsamehe haraka mtu anayejiuzulu (Mwinyi, Sokoine...)
Kama ningekuwa miye >
1. Ningelihutubia Taifa na kukiri bila kuuma maneno, kwamba makosa yalifanyika, na mimi, kama Kiongozi Mkuu, nachukua majukumu yote.
2. Ningeomba msamaha wa dhati kwa wananchi, kuahidi wote waliohusika kuchukuliwa hatua, na wote walioathrika kupatilizwa yaliyowasibu. Ningeunda mara moja kikosi kazi cha kuwatafuta na kuwarudisha wote waliopotea, ikiwemo miili ya marehemu, kuwaachia wafungwa wa kisiasa, na kuweka mipango ya kulipa ridhaa.
3. Ningetangaza kujiuzulu rasmi katika muda nitakaouanisha kwa mujibu wa taratibu za Katiba zinazoelezea nini kifanyike katika hali hiyo.
4. Ningeitisha mkutano wa maridhiano ya Kitaifa.
Kwa kuendelea kuongoza katika hali hii si tu makosa zaidi yatafanyika siku hadi siku. Na hata asipofanya makosa, kwa wengi, kila atakalolifanya halitaonekana zuri, hata akiamua kumpa kila Mtanzania nusu kilo ya dhahabu! Rais Samia asiamini kabisa kuwa Watanzania wengi na Dunia wanaamini kuwa ameshinda uchaguzi.
Hata akiamua kubakia, njia pekee ni kurudia uchaguzi.
Kuendelea kuongoza, inevitably, hiyo itabakia kuwa sumaku ya machafuko na migogoro. Aidha, Tanzania itaathirika na kusuasua (hatuna wakati; mwaka 2035 tutakuwa milioni 100). Asilimia 30 ya bajeti ya Tanzania yategemea misaada na mikopo.
Kamwe hakutakuwa na misaada kwa miaka mitano. Hii kusema "tutajitegemea, tutakaza mkanda, who're you, ni heri kula majani..." siyo scientific! Wachina, Warusi au Wahindi watatusaidia, technically, lakini hawana liquidity (fedha rojorojo).
Deni la nje la Tanzania linakaribia kula asilimia 45 ya GDP (mapato yote) yetu. Tutalipaje! Baya zaidi, bila mabadiliko, kuna uwezekano wa vikwazo zaidi vya uchumi.
Kwa maslahi ya Tanzania...
Huu ndio ushauri wangekupa washauri wako. Lakini...nani '(atamfunga paka kengele)'###
Naaa......'hoja haipigwi gongo'.