Ninasumbuliwa na "Chronical Acne. Zinaninyima amani mbele za watu

Mrucy Paul

Member
Oct 31, 2023
18
15
Mimi nina sumbuliwa na "Chronical Acne", zinaninyima amani mbele za watu, nakuwa uncomfortable , hata kumtizama mtu usoni inakuwa ni ngumu. Umri unaenda bado zipo, mpaka sasa 30 yrs

Inafikia hatua ukimtizama mtu usoni, maada inabadilika anaanza kunishauri tena mara tumia sabuni ya ngwanji, mara Dettol soap, mara tumia lemon, mara paka mkojo wa punda. Wakati huu mimi nimetumia product kubwakubwa kama:

CeraVe, The ordinary products, Vovi deep pole cleanser, Nax n.k lakini ngoma bado, ndo maana nimeziita Chronical Acne

Naombeni ushauri, nitumie nini ili nikae vizuri, Au nifanye nini ili niwe na amani japo kidogo hata nikiwa mbele za watu... Mawazo yenu ni faraja kwangu.....

Sent from my JamiiForums mobile app[/URL]
 
Sasa Ndugu yangu si ungesema Tu unasumbuliwa na chunusi? Kulikua na ulazima gani wa kutaja majina magumu magumu asubuhi yote hii? Anyway, angalia allergy ila sidhani kama hizo ndude ni big deal
 
Mkuu chunusi zinanyima confidence kabisa yan had kutembea unaweza ona aibu,
Nakumbuka miaka flani nilikua na machunus had mzazi aliniambia ww nenda kwanza hospital hahaa , ila kuna dawa nilitumia mkuu baada ya mwezi ziliisha zote had leo sina hata, nikiikumbuka nitarud kukwambia.
 
Nakushauri kwanza ielewe aina ya ngozi yako. Maranyingi ngozi za mafuta na ngozi sensitive ndizo zinakuana chunusi sana. Hatua za kufanya ni hizi. Kwanza meza dawa za minyoo kama Albendazole. Meza Dozi kamili. Kisha tafuta Mafuta yenye kiambata aina ya Salicylic acid, ukipata made in USA itakua ni uhakika sana. Kisha chukua na moisturizer yenye Salycilic Acid pia. Sasa Kuna hatua za kufuata ili kuleta ufanisi
Wakati unaanza kutumia kwa wiki mbili za mwanzo jitahidi uwe unajifuliza kwa mvuke marambili kwa siku asubuhi na jioni. Unaweza kutumia steamer maji ya moto. Ukimaliza kifukiza usoni au mwili Mzima Kisha paka hiyo toner ya Salicylic acid, Subiri kwa dakika 20 Kisha paka hiyo moisture. Toner tafuta Kampuni ya Clean & Clear na Moisturizer Tumia Neutrogena au Clean and clear pia.
Ikigoma hapo uje tuangalie dawa silia.
Ingia Instagram tafuta page imeandikwa "Trendi Cosmetics" huyo dada anauza OG toka USA.
Ukipona njoo ushuhudie pia
 
Kwavile umeshatumia dawa kubwa kubwa bila kupata matokeo chanya, isikufanye udharau hizo mdogo mdogo, huenda zikawa sahihi.

Anyways, umejaribu kupima allergy? Maana kuna baadhi ya reactions mfano chunusi zinaweza kusababishwa na allergy.
Nilienda kupima hospital, nikaambiwa ni allergy ya ngozi, pia nina sensitive skin, pia ni overproduction oil skin.
Wakawa wamenielekeza nitumie bidhaa za CeraVe, sasa CeraVe zote nimetumia, (CeraVe foaming cleanser, CeraVe soothing cleanser, CeraVe hydrating cleanser)...

Age inaenda bado zipo, mpaka sasa 30 years ila bado zipo....
 
Sasa Ndugu yangu si ungesema Tu unasumbuliwa na chunusi? Kulikua na ulazima gani wa kutaja majina magumu magumu asubuhi yote hii? Anyway, angalia allergy ila sidhani kama hizo ndude ni big deal
Kuna tofaut kati ya chunusi na Acne ....

Chunusi kwa kingereza zinaitwa pimples .
Acne hakuna jina la kiswahili,
Ila kuna definition of Acne......

Acne is a skin condition that occurs when your hair follicles become plugged with oil and dead skin cells. It causes whiteheads, blackheads or pimples. Acne is most common among teenagers, though it affects people of all ages.......
 
Nakushauri kwanza ielewe aina ya ngozi yako. Maranyingi ngozi za mafuta na ngozi sensitive ndizo zinakuana chunusi sana. Hatua za kufanya ni hizi. Kwanza meza dawa za minyoo kama Albendazole. Meza Dozi kamili. Kisha tafuta Mafuta yenye kiambata aina ya Salicylic acid, ukipata made in USA itakua ni uhakika sana. Kisha chukua na moisturizer yenye Salycilic Acid pia. Sasa Kuna hatua za kufuata ili kuleta ufanisi
Wakati unaanza kutumia kwa wiki mbili za mwanzo jitahidi uwe unajifuliza kwa mvuke marambili kwa siku asubuhi na jioni. Unaweza kutumia steamer maji ya moto. Ukimaliza kifukiza usoni au mwili Mzima Kisha paka hiyo toner ya Salicylic acid, Subiri kwa dakika 20 Kisha paka hiyo moisture. Toner tafuta Kampuni ya Clean & Clear na Moisturizer Tumia Neutrogena au Clean and clear pia.
Ikigoma hapo uje tuangalie dawa silia.
Ingia Instagram tafuta page imeandikwa "Trendi Cosmetics" huyo dada anauza OG toka USA.
Ukipona njoo ushuhudie pia
Daah asante sana, ni kweli kabisa salicylic acid ni nzuri sana, na ndo bidhaa nazo tumia sasa, sijui kuna vitu labda nakosea. Pia kujifukiza ni miongon mwa mbinu ambazo nishawahi fanya.

Nashukuru umeniongezea kitu.
Nitatafuta hiyo dawa ya minyoo,

IMG_20231213_083001.jpg
 
Vitu muhimu kabla ya kutaka kitibu chunusi sio product sema Niko busy kidogo kipenz nitakuja nikueleweshe vizuri
Daah asante sana, ni kweli kabisa salicylic acid ni nzuri sana, na ndo bidhaa nazo tumia sasa, sijui kuna vitu labda nakosea. Pia kujifukiza ni miongon mwa mbinu ambazo nishawahi fanya.

Nashukuru umeniongezea kitu.
Nitatafuta hiyo dawa ya minyoo,

View attachment 2841092
 
Okay sawa, ukikaa sawa basi kama hutojali nahitaji madini yako
Sasa muhimu kwanza kabla ya product ni kutambua tatizonna kurekebisha mazingira Yako binafs kwanza
1.unatakiwa ubadilishe mlo kama mpenz wa junk food ni janga
2.pima hormone Kuna wakat ni mvurugiko wa hormone unaweza kazana na product kumbe shida ni hiyo
3.hakikisha una badilisha folonya za mito ya kulalia Kila baada ya siku 3
4.uistumbue chunusi Wala kushika shika uso pia hakikisha Kam unapaka makeup unatumia brash safi ni vema kma mpenz uwe na brash zako mwenyewe unaenda nazo saloon
5.kupona ni process sio muujuza acha kuchange product Kila wakat tumia moja sio chini ya miez miwil hata mitatu kuna product zinachelewa kukupa matokeo
6.kutibu chunusi na madoa ni Kosa anza na chunusi zikiisha ndio unatafuta ya kuondoa madoa ukiwa hujacontrol chunus kupona madoa ni ndoto na ukitumbua chunusi ni tatizo zaid
 
Ulivopost hapo juu ni sahihi basic ingredients Kwa chunusi ni salicylic acid na citric acid
So ongezea facewash pamoja na moisturer na sunscreen pia ufanye routine asubuhi na usiku kilasiku
Nunua hii facewash
IMG-20230727-WA0007.jpg
 
Back
Top Bottom