Uache kugegeda kama upo kwenye mechi ya ushindani, unaweza kumletea matatizo!! Pia jitahidi kumfanya awe ni mtu mwenye furaha muda wote hata kama inatokea anakuudhi, furaha yake kwa sasa ndiyo furaha ya mwanao mtarajiwa!!
Ukiona kitu chochote tofauti wahi hospitali haraka, mfano kutoka damu sehemu za siri, kuumwa tumbo na mengineyo! Ni vyema ukawa na namba ya daktari mzuri wa maswala ya uzazi ili wakati mwingine unampigia kupata ushauri ingawa wabongo hatuna kawaida ya kuwa na madaktari binafsi lakini cha ajabu wafugaji wa kuku huwa wanakuwa na wataalamu wao wa kuku na wanawalipa vizuri tu hahahaaa!!
Hongera kwa kuwa baba mtarajiwa