NB: nadra Sana kupata tunu hizi Kwa nchi nyingi Kusini MWA jangwa la Sahara. Mfano Somali, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Burundi, Rwanda, Niger, Mali, Burkina Faso n.k
Mkuu kuhusu kujivunia nakuunga mkono kwa asilimia zote ila kusema hizo tunu hazipo kwenye nchi nyingi kusini mwa jangwa la Sahara sio kweli.
Mkuu ukweli ni kwamba kuna nchi chache sana zenye misuko suko kwa sasa kusini mwa jangwa la Sahara. Mathalan, Somali, DRC Congo. Central Afrika na sehemu kidogo ya Msumbiji!
Burundi na Rwanda ulizozitaja hazina misuko suko kabisa kwa sasa. Kuhusu Mali, Niger na Burkinabe wananchi wenyewe wameamua kubadili uongozi wao waliouona hauwafai.
Tujifunze kusema ukweli kwa faida ya wasomaji wengine na vizazi vijaavyo!
Kweli TZ bado tuko nyuma sana. Mleta mada unajiona fahari kujilinganisha na hizo nchi ambazo kutwa ni mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ??
Mleta mada unajiona bora kati ya nchi duni, hii inaamnisha hata TZ iko katika rank moja na hizo Nchi.