Sina uhakika sana kwa sababu mimi sio mchumi lakini nina wasiwasi kwa maana uchumi wa nchi ni tofauti na uchumi wa mtu mmoja.
mtu mmoja uchumi wake ni wa matukio kwa maana ya fedha aliyoipata ameitumiaje ukitumia kustarehe au kufanya miradi ya maendeleo.
lakini uchumi wa nchi ni zaidi ya matukio kwa ni lazima kuangalia mzunguko wa pesa.
tuchukulie kama tuna shilingi bilioni tano kama taifa na tukaamua kuzitumia katika sherehe za muungano na hapa fedha hizi zikaingia kwenye mifuko ya watu wa kawaida nadhani sherehe za muungano hazitumii imports nyingi. nadhani hapa ndani ya mwaka mmoja fedha hizi zikiwa zinazunguka na kutatua shida za watu mbalimbali huku zikirudi serikalini kupitia kodi mbalimbali zitatekeleza miradi mingi katika tanzania ikiwemo pengine kujenga barabara.
lakini kama tukichukua fedha hizo bilioni tano tukaziingiza kwenye barabara, nasikitika kusema asilimia kubwa ya fedha tunazoziingiza kwenye barabara zinatoka nje ya mipaka yetu. kwa maana vifaa asilimia kubwa, makandarasi kwa hiyo tunakuwa kama taifa fedha hiyo nyingi imeenda ngambo na sisi kubaki na kidogo kwenye mzunguko wetu na ukitathmini kwa mwaka fedha hiyo imeleta matokeo gani kwenye jamii nadhani inaweza kuwa ndogo.
jamani wachumi mliosoma uchumi jadilini mada hizi ili jamii ione umuhimu wa taaluma yenu kwenye jamii.