Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,188
- 8,215
Kila mtu ana maoni yake, yangu ni haya; Dirisha lililopita la usajili, lile kubwa na dogo, Simba walifanya sajili kwa utulivu wa hali ya juu sana. Walitulia na kuangalia mahitaji ya timu, ndiyo maana sura zao mpya zimelipa sana.
Kuanzia kwa Larry Bwalya, Bernard Morrison, Thadeo Lwanga na Chris Mugalu. Sidhani kuna hata mmoja ambaye, Simba wanajuta kumsajili.
Ukiniuliza mimi, usajili bora zaidi wa Simba katika dirisha lililopita, sitahitaji hata sekunde ya kufikiria, jibu langu litakuwa wazi na lililonyooka, 'JOASH ONYANGO'
Ni beki anayejua maana ya kulinda lango lake. Ni mtu ambaye jina lake unatakiwa ulitaje la kwanza kabisa unapoulizwa mfano wa 'STOPPER' mmoja wa uhakika.
Joash anakaba sakafuni, anacheza hewani tena uhakika sana. Achana na hilo, Onyango ni mwepesi sana wa kusoma madhaifu ya wenzake hivyo anasawazisha makosa yao kwa urahisi mno.
Jina la Chama, show za Bwalya na Miquissone, na magoli ya Mugalu na Kagere, yanafanya baadhi ya kazi za wachezaji wengine zionekane za kawaida, kama inavotokea kwa Onyango.
Nafikiri kati ya wachezaji watatu bora wa msimu wa Simba, jina lake linapaswa kutokea. Joash ni habari nyingine aisee. Kwa mabeki wa kati Ligi kuu Tanzania Bara Onyango anatokea dunia yake kabisa
.
@deo_mwanasoka