kumtorea = kumtolea
unaposema 'ulimpenda' ina maana mapenzi yamekwisha?
Moja ya silaha ya mahusiano ni communication, je umezungumza na mwenzio kuhusu mabadiliko yake ya tabia?
Umezungumza nae jinsi unavyojisikia?
Kwa upande wako unazungumza nae vipi? Kwa heshima na upole au kwa ukali na kushurutisha?
Kumbuka heshima ni pande zoye mbili na ukishurutisha pia huleta kutokuelewana.
Je anapokataa kufanya yale unayomweleza, na kufanya anavyojisikia , hayo anayoyafanya ni kwa manufaa yenu wote wawili? Je yanalengo la kuboresha future yenu?
Vunja ukimya mkuu, zungumza na mwenzio, ndipo utakapopata jibu kama umwache au uendelee nae, bila kusahau yapaswa ujinguze pia mapungufu yako na urekebishe.
Future ya mahusiano yenu ipo mikononi mwenu