Nimesikiliza audio ya Didas Masaburi, anatakiwa kushitakiwa kwani anaratibu vijana wengine

Ccm kama wabunge ndio hawa poleni sana sasa huyu ataenda kuteta nini cha wana ubungo zaidi ya maslai ya chama chake
 
Nilipoisikiliza audio ya jana, mitandaoni, inayosemekana ni ya kada wa CCM na mgombea wa CCM wa Ubunge Jimbo la Ubungo Dr. Didas Masaburi, nikakumbuka ile video iliyodaiwa kunasa mipango ya kamanda wa CHADEMA Bwana Winfred Muganyizi Lwakatare. Audio ya Masaburi inasikika mipango ya kuwaandaa vijana kuandamana kama wanachama wa CHADEMA kuonesha umma kuwa wanamuunga mkono Dr. Slaa kwa yale aliyoyasema.

Katika audio hiyo, anayesemekana kuwa ni Masaburi pamoja na watu wengine wanasikika wakipanga na kusifia maandamano ya vijana ili kuchora mchoro wa CHADEMA kuvurugika. Mipango hiyo ya kuwaandamanisha vijana,ni mipango ovu. Ni kama ile ya kwenye video iliyodaiwa kuwa ni ya Kamanda Lwakatare iliyokuwa ikisuka kutekwa,kuteswa na hata kudhuriwa kwa baadhi ya watu.

Audio ya Masaburi ililetwa humu jamvini na Mkuu KakaKiiza. Video ya Lwakatare iliwekwa humuhumu na Mkuu hugochavez. Ingawa zote ziliwekwa humu kunakosomwa na watu wa kila rika,kada na kazi/vitengo, video ya Lwakatare ilishughulikiwa haraka. Lwakatare alitiwa nguvuni na hata kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi na utekaji. Najua ilitumika ile pamoja na ushahidi mwingine.

Audio ya Masaburi hadi sasa imefuatwa na ukimya mkubwa. Hakuna aliyekamatwa hadi sasa kufuatia audio hiyo ambayo nayo inabeba mipango ovu kwa mustakabali wa Taifa. Hakuna hata aliyehojiwa juu ya suala hilo. Kwanini? Masaburi na Lwakatare wote ni watanzania ingawa ni wa vyama tofauti. Inajulikana kuwa Masaburi ni wa CCM na Lwakatare ni wa CHADEMA. Kiraia,wako sawa. Haki itendeke.


Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

kuna sehemu anasema alisahau kumpigia kova......hiii inaashiria jeshi la polis lina tumika vibaya.
 
Last edited by a moderator:
Masaburi akishinda tena akishinda kihalali basi hii nchi tuanzishe utamaduni wa kupima akili wapiga kura

Halafu alivyo na jeuri baada ya yale maandamano na hiyo clip kusambaa kaita vyombo vya habari na kwa kauli zake wala hajakana tuhuma zilizoelekezwa kwake...

Kakiri kabisa uhusika wake ingawaje kataja tu kuwa hao vijana ni wa CDM na yeye kawapokea na kuwapa kadi za CCM...

Mimi nadhani ukiwa kiongozi CCM kuna kiapo cha kujiwehusha lazima ukikiri...
 
Halafu alivyo na jeuri baada ya yale maandamano na hiyo clip kusambaa kaita vyombo vya habari na kwa kauli zake wala hajakana tuhuma zilizoelekezwa kwake...

Kakiri kabisa uhusika wake ingawaje kataja tu kuwa hao vijana ni wa CDM na yeye kawapokea na kuwapa kadi za CCM...

Mimi nadhani ukiwa kiongozi CCM kuna kiapo cha kujiwehusha lazima ukikiri...


Kama unawajua Wajaluo
walivyo majeuri huwezi mshangaa
 
Ndiye nilimsikia akitangaza kuwa $100 million za kujenga kituo kikuu cha mabasi Ubungo zilihamishiwa kwenye mradi wa mabasi yaendayo kasi!
Kama hamtaki kupimwa akili baada ya uchaguzi basi muulizeni ni kwa nini hizo za DART (?) hazikuhamishiwa kwenye kituo maana barabara iliyojengwa haionyeshi utofauti (positive) na iliyokuwepo labda kuwa nyembamba zaidi!
 
mnyika sisi tulimsubili wakati wa kampain ubungo ili atwambie zile nyaraka za richmond alizokuwa nazo mkononi na kutamba nazo ameziweka wapi?

na sasa ametukimbia mjanja,


Hii hapa sikiliza wee mpuuzi kamueleze Masaburi ndiyo hoja hapa jamvini
 
Kulingana na hii clip iliyorecordiwa kwa siri na mmoja wa vijana waliotumwa kufanya fujo, inatakiwa polisi wachukue hatua dhidi Masaburi dhidi ya siasa za kihuni maana huyu Masaburi anasababisha uvunjifu wa amani, inatakiwa Kamanda Kova kusimamia hili!

Nimeisikiliza kwa makini inamaana Masaburi bado anampango wakuwatuma tena vijana hivyo hii inaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Uratibu huu unaokuja ni wakumtukana Lowassa hivyo Polisi fanyeni kazi dhidi ya siasa taka za mitaroni.

Bonyeza hapa Kusikiliza.

Ile clip ya Slaa hotelini na hii ya masaburi dah vinanisikitisha sana. Kwamba tumefikia kufanya haya mambo na kutumia vijana sababu tu ya kuchafua wengine keli jamani?
 
WanaJanvi km ntawakwaza mnisamehe nimeitaji KUMJUA HUYU masabuli KWA kuwa Jana na LEO akauki masikioni mwangu....
Kukiri kuwa alikutana na VIJANA waliiandaliwa na CCM KUMPINGA LOWASA
Na ilo LA kutoa Bango LA LOWASA kariakooo!!!!
Narudia naombeni KUMJUA masaburi NI nani???
 
WanaJanvi km ntawakwaza mnisamehe nimeitaji KUMJUA HUYU masabuli KWA kuwa Jana na LEO akauki masikioni mwangu....
Kukiri kuwa alikutana na VIJANA waliiandaliwa na CCM KUMPINGA LOWASA
Na ilo LA kutoa Bango LA LOWASA kariakooo!!!!
Narudia naombeni KUMJUA masaburi NI nani???

Ah..ni baba mmoja anatafuta sifa za kuvizia....
 
Wabunge wa Dar wanafikiri kwa kutumia Makalio by Dr Didas Masaburi. Inaonekana akili zake ndivyo zilivyo, pia lile suala la ARVs Fake liliishia wapi?
 
Back
Top Bottom