Mie nakuunga mkono kwenye hili ila sio mwisho wao nadhani watajipanga na kuanza upya kama kipindi cha Rijkaard timu ilifanya vibaya ila baadae walirudi na kufanya vizuri kinachowasumbua kikubwa Barcelona ni ukongwe wa wachezaji wao na ndio naona huyu kocha mpya Ernesto Valverde amekuja na falsafa ya kuwakomaza vijana kama kina Sergi Roberto,Dennis Suarez maana nadhani mtu kama Javier Mascherano umri unamtupa mkono sasa anahitaji mbadala wake Andre Iniesta nae anaelekea huko kwa hiyo itachukua muda kidogo kuwapika hawa vijana ila nina imani chama litarudi tena na kufanya vizuri tujifunze kutokata tamaa ili tufanikiwe.Kila jambo huwa lina mwisho wake. Nimeshuhudia timu bora ya wakati wote Barcelona ikitamba katika soka la kisasa. Timu zote imara zilinyanyaswa na Barcelona ya kuanzia mwaka 2008-2012. Kisha Barcelona ya 2013 - 2015.
Wote ni mashahidi jinsi Messi, Xavi na Iniesta walivyoipa timu hii mafanikio. Kisha ikaja MSN nayo ikatamba na kunyayasa vilabu vingi vya Ulaya kama sio Dunia.
Na sasa naona mwisho wao Umefika, ni kama nilivyoshuhudia Mandela akifikia mwisho wake hapa Duniani, ni kama nilivyoshuhudia Ukuta wa Berlin ukidondoshwa mwaka 1990, Ni kama tulivyoshuhudia mwisho wa maisha ya Papa John Paul wa II, Ni kama nilivyoshuhudia mwisho wa Barack Obama kuwa Rais wa Marekani na sasa nashuhudia mwisho wa Timu bora ya wakati wote, Barcelona ikifikia ukingoni. Ni ukweli unaouma laikini hatuna budi kuukubali.
Asante mungu nimeishi katika kipindi cha timu bora ya wakati wote, na mimi nitakuja kuwasimulia wajukuu wangu panapomajaliwa.
Ni kweli kabisa unajua baadhi yetu tumekuwa ni watu wa kutoa matokeo mapema kwa hizo mechi mbili wakati kuna nyingine nyingi zitachezwa na kuamua matokeo.
Lucho alituletea falsafa yake ya Direct football akanunua na magarasa yake ambayo hamna kitu yanafanya.Kizazi cha sasa cha Barcelona kimefikia ukingoni, ni wakati wa Barcelona kuanzisha kizazi kingine.
Jana nilishuhudia Barcelona isiyokua na meno, jana nilimuona Messi akicheza kama namba 8,10,9 alifanya hivi akijaribu kufukia mashimo ya wengine lakini alishindwa.
Kuna wachezaji wengi hawana hadhi ya kuichezea Barcelona, wa kwanza ni Andre Gomes. Uyu jamaa sijui walimuokota wapi?
Man u kafungwa fainali mbili na barca ila arsenal ndo wameumizwa zaidSio kwa Barcelona hata ikibadirisha vipi mwendo wake ni balaa ukitaka details waulize ligi ya uingereza hasa man u.
Sent using Jamii Forums mobile app
Muosha huoshwa. Na wao sasa ni dhohofu ile hali.Man u kafungwa fainali mbili na barca ila arsenal ndo wameumizwa zaid
Sent using Jamii Forums mobile app