figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Heshima kwenu wakuu,
Baadhi ya sehemu ya mabalozi na wawakilishi wa Mabalozi wa nchi mbalimbali wakiwa Ukumbini wakati kura za ndio na hapana zilipopigwa
Mwenyekiti wa CCM amenisikitisha na kunikatisha tamaa kabisa. Najiuliza tunapelekwa wapi kama hata katiba ya CCM haiheshimiki. Hata ukijaribu kuhoji kulikoni unakamatwa na kuwekwa ndani au kupewa vitisho. CCM tumelazimishwa kufanya Mabadiliko sababu hayajafuata Sheria na Katiba ya CCM inavyotaka.
Tumelazimishwa kukubaliana na Matakwa ya Viongozi wetu wa juu.
Wasanii wa Bongo Movie wakiwa Ukumbini wakati kura za ndio na hapana zilipopigwa
Kilichoniuma zaidi ni hata kuwaleta Ukumbini wasanii wa Bongo Movie wakina Steve Nyerere, Mabalozi na wahasimu wetu wa kisiasa ili Wasaidie kupiga kura za Kupitisha Mabadiliko ya Katiba wawapo Ukumbini, na Wamefanikiwa.
Katiba ya CCM inasema hivi;
"Kiwango cha mahudhurio ya Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa kitakuwa ni theluthi mbili ya Wajumbe walio na haki ya kupiga kura kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wajumbe walio na haki ya kupiga kura kutoka Tanzania Zanzibar.".
Hii hapa Kinana alitutangazia mahudhurio akasema;
"Mkutano mkuu una Wajumbe 2,380, Wajumbe waliotoa taarifa kwamba hatahudhuria wapo watano, na wengine hawakuhudhuria kwa sababu nyingine wapo 19. Waliohudhuria humu ndani wapo 2,356 sawa asilimia 99.97". Hili sina tabu nalo.
Tatizo ni hapa;
"Kubadili sehemu yoyote ya Katiba ya CCM kwa uamuzi wa theluthi mbili za Wajumbe walio na haki ya kupiga kura kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili za Wajumbe walio na haki ya kupiga kura kutoka Zanzibar."
Lakini kura hazikupigwa wala matokeo hayajatangazwa kama Katiba inavyotutaka tufanye. Ni kwa mara ya kwanza kura za kubadilisha katiba ya Chama chetu CCM imepitishwa kwa Kura za Kinyemela za Ndio na hapana. Hata wale wasio na sifa za kupiga kura (Wasanii wa Bongo Movie) walisema ndio.
Haya Mabadiliko yaliyopitishwa HAYANA UHALALI.

Maswali yangu:
i) Theluthi mbili za Wajumbe walio na haki ya kupiga kura kutoka Tanzania Bara walikuwa Wangapi?
ii) Theluthi mbili za Wajumbe walio na haki ya kupiga kura kutoka Tanzania Zanzibar walikuwa Wangapi?
iii) Waliopiga kura ni Wangapi?
Kama hakuna Majibu, haya mabadiliko ya Katiba hayana Uhalali wa Kisheria (null and void). Tumepelekeshwa pelekeshwa bora liende na hii ni mbaya kwa Demokrasia yetu wancahama kama CCM.
Naamini 2020 hamtatubadilisha Katiba kwa style hii.