teh teh, life jackets zikae kwa pilot??ulijaribu kuwaulizia kuhusu hizo life jackets zilipo!!!labda wamezitunza kwa rubani,wanaogopa abilia wengine huwa wanateremka nazo!!!
jnia-kia, kia-mwz, mwz-jnia.
great thinkers,
hivi punde nimesafiri na ndege za 540.
Wahudumu wangu walikuwa george na moses akati ruban wetu alikuwa adili. Ila co pilot simkumbuki)
maelezo ya usalama yalitolewa kwa uzuri na moses huku george akitumia ishara mbalimbali kama namna ya kufunga mkanda nakadharika.
Nilishangaa sana moses alijizuia mazima bila kueleza namna ya kutumia life jackets ikabidi niangalie chini kiti changu nikagundua kuwa halikuwepo.
Nikasema labda kwa wenzagu yapo nikapitisha jicho pia sikuyaona.
Siku nyingine tena hivyo hivyo zaidi kukawa ndani ya ndani hakuna fan ama sijui ac ilikuwa haifanyi kazi ila akatuomba radhi wasafiri kuwa pindi ndege ikipaa hewa itakuwa ya kutosha.
Naomba sana mamlaka husika ziwe makini kuangalia masuala haya, nilitoa lalamiko kama hili juu ya mafuriko haikupita mwezi yaliyotokea dar kila mtu ni shahidi.
Nawasilisha
Ile jet CRJ 200 ? Inapaswa kuwa hivi.....ni kweli hazipo labda unanyofoa siti
dah....hili basi gani...? Linaenda wapi na wapi....?zuri kweli....
dah....hili basi gani...? linaenda wapi na wapi....?zuri kweli....
We Preta wee......basi hili kweli? N madirisha ya hivo kweli?
mkuu pole kwa kukosa vifaa muhimu vya kunusuru uhai endapo chombo cha angani kingeleta taabu. Inaonekana ndio umeanza kutumia usafiri huu wa angani na huna uzoefu nao. Ni wazi kwamba ulitanguliza uoga na hofu sana mkuu, wakati mwingine hivyo vifaa vinaweza kuwepo ikitokea taabu hata kukumbuka mahali kilipo au ukikipata unashindwa kukitumia, ukikitumia uhakika wa kunusurika pia sio asilimia 100. uwe unamtanguliza mungu kwa kila jambo. usitumie tena hizo ndege za hao uliowataja.