Kwanza pole. Fanya kama ifuatavyo:
(a) Tafuta copy ya kadi ya gari yako ambayo umepoteza.
(b) Nenda kituo cha Polisi waambie wewe umepoteza gari ya gari, watahitaji hiyo photocopy ili waridhike kuwa wewe ndio mwenye gari. Usijali kwa sasa hivi kama umekata kipande na kuweka kingine. Achana na mambo ya chasis no. nk. Waombe wakupe 'Police Lost report.'
(c) Wakisha kupa hiyo 'police Lost report', nenda nayo TRA sehemu wanayo andikisha magari, waoneshe hiyo 'Police Lost report', watakuambia uende benki ukalipe sh. 10,000.00 kisha mwandikie barua meneja wa TRA kuomba 'duplicate copy' ukiambatisha vifuatavyo: 1. 'Police Lost report'
2.Bank payment receipt ya sh. 10,000.00
3. Kitambulisho ( photocopy) ( cha mpiga kura kinatosha)
(d) TRA watakupa kadi nyingine baada ya siku thelathini (30 days)
Kila la heri