Mavindozii
JF-Expert Member
- Oct 20, 2012
- 2,111
- 2,778
Msaada jamani nimepoteza cheti cha form IV ,kwa anayejua namna ya kupata kingine please anisaidie jamani. I hope to hear from you Guys,
Kwa sasa siyo kazi ndugu KikaragosiDah shughuli yake sio ya kitoto aisee.
Zamani walikuwa wanatoa kitu inatiwa testimonials sijui kama bado utaratibu huo upo.
Kama uko Dar nenda pale maeneo ya Bamaga maeneo ya Sinza/Mwenge Baraza la mitihani watakupa taraibu zote.
Basi ashugulikie tu atapata cheti chake.Kwa sasa siyo kazi ndugu Kikaragosi
Kwanza toa taarifa kituo cha polisi kalibu na eneo ulilopotezea cheti, Baada ya hapo nenda Gazeti la mwananchi au gazeti lolote linalosomwa sana toa tangazo. Baada ya wiki mbili au tatu chukua kopi ya kipande cha gazeti la tangazo ambatanisha pamoja na R/B lost report peleka balaza la mitihani. Pale utapata maelezo mengine kwa hatua zaidi ila huwezi pata cheti bali utapata results zako.