Ngongoseke
JF-Expert Member
- Jan 1, 2012
- 3,202
- 1,464
inaelekea una bahati ya kutapeliwa. Sasa ukitaka uwe salama jinyamazie kimya la ukitaka kubahatisha kutapeliwa basi wee fuata maelekezo yao.
Matapeli wa kizamani sana! Mimi nilipata ujumbe kama huo kabla ya kombe la dunia South Afrika.
Hiyo ya leo hata kidhungu hakijakaa vizuri yaani, YOUR MOBILE NUMBER HAS BEEN WON. Kwa tafsiri, hii inamaana kuna mtu ameshinda namba yako ya simu. Inamaana namba yako ya simu ya mkononi ilishindanishwa bila wewe kujua na sasa mshindi, anayepaswa kukabidhiwa namba yako ya simu ya mkononi, amepatikana. Kazi yaki sasa ni kumpatia namba yako mshindi wa namba yako. In other wordss, namba hiyo siyo yako tena na umpe aliyeishinda. Pole kwa attempt la kutapeliwa
Ngongoseke! Usijaribu chochote hapo! Huu ni utapeli mkali sana. Kuna watu wanaamini wapo watu waliolala wa kuibia hela.
Aisee Ngongoseke usisikilize maneno ya bajamaa, wanakuonea wivu kwa sababu umeshinda bahati nasibu na wao hawajashinda. Wewe wakontakti tu hao waliokutumia ujumbe ili uchukue mkwanja wako kiulaini. Ukichelewa hiyo bahati ya kutapeliwa itakupita. Shauri yakooo!!!!
Jaribu bahati yako...kila mtu ana zali lake bhanaaa! ...hata JK hakujua km atakua Rais mpaka alipopigiwa kura
hivi jiulize, una simu ya blackberry? Kama huna iweje uambiwe umeshinda wakati simu ya blacberry huna.
je ulishirika hiyo bahati nasibu wanayodai umeshinda? Kama hukushiriki sa ushindi umeutoa wapi.
Hao scammers mimi uwa napokea emails kibao kila week mara nimeshinda bahati nasibu ya gmail, mara yahoo mara sijui comesa mara sijui bank gani wizi mtupu..
Wizi kama wataka tapeliwa haya go for it
Ngongoseke! Usijaribu chochote hapo! Huu ni utapeli mkali sana. Kuna watu wanaamini wapo watu waliolala wa kuibia hela.
Yah ukweli natumia blackberry na wamenitumia kwenye simu ya bb hapo sasa ndo najiuliza vp wamejua natumia bb?