Nimepigwa na kitu kizito! Nimehudumia mtoto mwaka mzima kumbe sio wakwangu

Dunia ina Mambo,Kuna kitu Cha kujifunza hapa wahenga wanasema simulia Sana omba yasikukute.Pole Sana kwa yote ila msamehe huyo mkeo, sikuzote ukiwa unarukaruka Leo na Huyu kesho mwengine lazima uje upakaziwe ujauzito tu.,Ukipenda boga penda na ua lake huyo mwanamke anakupenda lakini aliogopa kukwambia ukweli yawezekana mwenye mtoto alimkataa akaamue akupakazie wewe labda kutokana na ustaarabu wako.Na ukiamua kumuacha Leo hii ataishije maisha haya yalivyo na changamoto chamsingi wewe onesha kwamba unatoa sadaka,Tenda wema usingoje shukrani kumbuka wema ni akiba na ubaya pia ni akiba.Ni ngumu Sana kumuacha mtu mliozoeana wengi watakushauri piga chini lakini sio rahisi kiivyo.kama baba wa mtoto anamuhitaji mtoto wewe mpe mtoto ubaki na mke Kama unaweza kulea wote unalea tu na utampata mtoto wako.maji yakishamwagika hazoleki Cha muhimu ni kusonga mbele.wakati nasoma cheko zilinibana nikajikuta nacheka kwa sauti utazani mazuri vile ebu wazia we ingekuwa kwako msomaji.Nukuu-" Upendo huvumilia,hufadhili,upendo hauhusudu;upendo hautakabari,upendo haujivuni".(1Kor.13:4)
Usimwingize Chaka mkuu

Huyo mwanamke angekuwa anampenda angemwambia ukweli juu ya ujauzito kwann alimdanganya

Alikaa na yeye kwakuzuga pengne baba mtoto Mambo yake n magumu so akawa anasuburi ajipange yakikaa sawa asepe

WAKATI MWINGINE TUAMUE MAMBO KAMA WANAUME HURUMA HUZAA DHAMBI

fikiria angegundua mtoto anamiaka 4 SI ndo Mambo ya kuandaa mkaa gunia 4 kuwachoma kabisa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Naenda kwenye maada,, stak kupoteza mda wakuu,,

Naumia sana tena inauma

Nimehudumia mimba mpaka kujifungua mbaya zaidi mtoto akafikia mwaka na miezi sita ndipo nikabaini mtoto sio wakwangu

iko hivi, nilikuwa kwenye mahusiano na binti alivyobeba ujauzito akafukuzwa kwao, nilitumia gharama nyingi ili isijulikane nikapoteza kazi nilionayo, tukayajenga nilee mimba nikaendelea kulea mpaka alivyojifungua mtoto wa kike, nikampa jina mtoto kwa jina la mama yangu mzazi (MINZA) kwakuwa ndio mtoto wangu wa kwanza,

Juzi nmeshinda bila kula nilivyogundua minza sio mtoto wangu

Ukatili niliofanyiwa alikuwa akienda kliniki kadi kaandika jina jingine na baba mwingine, akitoka huko ana kadi nyingine sijui kaitoa wapi, anakopi yaliyoandikwa huko anajaza kwenye kadi ile yenye jina nililompa mtoto, kawaida yake kila akitoka huko ananiletea kadi naiona.

Kilichotokea, nimepanga nyumba moja na nesi mmoja akaniuliza mtoto wako ESTA anaendeleaje? nikamwambia haitwi Esta bali anaitwa MINZA akaniuliza mbona kwenye kadi mmeandka ESTA BALELE ambalo jina la Balele siyo la kwangu aisee tulibshana, akaniambia siku wakija kliniki atazizuia kadi ili anitoe ubishi nikamhakikishia haiwezi kuwa hivyo sababu kadi naijua ina jina langu

Juzi nimeiona kadi ina jina jingne la mtoto baba babu,, ikabidi nimpigie simu tukutane ilipofika jioni akaja, nilimuuliza neno moja tu, niambie MINZA ni mtoto wangu au sio wangu sema ukweli najua kila kitu na Balele ni nani, binti akaanza kulia akasema sio mtoto wangu ni mtoto wa Balele, nilipwatwa hasira nilimpiga

Niliona haisaidii nitamuumiza na mpaka sasa sina cha kufanya gharama nilizowekeza ni nyingi mno naumia mwenye mtoto alikuwa ahudumii.

Nifanyeje jamani mtoto alikuwa anakesha usiku analia nahangaika,

Nahitaji faraja.

Yuda exalioth
natumia jamiiforums
karibuni Geita.
Hiyo kawaida sanaa mkuu wala isikuumize kichwa piga chini sahau garama zote songa mbele pesa zinatafutwa tu wa sio issue. Binafsi ishawahi nitokea na nikahudumia mtoto na mamaake karibu miaka miwili ikaja bumbuluka mtoto sio wangu kumbe dem aliona mwenye mzigo huduma hawez akaleta kwangu mi sina hiyana nkalea tu mpaka mtoto kakua almost 2 yrs of age ndo nakuja kujua sio wangu nkamachek mwanaume mwenzangu tukayajenga kiume na tukawa washikaji dem nkapiga chini nkablock kila mahali na maisha yanasonga huu mwaka wa pili sina contact nae
 
Mkuu kuna watu wanapenda kuumiza wenzao na kazi kuvuruga ona yaliyonitokea mimi hapa

huyu binti alikua anajua kabsa rakin akaamua kuniumiza kama alikua hafanyi makusudi asingetumia kadi mbili , sijui lengo lake badae ilikua nini jamani
Story yako ni the same na jamaa yangu yaliyo mkuta, sasa yeye alikuwa na demu ila demu walikuwa wanaishi wilaya tofauti, demu akanasa mimba ya fundi nguo akamwambia jamaa yangu amtumie hera ili anunu chakula kumbe ndo pesa ya kutoa mimba, akanasa mimba ya pili kwa kajamaa kanafunzi ka veta anamwambia jamaa yangu make sure ndani ya wikii hii tunasex na kweli jamaa akamfuata demu wakasex baada ya mda demu akamwambia ninaujauzito wako, aisee, rafiki wa demu ndo alikuja kufumua siri zote na uchafu ambao demu alikuwa anamfanyia msela mbali na kwamba msela ameshaenda kujitambulisha kwa demu na imebakia akatoe posa
 
Angeoa malaya jamaa yako asee
 
Nami naziona dalili hapa kuna kamtu kamekomaa kana mimba kana mimba ila kenyewe kanataka kutoa mm nimekaambia huwa sishiriki utoaji mimba na nitakaruhusu endapo tu kakinithibitishia mimba hiyo sio yangu maana ktk dhambi nisiyoipenda ninkuleleshwa mtoto wa mwingine.

Kamekubali kuwa hakatoi ila kwenye suala la mimba ni ya nani haswa hapo siri kanabaki nayo kenyewe yaani natamani nipate ujanja wa kukabana kafunguje ukweli mimba ni ya nani ila sijaipata hiyo mbinu
 
Ni ushauri mzuri sana mkuu ulionipa nakusanya mawazo kama haya niyafanyie kazi asante sana
 
Nami naziona dalili hapa kuna kamtu kamekomaa kana mimba kana mimba ila kenyewe kanataka kutoa mm nimekaambia huwa sishiriki utoaji mimba na nitakaruhusu endapo tu kakinithibitishia mimba hiyo sio yangu maana ktk dhambi nisiyoipenda ninkuleleshwa mtoto wa mwingine.

Kamekubali kuwa hakatoi ila kwenye suala la mimba ni ya nani haswa hapo siri kanabaki nayo kenyewe yaani natamani nipate ujanja wa kukabana kafunguje ukweli mimba ni ya nani ila sijaipata hiyo mbinu
Hata mimi nisingejua kama isingekua nilipata pakuanzia kwenye kadi mbili, rkn tofauti na hivyo anakwambia niyako
 
Story yako ni the same na jamaa yangu yaliyo mkuta, sasa yeye alikuwa na demu ila demu walikuwa wanaishi wilaya tofauti, demu akanasa mimba ya fundi nguo akamwambia jamaa yangu amtumie hera ili anunu chakula kumbe ndo pesa ya kutoa mimba, akanasa mimba ya pili kwa kajamaa kanafunzi ka veta anamwambia jamaa yangu make sure ndani ya wikii hii tunasex na kweli jamaa akamfuata demu wakasex baada ya mda demu akamwambia ninaujauzito wako, aisee, rafiki wa demu ndo alikuja kufumua siri zote na uchafu ambao demu alikuwa anamfanyia msela mbali na kwamba msela ameshaenda kujitambulisha kwa demu na imebakia akatoe posa
Jambazi sugu, unaoa mke kumbe jitu hatari
 
Hiyo kawaida sanaa mkuu wala isikuumize kichwa piga chini sahau garama zote songa mbele pesa zinatafutwa tu wa sio issue. Binafsi ishawahi nitokea na nikahudumia mtoto na mamaake karibu miaka miwili ikaja bumbuluka mtoto sio wangu kumbe dem aliona mwenye mzigo huduma hawez akaleta kwangu mi sina hiyana nkalea tu mpaka mtoto kakua almost 2 yrs of age ndo nakuja kujua sio wangu nkamachek mwanaume mwenzangu tukayajenga kiume na tukawa washikaji dem nkapiga chini nkablock kila mahali na maisha yanasonga huu mwaka wa pili sina contact nae
Mliyajengeje huyo msela gharama alirudisha au
 
Usimwingize Chaka mkuu

Huyo mwanamke angekuwa anampenda angemwambia ukweli juu ya ujauzito kwann alimdanganya

Alikaa na yeye kwakuzuga pengne baba mtoto Mambo yake n magumu so akawa anasuburi ajipange yakikaa sawa asepe

WAKATI MWINGINE TUAMUE MAMBO KAMA WANAUME HURUMA HUZAA DHAMBI

fikiria angegundua mtoto anamiaka 4 SI ndo Mambo ya kuandaa mkaa gunia 4 kuwachoma kabisa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Naunga mkono
 
lea tu mzee mbona tunafuga mbwa anazaa na unaweka oda ya mabak buchan na hotelin na umjui baba mbwa,. Huyo ndio mwanamke kiumbe ambacho kikikupenda hukupa hata mtoto asie wako na kukuaminsha n wako
 
Back
Top Bottom