figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,720
- 55,843
Halmashauri ya Songwe huko Tunduma Mbozi, CHADEMA ina Madiwani wa Kata 14 na CCM 1. Hivyo Halmashauri inaundwa na CHADEMA.
Leo wakati naangalia Taarifa ya habari naona viongozi wa UVCCM wilaya wakiiomba Serikali kufuta uchaguzi wa Madiwani na kuunda Kamati ya muda ya kuongoza Halmashauri kwakuwa hao Madiwani waliochaguliwa kuunda Halmashauri hawana uwezo wa kuongoza zaidi ya kuwagawa.
Hawa ndio Vijana wa chama tawala wanakuwa na Jecha syndrome! Halafu ndio baadae warithi uongozi na fikra hizo.
Kweli ni ileile haibadiliki! Nilidhani vijana wa sasa hivi watakuwa na fikra tofauti, kumbe haibadiliki. Ni ileile.
Hiki chama kina safari ndefu sana ya kujifunza maana ya Demokrasia ya uchaguzi na Chama kujiendesha bila kutegemea mbeleko ya Serikali na Taasisi zake.
Hii figisufigisu, inawaumbua CCM walivyo waroho ma Madaraka. Hayo yatokea huku Viongozi wao wa kitaifa wakishangilia, kucheka na kuwapigia makofi vijana wao wa UVCCM Mbozi.