Ambiele Kiviele
JF-Expert Member
- Dec 29, 2014
- 15,271
- 29,934
NIMEYAPENDA SANA HAYA MANENO
Mwanamke ni kama Jua unaweza
usione umuhimu wake, yaani kila
siku unaenda mjini jua lipo tu,
unaliangalia lakini huangalii umuhimu
wake kwako.
Wakati mwingine likiwa
kali unaanza kulalamika kuwa
linachoma na lina kera. Lakini
ukitafakari kidogo tu utajua kuwa bila
jua maisha yasingekuwepo.
Hembu
chukulia mfano mchana kungekuwa
giza tu kama usiku nini kingetokea?
Chakula tunachokula ni kwasababu
ya Jua, mvua ikinyesha sana
mafuriko yakitokea tunatamani jua,
kwenye baridi tunatamani pia jua,
Hatuliwazii kwasababu lipo tu na
linatimiza majukumu yake kimya
kimya bila kelele.
Hiyo ni sawa na
mwanamke, ukishaoa kuna mambo
ambayo mwanamke huyafanya na
baada ya muda unaanza kuyaona ya
kawaida kawaida, chakula kinakuwa
mezani kila siku hujui kinapikwaje na
vyombo vinaoshwaje, anabeba
mimba na watoto wanazaliwa hujui
maumivu aliyoyapata lakini
unatabasmu na kucheka ukijisifia
watoto wangu na hata mkigombana
unasema niachie wanangu wewe
nenda tu tafikili unajua maumivu
aloyapata kipindi anawaleta duniani
ao watoto.
Watoto wanaumwa mpaka
wanapona hujui hata wameponaje,
wanalia usiku hujui hata nani alikuwa
anawabembeleza, ukirudi unakuta
nguo safi chumba kisafi hutoi hata
shukurani kwakuwa ushasahau kua
kuna mtu anasafisha siwe safi muda
wote.
Na anafanya vitu vyote hivyo
kama Jua bila kelele lakini wewe
ukitoa elfu mbili ya sukari
utamnynayasia mpaka ndugu zake
kuwa unawalisha wewe!
Hembu siku
aondoke akuachie hao watoto
unaojisifia kila siku kuwa ni wakwako
na kumuambia hajaja na kitu, uanze
kuwapikia na kuwaandaa kwenda
shule, ufue nguo zao na zako.
Unaweza kuajiri mfanyakazi lakini
hawezi kufanya hata nusu ya kile
anachokufanyia mkeo, kwani yeye
atafanya kama kazi lakini mkeo
anafanya kwa mapenzi, hahitaji
umlipe chochote zaidi ya kutimiza
majukumu yako na kumheshimu
kama mke katika maisha yenu.
Vuta
picha umeamka mkeo hayupo, watoto
wanataka kuogeshwa kunywa chai na
kwenda shule, hapo unatakiwa
kuwahi kazini na mchana watoto
wale! Mheshimu sana mkeo kuna
mambo mengi ambayo anayafanya
ukiambiwa uyafanye ww
utachanganyikiwa na mkeo huyafanya
kwa upendo.
Mwanamke anachohitaji
kwa mume ni upendo na heshima tu.
Mhudumie, mpe upendo, muheshimu
na muonyeshe kuwa kwako ana
umuhimu mkubwa, mfanye mkeo
atabasamu kila mara na familia nzima
itatabasamu
Mwanamke ni kama Jua unaweza
usione umuhimu wake, yaani kila
siku unaenda mjini jua lipo tu,
unaliangalia lakini huangalii umuhimu
wake kwako.
Wakati mwingine likiwa
kali unaanza kulalamika kuwa
linachoma na lina kera. Lakini
ukitafakari kidogo tu utajua kuwa bila
jua maisha yasingekuwepo.
Hembu
chukulia mfano mchana kungekuwa
giza tu kama usiku nini kingetokea?
Chakula tunachokula ni kwasababu
ya Jua, mvua ikinyesha sana
mafuriko yakitokea tunatamani jua,
kwenye baridi tunatamani pia jua,
Hatuliwazii kwasababu lipo tu na
linatimiza majukumu yake kimya
kimya bila kelele.
Hiyo ni sawa na
mwanamke, ukishaoa kuna mambo
ambayo mwanamke huyafanya na
baada ya muda unaanza kuyaona ya
kawaida kawaida, chakula kinakuwa
mezani kila siku hujui kinapikwaje na
vyombo vinaoshwaje, anabeba
mimba na watoto wanazaliwa hujui
maumivu aliyoyapata lakini
unatabasmu na kucheka ukijisifia
watoto wangu na hata mkigombana
unasema niachie wanangu wewe
nenda tu tafikili unajua maumivu
aloyapata kipindi anawaleta duniani
ao watoto.
Watoto wanaumwa mpaka
wanapona hujui hata wameponaje,
wanalia usiku hujui hata nani alikuwa
anawabembeleza, ukirudi unakuta
nguo safi chumba kisafi hutoi hata
shukurani kwakuwa ushasahau kua
kuna mtu anasafisha siwe safi muda
wote.
Na anafanya vitu vyote hivyo
kama Jua bila kelele lakini wewe
ukitoa elfu mbili ya sukari
utamnynayasia mpaka ndugu zake
kuwa unawalisha wewe!
Hembu siku
aondoke akuachie hao watoto
unaojisifia kila siku kuwa ni wakwako
na kumuambia hajaja na kitu, uanze
kuwapikia na kuwaandaa kwenda
shule, ufue nguo zao na zako.
Unaweza kuajiri mfanyakazi lakini
hawezi kufanya hata nusu ya kile
anachokufanyia mkeo, kwani yeye
atafanya kama kazi lakini mkeo
anafanya kwa mapenzi, hahitaji
umlipe chochote zaidi ya kutimiza
majukumu yako na kumheshimu
kama mke katika maisha yenu.
Vuta
picha umeamka mkeo hayupo, watoto
wanataka kuogeshwa kunywa chai na
kwenda shule, hapo unatakiwa
kuwahi kazini na mchana watoto
wale! Mheshimu sana mkeo kuna
mambo mengi ambayo anayafanya
ukiambiwa uyafanye ww
utachanganyikiwa na mkeo huyafanya
kwa upendo.
Mwanamke anachohitaji
kwa mume ni upendo na heshima tu.
Mhudumie, mpe upendo, muheshimu
na muonyeshe kuwa kwako ana
umuhimu mkubwa, mfanye mkeo
atabasamu kila mara na familia nzima
itatabasamu