Ramea
JF-Expert Member
- Mar 19, 2015
- 2,146
- 4,090
Kuna siku nilikuja na Uzi wa kwanini dokta wa Ultrasound hakutaka kuniambia jinsia za wanangu. Wengi mlitoa comments zenu, nikaridhika nazo.
Kiukweli tarehe ya matazamio ya kujifungua tuliambiwa ni 21 November ila wife kajifungua tangu October 7th. Alipata complications na baada ya kucheck kwa Ultrasound tena na tena, majibu yalionesha mtoto mmoja aligeuka vizuri na mmoja alilala vibaya (kiubavu).
Madokta zaid ya watatu walisema lazima afanyiwe operation ingawa alianza kuonyesha dalili za uchungu wiki ya 33, wakanishauri tusubiri walau hadi iishe wiki ya 34. Ila uchungu ukazidi akajifungua mtoto wa kwanza (yule aliyekaa vizuri) kwa kawaida.
Mungu si Athman maandalizi ya operation ya kumtoa mtoto aliyebakia yalipokamilika akajifungua mtoto wa pili kwa njia ya kawaida. Tulikaa hospitali wiki moja tukaruhusiwa, ila huyu aliyebanwa na mwenzie alikula sindano 16 because alizaliwa dhaifu.
Kwa sasa hivi tunaenda hospitali kwa wiki mara moja kwa ajili ya kupima uzito. Mmoja ashafikisha 2 kg, na mwingine bado ana 1.7 kg. Ingawa wameongezeka hawakuzaliwa na kilo hizo.
Vipi kwa uzoefu na utaalam wenu, nipeni experience kwani hadi sasa hawajapata chanjo hadi watimize 2.5 kg.
Pre mature babies kama hawa hukua vizuri kama wengine ambao walitimiza umri tumboni?
Nifanye nini cha ziada?