Nimepata kazi ya mkataba ila nilikuwa na uhitaji wa kazi ya kudumu

Unanishauri kwa ukali mkuu.
Binafsi huwa sipendi kuajiriwa ila mkuu umezingua

Nenda kapige hiyo miaka miwili

Kuwa na nidhamu ya Pesa

Jiwekee akiba ukiweza fungua fixed account kabisa ili endapo mkataba wako utaisha na usipopewa mwingine unakuwa tayari una mtaji

Unaangalia biashara ambayo una uzoefu nayo unafanya

Biashara ikichanganya unaweka mtu kisha unatafuta ajira nyingine(kama unapenda kuajiriwa)

Mtaani sio kuzuri mkuu

Unaweza ngoja hizo nyingine kisha ukazikosa, utafanyaje?
 
Nakushahuri uende ukafanye hio kazi, kama sikosei ni kazi ya mradi wa wizara ya afya upate uzoefu na connection. Zikitoka za kudumu omba pia, Hizo database za wafanyakazi wa kudumu na wa mradi ni mbili tofauti wala Haito leta shida ukija kuomba kazi ya kudumu.🙂🙂🙂
 
Tusio na ajira na hatujui Ni lini tutapata ajira, tunakuangalia kwa jicho Kali Sana...tunatamani tukutukane Ila Sheria za jukwaa hazirihusu.
Acha basi mi nikushauri kwa kuzingatia Sheria za jamiiforum.

Nakushauri nenda kafanye kazi.. miaka miwili Ni mingi Sana endapo utafanya kazi kwa umakini na kujituma na kua na nidhamu na pesa, kupitia ajira hio ya Muda utapata connection nyingi tu.

NB: Usipoenda usirudi hapa kulalamika mtaani kugumu.
 
KAZI hipi??umepata..wewe NI mwalimu au dactor..na je majina yakitoka haupo inakuwaje...Kwann usiende Tu kufanya utafte mtaji
Wazo zuri yeye anawaza la kesho badala achangamkie fulsa .anauhakika Gani kama hao elf 23 na yeye ataapia Malaki Hawana ajira yeye kapata ya mkataba anaanza maringo tena sasa asiripoti asubir kibali Cha mama
 
Halafu aliyekudanganya ni nani kuwa ukipata ajira serikalini huwezi PATA tena serikarini?wewe hujafukuzwa kazi umepata kazi ya muda omba kazi ya kudumu ukiwa kwenye kazi ya mkataba ni ruksa
 
Shida Ajira za kudumu zinatangazwa mwezi ujao.
Unachotakiwa kuelewa ni kwamba humu jamvini kunawatu wako kwenye mifumo ya ajira za serikali wanajua wanachokushauri nenda karipoti ,Fanya kazi Kwa uadilifu mkubwa kajitume utaonekana tu na utapata kazi ya kudumu inshallah.lakin chamsingi mshahara wako jibane sana achana na starehe.ndani ya miaka miwili utakuwa umejipatia mtaji Ili upate kiofisi chakujishikiza Huku mapambano yakiendelea yakutafuta kazi.
 
Well spoken my friend,hakuna kitu Cha kudumu Cha msingi nikumuomba mungu atujali afya na uhai tu unapata kazi ya kudumu unapigwa na stroke huwezi hata kuamka kitandani
 
Wewe achana na utoto! Yani wewe unaweka budget kwa hela ambayo huna? Hiyo kazi ya Samia usipopata? Nenda kafanye kazi wewe achana na ndoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…