Nimeongea na tyre la gari

beco

JF-Expert Member
May 7, 2013
1,339
782
Habar za usiku wana JF,

Jioni ya leo nikiwa natoka kazini kuelekea nyumban nikiwa na kisura chenye bashasha, baada ya kupata kahela kidogo ambacho kwa hesabu za haraka kalikuwa kananipeleka mpaka tarehe 23 ambapo mshahara utaingia,nikiwa maeneo ya kigogo kama vile naelekea loyola nilipanda tuta wakati nashuka tuta nilijikuta narushia watu maji

Kumbe pale chini ya tuta kulikuwa na bonge la shimo ambalo sikuliona kutokana maji kujaa, nikatoa ishara ya kuomba msamaha nikasepa hatua chache tu watu wananipigia kelele pancha panchaa, ikabidi nipaki nishuke kuangalia, dah limekatika na halifai tena nikifikiria sina hela ,

Nina madeni kila kona nimepata kijisenti bwana tyre nae ananifanyia uhuni kwakweli kwa uchungu mkubwa nikaliambia 'HATA WEWE TYRE UNANIFANYIA HIVI !!!AU HAKA KAHELA NILIKOPATA KAMEKUTOA ROHO,HUJUI HALI YANGU NILONAYO ,WE HAYA ILA JUA MUNGU ANAKUONA, KAGIZA HAKA NA KAMVUA HAKA UNANITESA KWELI ,HAYA BWANA MJANJA WW.......

Ndugu zanguni hivi vyuma sasa vinatutia wazimu grisi nayo bei juu
 
Pole sana. Inawezekana gari yako ina rim low profile. Janga kama la kwako lilinitokea karibu napanda mlima Sekenke saa tisa za usiku. Ilikuwa nataka niwahi kufika Shinyanga ili kesho yake alfajiri nigeuze kurudi Dar, sasa kuna gari iliniovertake nikawa nayo kwa karibu na sikuweza kuona maishimo. Basi nikaingia shimo matairi yote ya upande wa kushoto yakapasuka. Mimi nilikuwa na spea moja tu kwenye gari. Basi ikabidi nilale mpaka asubuhi kutafuta msaada. Nilihangaika kupata tairi nikaenda kuipata Igunga used... Siku hiyo nilijuta kusafiri usiku usiku!
 
Dah thnx ila wewe pole zaidi maana tyre mbili halafu ulikuwa mbali tena usiku
 
Mazee, ukiwa na gari ni lazima ukubali kuna siku litakubeba, kuna siku utalibeba.

Juzi kati nimeona kioo cha mbele kimeanza ufa, nikawahi, ila naona ma snow yanavyoanza huku kiwanja na ku heat ndiyo inasababisha ufa unasambaa,Ijumaa napigwa kama $420 kubadili kioo, naambiwa kioo kina makorokocho ya rain sensor kwa hiyo si cha kawaida, na hapo nimekataa kwenda kwa dealer BMW kupata OEM kwa $2100.

Ila nashukuru hakuna uhai uliopotea au mtu aliyeumia, nimali tu imeharibikakidogona kuitengeneza namudu.

Ukiona kwako kunaungua, kwa wenzako kunateketea.
 
Back
Top Bottom