Nimeokota nyumba Dar es Salaam Magomeni

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
14,304
29,834
Hii nyumba inasemekana Ina miaka zaidi ya 15 hapajawahi kukaa mtu wala hakuna dalili za mmiliki kwani Kuna jamaa aliyekuwaga mmiliki aliendaga uingereza na Familia yake wakadai watarudi lakini ikawa byebye kwahiyo mimi baada ya kupata hizo taarifa nikachukua uamzi wa kutafuta homeless ambao hawana uoga wakavunja mlango wakaingia asubuhi wakaingiza vitu kama vyombo I kitanda na godoro.

Imepita miezi mitatu Hao majaa niliwaambia wakalale bado wanalala na mwenyekiti wa serikali ya mtaa alipoenda kuwahoji wakasema ni ndugu wa huyo jamaa aliyeendaga uingereza kwahiyo mwenyekiti akawaita na baadhi ya viongozi, viongozi wakakubali nahao majamaa bado wanakaa na mda si mrefu nafanya miliki. Sio utani ni ukweli.

images%20(58).jpg
 
Msimpinge mtoa mada,

Zipo nyumba nyingi ambazo wenyewe wamekimbia tangu miaka ya 1970.
Ambazo ukiingia vizuri ki documents na history ya hizo nyumba,
unaweza kujipatia nyumba ya kuokota..

Watu wa ardhi wanajuwa nyumba zote ambazo ni mfu,
Ni suala la muda na timing za kuzipora kutoka kwa wanaozilinda.

Haiwezekani mtu ambaye hana back up na watu wa ardhi akawa na vielelezo vyote vya nyumba husika ,
Wakati yeye sio mmiliki wa nyumba Ile.

Kuna nyumba moja ipo magomeni mikumi,,
Nyuma ya police magomeni,

Kwa sasa imejengwa ghorofa halijaisha,
lakini lilikuwa na kesi mahakamani kuna watu 2 kila mmoja anasema ni nyumba yake.

Ukwl ni kwamba Kati ya hao watu wanaogombea nyumba,
Hakuna hata mmoja ni mmiliki halali.

Story ipo hivi...

Kuna Mzee mmoja wa kimakonde alikuwa akilinda nyumba hiyo tangu miaka ya 1970,
Mzee aliishi na family yake humo kwenye nyumba hiyo kama mlinzi.

Kuanzia miaka hyo hakuna mtu yeyote aliyejitokeza au kuja kusema yeye ndy mwenye nyumba.

Inasemekana kuwa mwenye nyumba alikuwa ni mzungu ambaye alikimbia Mambo ya azimio la Arusha au uhujumu uchumi miaka hiyo,
Hakuweza kurudi tena inchini tangu muda huo.,
Na ni Mzee pekee ndy aliyekuwa akimjuwa mmiliki halali wa nyumba Ile,

Kwa jinsi nyumba ilivyojengwa kila mtu alijuwa Yule mmakonde ni mlinzi Tu,
Na sio mmiliki wa nyumba Ile.

Miezi kadhaa baada ya yule Mzee wa kimakonde kufariki miaka ya 2006.

Waliibuka watu kusema kwamba wao ndy ndugu wa yule mmiliki wa mwanzo aliyemuweka Mzee wa kimakonde kama mlinzi.,
Na Wana documents zote.

Jamaa walijitoa muhanga na kuwalipa watoto wa mlinzi wa kimakonde pesa za ulinzi wa nyumba Ile tokea miaka ya 1970 hadi 2006.

Nadhani waliwanunulia Banda kinondoni Moscow.

Wenye nyumba fake wakaanza ukarabati wa nyumba Ile.

Baadae walikuja kusimamishwa na stop order kutoka mahakamani kwamba,
kaibuka mtu mwingine anasema pia ni nyumba yake na ana documents kama zile.

Kesi imekwenda sijajuwa haswa mmiliki halali aliyekabidhiwa na mahakama ni Nani.

Ila wakuu humu mjini zipo nyumba ambazo kama sio muoga,

Unaweza kuokota tena bure kabisa.
Kipindi cha Mambo ya uhujumu uchumi kuna wengi sana walikimbia inchi na kuacha Mali zao huku nyuma bila kujulikana na watu wao.

Kama mtu anataona hii story ni chai,

Aaende magomeni mtaa mikumi na ruaha Street,
Nyuma ya police magomeni aulize nyumba zamani walikuwa wanaishi wamakonde .
Ambayo Kwa sasa walikuwa wanalala wamasai kama walinzi..

Atatambuwa ukwl..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom