Nimeoa na ninaishi na mke mwenye VVU kwa miaka 7

JabagaM

JF-Expert Member
May 24, 2013
539
354
Hakika Mungu ni mwema, kwa mtu wa kawaida utaona kama ndoto lakini huu ndio ukweli.

Nilimchumbia mpenzi wangu bila kutambua status zetu za maambukizo ya VVU.

Kosa nililofanya ni kutokwenda nae ANGAZA siku hizo kwa kujiamini kuwa yeye pia anajali afya.

Nilicheki afya peke yangu na kukutwa sina maambukizo ya vvu. Nikamsisitiza na kumshauli pia nae acheki.

Lakini baada ya kucheki akanificha hali yake ya maambukizo ya VVU kwa kuogopa ningemwaacha.

Tuliendelea kukutana as husband & wife bila kinga. Very innocent and stupid, tukakubaliana tuzae mtoto na MUNGU akatubariki, baada mtoto kuzaliwa nikagundua ahaaa kumbe mwenzangu looh ana VVU na alitumia dawa akiwa mjamzito ili kumkinga kiumbe.

Baada ya hapo sasa, je, nikawaza nimwache au. Nikasikia sauti ininiambia nikimwacha tu, atakufa ghafla hivyo nijipe moyo tufunge ndoa nae na nimwaanzishie dawa na nikafanya hivyo na yupo salama nami pia kwa neema za MUNGU bado sina maambukizi ya VVU angalau hadi leo.

Tunaishi tu kwa amani na tunashiriki kwa kutumia kinga kama wataalam wanavyoshauri. Huu ndio msalaba wangu nimeamua kuubeba kwa gharama zote kwani bado nampenda sana mke wangu kipenzi na tunaheshimiana vizuri.

Niliwaza pia, je ningekuwa ndio mimi yeye angefanyaje, na kama ningemwacha ninayemjua tayari ni yupi tena, huwezi jua ningekutana na mabaya zaidi ya VVU.

Ujumbe wangu: vijana wote ninawaomba tumshirikishe MUNGU kwa kila hatua ili kumpata mke/ mume mwema na tusipende kwa matamanio ya kitandani au sura, umbile, na mali tusije tukajilaumu mpaka kufa.

Mungu ni mwema anitiae nguvu mpaka leo nimekuwa karibu nae zaidi na zaidi na anazidi kufanya miujiza mingi tu maishani mwangu.
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana mkuu, Mungu aendelee kukupa huo moyo wa ukarimu Na Upendo
 
Asante mkuu, ni kwa neema tu za Mungu. Ushauri kwa vijana wote tuwe makini sana katika mahusiano hasa mapenzi.
 
Kama maajabu fulani iv,binadamu katika kizazi cha nyoka kula pipi na ganda almost 7years....
Mwingine angeshakimbia kitambo hata ndoa isingefungwa.
HONGERA SANA.
 
Ni kweli kumekuwa na mada nyingi kuhusu who can and not get infected with HIV. Lakini kwangu nahisi Mungu alitaka kunionesha maajabu yake. Na baada ya kutafakali..., nikasema sasa nimejua nafanyaje au natokaje hapa? Kama nivosema nikasikia sauti hakika ni yake MUNGU, ikisema usimwaache kamwe usije patwa na balaa ambalo sitokutoa tena. Vijana nasisitiza tujifunze kuwa makini na kumshirikisha Mungu. Sio mara ooh tunaaminiana sijui beibi baby nini..., unaweza kwenda na maji. Embu jifikirie una mpenzi halafu anakumbia au unakuja tambua ndio hivo tena... But, I thank God kwa courage hii. Pungufu ya hapo ningempoteza mwenzangu. Lkn we are both alive and safe at the same time.
 
Hongera saana mkuu,umetuachia ujumbe mzur saana sisi nduguzo.....maana wengi wetu tunajali sana sura,umbo kwa ajili ya sexual pressures only...bila hata kumshirikisha Mungu
 
Inatia moyo kuona bado kuna mada kama hizi MMU maana hili jukwaa limevamiwa na watoto. Kila la heri mkuu
 
Back
Top Bottom