DAKA MTUMBA
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 1,288
- 801
Jamani naombeni ushauri.
Ni miaka 9 ya ndoa sasa ila mke hata dalili za kula maembe mabichi hakuna. Mwisho wa siku kanigeuzia kibao eti mimi ndiye jipu, eti mbegu zangu kimeo, nikimwambia twende hospital hataki. Mbaya zaidi amekuwa yupo bize sana na kazi za ofisi so hata muda wa mazungumzo hakuna.
Baada ya kuchoka kuvumilia nikaenda hospital kucheki, majibu yakawa supa sana, nikarudi home nikamueleza wife kwamba nimepima na niko vizuri so twende na wewe ili tujue tatizo, lakini aligoma na kusema kwamba mtoto haletwi na Dr bali huletwa na Mola so tusubiri.
Lakini baada ya mwaka mzima wa mimi kupima lakini bado hakuna kitu, nikaona ngoja nimkumbushie kuhusu mtoto, kiukweli nilijuta wakuu, maana alinitemea mbovu mpaka nikapatwa na usingizi, mbaya zaidi akasema kama mimi sizai mbona hajasikia kama nina mtoto nje? Wakati wote huo anaongea kwa sauti mpaka msichana wetu wa kazi anasikia.
Nikaona kujibishana na mwanamke ni upuuzi so ngoja niendelee na mambo yangu.Ilifikia wakati mpaka akahama chumbani kwangu akawa analala na housegirl.Siku moja nilimuita housegirl na kumwambia kwamba anayoyaona ndani kwetu ayaache ndani kwetu na nisiyasikie nje bcoz wife nampenda sana kiukweli.Tabia yake iliendelea kuwa mbovu mpaka ikafikia akahamisha mpaka nguo zake na kuhamia rasmi kwa housegirl, Nikaona hii ni hatari na nikaamua kuwashirikisha wazazi wa pande zote ili kuinusuru ndoa yetu.
Sababu kubwa ni kwamba anahisi nitamuacha maana sijampatia mtoto so kama kweli nampenda nimpe hati ya nyumba, wazazi wangu waligoma but mie nikaona haina tatizo bcoz mshahara wake ulihusika kwenye ujenzi, nikamkabidhi hati kisha akarudi chumbani. Nilipata furaha ya masaa 48 tu kisha vitimbi vikaanza upya.
Kwa wakati wote huo wa matatizo huduma zote za kufua nguo na kunitengea chakula alizifanya housegirl.Kiukweli tulikua tunafanya sex tu kama mke na mume but sikua napata raha yoyote, nikimwambia twende hospital jibu ni lile lile kwamba mbona sina mtoto wa nje so nisimpigie kelele.Kiukweli Mnyamwezi huyu mrembo nilishindwa kumuacha maana nilimpenda kufa.
Itaendelea.............