Huyo dogo ni noma na sidhani kama yupo Dar maana mpaka kuingia humu JF inaonyesha anakaujanja ka kucheza na mtandao alafu pamoja na maelezo mazuri anakuwa hapajui TIA (hata kama hapajui kwa kufika basi angalau hata kwa kichwani kuwa na picha kidogo), labda anapajua kwa jina lile la zamani kabla ya kuwa TIA
Dogo punguza kucheza na mitandao ya kijamii kama upo serious na unataka kutimiza hiyo ndoto uliyokuwa nayo....unaonyesha toka uko form 1 unaijua Jamiiforums sipati picha kuhusu hzo social network nyingine.
Napata mashaka hata hayo matokeo yako ya form four yamereflect uwajibikaji wako katika mitandao kuliko katika masomo.
Kuwa muangalifu vinginevyo lala sana ili uote ndoto nyingine tofauti na uliyokuwa nayo uwenda hiyo ndoto mpya ikaendana na jinsi ulivyo hivyo kuwa rahisi kuitimiza.