Nimekubali, Lowassa jembe!

Nimekubali, Lowassa jembe!

Joined
Jan 19, 2015
Posts
16
Reaction score
3
Dhoruba imetulia, nuru imetamalaki
Sasa naishika njia, naja tokea Kowak
Ombi ninakuletea, baba naomba nilaki
Simama tangaza nia, taifa lakuhitaji

Elimu yadidimia, kwa kasi iso kifani
Usipotangaza nia, wataizika shimoni
Ujinga utarejea, turudishwe utumwani
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Hatunae kama wewe, kunako uchapakazi
Katu hauna kiwewe, ufanyapo maamuzi
Iwe Tanga ama Kawe, baba huna ubaguzi
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Uchumi utachipua, kwani u mchapakazi
Milango utafungua, ajira zikae wazi
Panya rodi watanywea, tuupate usingizi
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Japo orodha ni ndefu, Lushoto hadi Sikonge
Kwako hawafui dafu, wengine wasaka tonge
Uliza hata Shekifu, wamedoda ka chuchunge
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Hakika wewe ni bora, bara hata visiwani
Tena umetia fora, tangu kura za maoni
Utaibuka kinara, shamba na hata mijini
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Siwezi fika tamati, pasi hili angalizo
Lifike kwenye kamati, isijeleta mchezo
Tutaipiga manati, tukimkosa tulizo
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji


Max Mondu
mondu87@gmail.com

NAWASILISHA KAMA NILIVYOIPOKEA.
 
Subiri kwanza. Hawa watu wanaendelea na adhabu kwanza.
 
Watu wanasaka noti LOWASSA mpe kijana hata laki 5, sitamtosha kufanyia mambo yake.
 
Last edited by a moderator:
Lowassa ndo habari ya mjini kwa sasa,post umeileta wakati mwafaka kabisa aisee
 
Dhoruba imetulia, nuru imetamalaki
Sasa naishika njia, naja tokea Kowak
Ombi ninakuletea, baba naomba nilaki
Simama tangaza nia, taifa lakuhitaji

Elimu yadidimia, kwa kasi iso kifani
Usipotangaza nia, wataizika shimoni
Ujinga utarejea, turudishwe utumwani
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Hatunae kama wewe, kunako uchapakazi
Katu hauna kiwewe, ufanyapo maamuzi
Iwe Tanga ama Kawe, baba huna ubaguzi
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Uchumi utachipua, kwani u mchapakazi
Milango utafungua, ajira zikae wazi
Panya rodi watanywea, tuupate usingizi
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Japo orodha ni ndefu, Lushoto hadi Sikonge
Kwako hawafui dafu, wengine wasaka tonge
Uliza hata Shekifu, wamedoda ka chuchunge
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Hakika wewe ni bora, bara hata visiwani
Tena umetia fora, tangu kura za maoni
Utaibuka kinara, shamba na hata mijini
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji

Siwezi fika tamati, pasi hili angalizo
Lifike kwenye kamati, isijeleta mchezo
Tutaipiga manati, tukimkosa tulizo
Lowassa tangaza nia, taifa lakuhitaji


Max Mondu
mondu87@gmail.com

NAWASILISHA KAMA NILIVYOIPOKEA.

Umebarikiwa sana wewe pamoja na kizazi chako kwa uzalendo uliouonesha.. Kwa hakika Lowassa ni zaid ya jembe na ndiye rais tumtakaye sisi watanzania kwa sasa
 
da....siomcheizyo mama kazi imeanza.....tunasemaje tugawane tu langi za chama si ziko mbili njano na kijani.
 
Jembe metiwa chumvini, lapukutika kwa kutu,
Limepotelea pwani, kimebaki kibubutu,
Hadhari muwe makini, Mpini ni mtukutu,
Mpini kifimbocheza, takutandika mgongo.
 
Hilo liko wazi Lowassa ni Tsunami..... Kwa sasa ana nguvu ya ajabu kama nabii
 
Jembe metiwa chumvini, lapukutika kwa kutu,
Limepotelea pwani, kimebaki kibubutu,
Hadhari muwe makini, Mpini ni mtukutu,
Mpini kifimbocheza, takutandika mgongo.

Ndiyo umeandika nini sasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom