MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,239
- 50,413
Barabara ya kuanzia Manyoni kwenda Tabora ukiacha ile ya kupitia Singida, nusu yake nakisia kama kilomita 150km (equivalent of Nairobi to Nakuru) haijatiwa lami, ni vumbi tupu. Na kuna maeneo yenye makazi ya watu pembezoni. Hapo vumbi balaa, kiasi kwamba unatamani kuona hata ishara ya lami.
Lakini yote tisa, Tabora pazuri watu wa pale wakarimu na hawana hulka za kibaguzi, wageni tukifika tunafanya biashara zetu kwa amani na kugeuza bila matatizo. Hali ya hewa nzuri, vyakula vitamu maana vinatokea moja kwa moja shambani. Japo maji kwenye mabomba hotelini ni tatizo kama ilivyo mikoa mingine kama Morogoro.
Japo nilipata raha pale Isevia na Oxygen, watu wa Tabora humu JF watanielewa nikitaja Isevia.