Nimekua na mashaka na huyu mtoto tangu kuzaliwa kwake

dada zetu mnatupeleka wapiiii!!??nina same story kwa jamaa yangu wa karibu

jamaa alikuwa na mahusiano na binti mmoja msomi mzuri tuu ( nadhani anaweza pia kuwa humu jf), kwenye mahusiano yako binti alipata ujauzito, wakati akilea ujauzito jamaa aligundua kuwa binti alikuwa na mahusiano na mtu mwingine (mume wa mtu), waligombana sana na ikabidi jamaa akatishe mahusiano na yule binti, hakuulizia habari zake wala mambo ya mimba, baada ya muda binti alimtafuta mtoto akiwa na mwaka na miezi miwili hivi, jamaa alishapoteza kabisa hamu hata ya kumuona ila alimwambia kuwa mtoto ni wake na alimtumia picha, kwa kulazimisha kuwa mtoto anafanana naye, jamaa alikwenda kumuona mtoto lakini alikuwa na mashaka kwani huo mfanano aliodai mama mtoto hakuuona kivile akajipa mooyo labda akikua atagundundua, walirejesha mahusiano lakini sio kama ilivyokuwa awali, baada ya muda aligundua kuwa yule baba alikuwa anahudumia kila kitu hadi kodi ya nyumba na anafahamika hadi kwa mama yake binti!alopodai kadi ya mtoto hakupewa na aliamua kumwaga manyanga jumla jumla! hakuwahi kukutana na huyo baba mwingine na wala hamfahamu, binti amekuwa akimshumbua mara kwa mara kudai hiki na kile lakini jamaa amegoma kabisa na hataki hata kumuona mtoto tena!!...kina dada hebu waoneeni huruma watoto...khaaaaaaaaaaaa
 
Wewe huyo mtoto mbona bado unamfatilia..mpoteze mama wa mtoto na mama yake ni matapeli watakusumbua maisha yote..kama bado kuna kitu bado unataka kuwasaidia.. basi mpeleke kwenye shule za bure za magufuli alafu unyamaze kimya
 
Sisi hatuwezi kujua kama mtotot anaweza kuwa wako au la.....pamoja na mlolongo wa DNA ufuate mkapime ili mjue
 
I have similar story... Jamaa yangu best sana tupo nae mtaa.. Alikutana binti wakaanza mahusiano, kumbe binti ana mtu wake mwingine anapigwa huku anapigwa kule. Mimba ikadaka.. Sie tukawa tunasubiria mtoto wetu bana.. Dah..mtoto akazaliwa,sasa mtoto mchanga huwezi amua kwamba wako au laa. Tukaendelea kulea ,kumbe mama wa mtoto kuna vitu vinacklic kichwani, mtoto anapozidi kukua sura ya Baba(mshkaji wetu) haisomi kabisa. Na mtaa kina mama wanasema mtoto wa flan yule,huyo jamaa anajulika. Kuona mama akapaniki akamfosi mshkaji wetu wakafunga ndoa fasta ya kiserikali. Kufupisha habari, jamaa kabaki Baba jina tu mtoto kasafirishwa kwa ndugu zake na mkewe na anasoma huko.. Rumors has it kwamba jamaa kachanganyiwa madawa kabisa ili aendelee itwa Baba jina tu..na kumsahau kabisa mtoto. Its very sad. Wanawake hawaaa!!
dada zetu mnatupeleka wapiiii!!??nina same story kwa jamaa yangu wa karibu

jamaa alikuwa na mahusiano na binti mmoja msomi mzuri tuu ( nadhani anaweza pia kuwa humu jf), kwenye mahusiano yako binti alipata ujauzito, wakati akilea ujauzito jamaa aligundua kuwa binti alikuwa na mahusiano na mtu mwingine (mume wa mtu), waligombana sana na ikabidi jamaa akatishe mahusiano na yule binti, hakuulizia habari zake wala mambo ya mimba, baada ya muda binti alimtafuta mtoto akiwa na mwaka na miezi miwili hivi, jamaa alishapoteza kabisa hamu hata ya kumuona ila alimwambia kuwa mtoto ni wake na alimtumia picha, kwa kulazimisha kuwa mtoto anafanana naye, jamaa alikwenda kumuona mtoto lakini alikuwa na mashaka kwani huo mfanano aliodai mama mtoto hakuuona kivile akajipa mooyo labda akikua atagundundua, walirejesha mahusiano lakini sio kama ilivyokuwa awali, baada ya muda aligundua kuwa yule baba alikuwa anahudumia kila kitu hadi kodi ya nyumba na anafahamika hadi kwa mama yake binti!alopodai kadi ya mtoto hakupewa na aliamua kumwaga manyanga jumla jumla! hakuwahi kukutana na huyo baba mwingine na wala hamfahamu, binti amekuwa akimshumbua mara kwa mara kudai hiki na kile lakini jamaa amegoma kabisa na hataki hata kumuona mtoto tena!!...kina dada hebu waoneeni huruma watoto...khaaaaaaaaaaaa
 
[Pole Sana kaka kwa mchezo uliofanyiwa na huyo mwanamke, mwambie kama kweli mtoto ni wako mwende mkapime DNA ukiona anaanza drama nyingi kimbia sana maana yeye na mama yake wamewafanya vitega Uchiha vyao
 
We nae kwaiyo garama za shule na dna kipi expensive? Acha utoto dna ni laki 5 na kwa sasa haina mlolongo unaweza kuongea na dr na akapima akakupa majibu. Chukua unywele wa mtoto unatosha.

Option 2 ya kimila muite mama aje na mtoto. Mtoto akilala usingizi toa dushe mpige kichwani kama ni wako ataendelea kuishi, kana umefanyiwa ukanjanja anakufa hapo hapo. Chaguo ni lako.
 
The only way out hapa ni DNA TESTING OF THE CHILD, MOTHER AND BOTH OF THE FATHERS!!!
Sioni jinsi nyingine yoyote hapa ya kumaliza huu mgogoro zaidi ya DNA!! Process ya hii kitu kama ukiamua siyo ndefu kivile compared na umuhimu wa hii kitu!!
Mtafute huyo mwenzio au mtu wake wa karibu anemuheshimu ongea nae kiume kwamba wewe unachotaka ni kumaliza huu mgogoro once and for good mambo mengine yaendelee.
Mnaweza/unaweza pia kwenda kwa mwanasheria na kumuomba ushauri wa kisheria kuhuu legal procedures za kufuata ili kuweza kufanya DNA.
Nime copy na ku paste hapa chini sub-section ya "THE HUMAN DNA REGULATION ACT OF 2009" Ya hapa kwetu kujaribu kukusaidia uanzie wapi ili kufanikisha hilo.

23. The samples for Human DNA shall be collected and analyzed forthe purpose of establishing parentage, kinship, criminal investigation,Human DNA Regulationresearch in population genetics, medical, pharmaceutical, chemical andnutrition assessment.24. The samples for Human DNA shall be collected by samplingofficers and analyzed by the Human DNA Laboratory of the GovernmentChemist Laboratory Agency or other designated laboratory for HumanDNA.25.-( 1) The analysis of sample for Human DNA shall be initiated by awritten application by the requesting authority to the Human DNALaboratory of the Government Chemist Laboratory Agency or designatedlaboratories for Human DNA.(2) For the purpose of this Act the requesting authority shall be:-(a) the court where the subject matter is in dispute between theparties;(b) advocates of the court of law, Social Welfare Officers andcommunity development officers for law matters which arenot in dispute;(c) a Police Officer of or above the rank of inspector;(d) research institutions that are mandated to conduct researchin Human DNA;(e) a District Commissioner in the case of a mass disaster; or(f) medical practitioner for medical cases.
Pole sana brother kwa haya yanayokukuta, jitahidi umalize huu mgogoro kiume baptiste

dr ushauri huu ni mzuri sana ila kama mama(huyo bint) hakatai kupima kwani kuna sheeda gan? Hii hutumika iwapo mama anakataa wasipime DNA. atumie njia ya kumushawishi binti hakubali wapime kwa hiyari mahakama wana mambo mengi yatamuhalibia kazi na kwa mwendo huu mtoto sio wake. So asitumie gharama nyingi itamkost na mwisho dna itaonesha tofauti.
 
Last edited by a moderator:
Kuna huyu binti ambae takribani miaka saba iliyopita tulikua wapenzi, katika miezi 2 ya uhusiano akaniambia ana mimba yangu, wakati huo nilikua ndio nimepata kazi, miezi 6 ya ujauzito wa huyo binti akatokea jamaa mwingine na kudai ile mimba ni yake

Kwamba binti alimwambia hivyo tangu mimba changa, hivyo akaniambia nisisumbuke mimba ni ya kwake yeye, nikaizira mimba na kumwambia binti mimi basi sitaki tena, ambapo kwa ugomvi huo alipata complications na kulazwa

Nilisusa hivyo hadi mtoto alipozaliwa binti na mama yake wakanibembeleza sana nikamuone mtoto kwamba yule jamaa mwingine ni muongo alifanya vile kwa kuwa alikataliwa, nikaenda, nikapata Wazo la kuomba tangazo la kuzaliwa mtoto linalotolewa hospt, wakaenda chumbani binti na mama yake, mtoto nikabaki nae ukumbini, walikaa huko nusu saa nzima wakibishana

Walipotoka wakaja na tangazo likiwa tayari na jina la mtoto, lakini lile jina limefutwa kwa wino wa kukandamiza kabisa halisomeki tena, nikawahoji kulikoni, wakadai yule jamaa alikuja na ndugu zake bila mwaliko na wakaomba tangazo na kujaza jina bila ridhaa ya wahusika, ndio maana wamelifuta jina
Ila nilipotazama vizuri nikaona ule wino ni kama wa muda huo huo, nikapotezea baadae nikaondoka

Miaka 2 mbele ugomvi ukawa mkubwa, ambapo tuliitwa kwao na msichana pande zote, mm, jamaa na ndugu zake Mshikaji, demu alipoulizwa amtaje baba wa mtoto wake akanitaja mm, yule jamaa aliinuka kwa hasira na kuwauliza mbona kwa miaka yote miwili vitu vyangu huwa mnapokea, maziwa, vyakula, mavazi na kadhalika?

Mama mtu akamjibu kwa hiyo ulitaka tukuzuie? Wakati umependa mwenyewe kuleta?Ikafikia hatua yule jamaa akaanza kulia machozi kwa uchungu sana, akisema wanataka kumdhulumu mtoto kwa kuwa hana maisha yanayoeleweka, kwamba hawezi kukubali, wakaondoka na watu wake, nilipata mapya siku hiyo ambayo sikuyajua nyuma, wakanibembeleza sana nikaondoka kwa hasira, nikawasusa mwaka mzima

Baada huo mwaka nikapokea sms kutoka kwa huyo binti kwamba mtoto amefariki, kwamba """ ulimsusa mtoto na kumkataa sasa furahi amefariki"" nikaone nipige simu ikawa haipokelewi, hadi nawapigia hadi kwa kubadili namba hawapokei, nikapata Wazo nikampigia mama MTU,
Akashtuka sana akasema hakuna aliekufa," baba hatuna msiba na wala mtoto hajafariki, huyu mwenzio ana hasira tu kachanganyikiwa, nikashangaa sana G amepatwa na nn kufikia hatua kusingizia mtu kifo

Kwa kifupi, niseme tu kwamba sijawahi kumpenda huyo mtoto wala kuwa na affection nae kutokana na hiyo historia niliyowaeleza, kuna roho huwa inaniambia mtoto ni wa yule jamaa, asilimia 70% roho inadai hivyo, ndio maana sina mapenzi na huyo mtoto
DNA kwangu sio muhimu, muhimu ni affection, DNA haiwezi kuleta Upendo kwa mtoto, roho yangu Ilishatumbukia nyongo ni vigumu kuibadili

Kuna wakati nilijaribu kuangalia hiyo DNA inakuaje na taratibu zake, niligundua sio jambo rahisi kama watu wanavyodhani, lina mlolongo mrefu mno na expensive, wakati mwingine hadi mpelekwe pale na barua ya mahakama.

Bahati mbaya mtoto hafanani na sisi anafanana na mama yake copyright, sasa limekuja suala la shule, mwakani mtoto anaanza standard one, wanadai wanahitaji gharama za utaratibu mzima, cha kushangaza kwa miaka yote hii yule jamaa pia anapeleka gharama mbali mbali, na si ajabu hata la shule labda wamemwambia, huwa Nina mtoa taarifa wangu kwenye hiyo familia.

Wakati ule anajifungua niliazimia kumuoa huyu binti, lakini baada ya sintofahamu iliyojitokeza nilifuta kabisa wazo hilo, na hadi Leo bado sijaoa.

Kwa historia hii niliyowaeleza mnadhani huyo mtoto anaweza kuwa wa kwangu kweli? Na sio wa huyo jamaa?

Tatizo lako wewe ni kuzira na kususa. Mwanaume huwa hasusi anatafuta suruhisho la kudumu. sasa wewe unasusa, unazira na ndio maana tatizo limeendelea kwa zaidi ya miaka mitatu sasa
 
dna ya nini unang'ang'ania mtoto kijana kabisaa msomi au domo zege we kama unashida ya mtoto mpe mimba au tafute mwanamke mwingine zaa naye kama wewe ni mgumba unaweza ukaendelea kung'ang'aninia kiukweli nimekuona zuzu sio jambo la kuja kuomba ushauri wee achana nao. nabaadae ukienda dna ukaambiwa sio wako utafanyaje
 
Ushauri walioutoa watu hapa wa kupima DNA usiupuzie, kapime DNA kwa process yoyote ilivyo ili ujihakikishie wewe na nafsi yako kwamba kweli mtoto siyo wako au ni wa kwako.

Unaweza baadae ukaja kujua ukweli huku umeshachelewa na huna jinsi ya kumsaidia huyo mtoto.
 
Dah hawa viembe wa ubavu wetu, isingekua wanatuweka miezi 9 tumboni na kutuzaa kwa uchungu hakuna mtu angewaheshimu hii dunia kwa mambo wanayotufanyia ila basi tu mungu ana makusudi yake. Mkuu ushauri wangu kapime tu DNA kama sio mtoto wako achana nae kabisa uyo mwanamke inabidi ajute kukukosa ili ajue umuhimu wa kuwa mkweli.
 
nikwambie kitu ...........hata baba yako ana wasi wasi na wewe kama kweli ulitokea maungoni mwake lakini alikulea na kukutunza mpaka umepata akili ya kuandika haya uandikayo ...........umesema kweli d.n.a is nothing .........go and love that kid man! au wajiona utabaki kuwa kijana milele?

nakushauri umpende tu mtoto na ondoa negatives zote ..........ukiamua vinginevyo jiandae pia kuziishi gharama zake ...yep.........katu usijidanganye kuwa kipimo kitakuletea amani ya moyo! na kuitwa baba sio lazima ushiriki kuchangia mbegu!
 
U don't have elders in ur family? Zamani wazazi hawakuwa na DNA walitumia mabibi, babu, shangazi kukagua mtoto! Just tell ur mother wakimchukua mtoto wanamkagua kucha, kichwa na vidole watatoa majibu sahihi! U can't handle it by itself they will play u like remote control! Seems familia iyo ina njaa wanatumia mtoto kuwa cage wote wawili.
 
Back
Top Bottom