singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Nimejipa kazi ya kuwa mtumbua maji
JAMBO moja nililolisemea kwa nguvu kubwa wakati wa kampeni ni mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Sikufanya hivyo kwa sababu nilitaka tu kuwarubuni wananchi ili wanipe kura zao na kunifanya kuwa Rais wao. Nililiongea jambo hili kwa dhati kabisa, na nilichokisema na kuwaahidi wananchi ndicho hasa nilichokikusudia.
Wananchi wanachukia sana rushwa na ufisadi, na wamechoshwa na vitendo hivyo. Mimi pia ninachukia rushwa na ufisadi. Sifurahishwi kabisa na vitendo vya rushwa na ufisadi vinavyoendelea hapa nchini. Vitendo vya rushwa na ufisadi vinawanyima haki wananchi na kuitia hasara serikali kwa mamilioni ya fedha ambazo zingeweza kutumika kwa ajili ya kujenga miradi ya maendeleo kwa ajili ya watu wetu.
Chama changu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimejengwa katika misingi ya kukataa rushwa na ufisadi. Ndiyo maana moja ya imani kuu za CCM ni ile isemayo: “Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala kupokea rushwa”.
Kwa Mtanzania mwaminifu kwa imani yake hatakuwa na kigugumizi katika kuwa mstari wa mbele katika kupambana na rushwa na ufisadi. Akiongea bungeni Mei 1960, Mwalimu Nyerere alisema yafuatayo kuhusu rushwa: “Rushwa (na ufisadi) havina budi kushughulikiwa bila huruma kwa sababu naamini wakati wa amani rushwa na ufisadi ni adui mkubwa kwa ustawi wa watu kuliko vita.”
Haya ni maneno makali ya mtu na kiongozi aliyeichukia na kuikemea rushwa katika maisha yake yote ya uongozi. Ni maneno yanayotukumbusha tu nini kinaweza kikatutokea kama taifa endapo tutaendekeza rushwa na ufisadi. Chuki za wananchi dhidi ya rushwa na ufisadi ni dhahiri, wamechoka kabisa, wamechoka sana, hawako tayari kuvumilia upuuzi wa serikali itayoonea haya rushwa na kulea mafisadi.
Mimi nimewaahidi wananchi, na nataka niirejee ahadi yangu kwao mbele ya Bunge lako tukufu, kwamba nitapambana na rushwa na ufisadi bila kigugumizi na bila haya yoyote. Dawa ya jipu ni kulitumbua, na mimi nimejipa kazi ya kuwa mtumbua jipu.
Najua kutumbua jipu kuna maumivu lakini bahati mbaya halina dawa nyingine. Hivyo ninaomba Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote mniombee na muniunge mkono wakati natumbua majipu haya.
Ninafahamu ugumu wa vita niliyoamua kuipigana. Nasema nafahamu ugumu na changamoto zake kwa sababu wanaojihusisha na rushwa sio watu wadogo wadogo. Vitendo vya rushwa na ufisadi vyenye madhara makubwa kwa nchi na ustawi wa nchi yetu hutendwa na watu wenye dhamana kubwa za uongozi na utumishi ambazo wamezipata kutokana na ridhaa ya watu.
Kwa hivyo ili niweze kufanikiwa lazima nipate ushirikiano mkubwa toka kwa Bunge na vyombo vingine vilivyopo na vyenye majukumu ya kupambana na vitendo hivi. Aidha, tutashinda vita hii endapo wananchi pia watatuunga mkono. Sina mashaka kuwa kwa vile wao, kwa wingi wao, wanachukia rushwa na ufisadi, watakuwa tayari kutoa ushirikiano wao katika mapambano haya dhidi ya rushwa na ufisadi.
Katika kushugulikia tatizo hili nimeahidi kuunda mahakama ya Rushwa na Ufisadi. Ni matumaini yangu vyombo husika katika jambo hili havitanikwamisha. Aidha, nataka niahidi kwamba kiongozi yeyote wa kuteuliwa, ambaye mimi nitakuwa nimemteua kwa mamlaka niliyonayo kikatiba, na ninayo mamlaka ya kumwajibisha, pindi tu nikibaini na kujiridhisha kuwa anajihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi nitamtimua mara moja.
Baada ya mimi kuchukua hatua hizo hatua na taratibu zingine za kisheria zitafuata. Mheshimiwa Spika; Ninachotaka kusema ni kuwa Serikali yangu itafuatilia kwa karibu mienendo ya viongozi na watendaji wake ili kubaini kwa haraka nani anajihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi. Na tukishajiridhisha hatutasubiri, tutachukua hatua. Ni imani yangu wengine pia katika ngazi mbalimbali mtafanya hivyo.
Kwa sababu bila kufanya hivyo, rushwa na ufisadi vitazoeleka na kuwa wimbo unaoburudisha badala ya kuudhi na kukera.
Nilipokuwa nazunguka na kuzungumza na wananchi wakati wa Kampeni za Uchaguzi, niliahidi kuwa nitaunda serikali ndogo ya wachapa kazi. Aidha, niliahidi pia kuunda serikali ambayo itawatumikia watu na hasa wananchi wa kawaida. Serikali nitakayounda, nataka iwe inawahudumia wananchi kwa haraka na sio kuwasumbuasumbua na kuwazungusha.
Natoa rai kwa watumishi wa serikali, hasa ambao ni wazembe na wavivu, kujiandaa. Wamevumiliwa kwa muda mrefu sasa basi. Kwa sababu watumishi wa aina hiyo hawatavumuliwa katika serikali nitakayoiongoza. Lugha za “hiyo ni changamoto tutaishughulikia”, au “Mchakato unaendeela” hazitavumiliwa katika Serikali ya Awamu ya Tano.
Mimi nataka watu wa Kazi Tu. Hatuwezi kulea watu ambao wanalipwa mishahara lakini hawafanyi kazi wanazotakiwa kufanya, au wamegeuza ofisi za umma kuwa ni mahala pa kuchuma bila kufanya kazi. Pamoja na kuwataka watumishi wa Serikali kufanya kazi hatuna budi kuyaangalia na kuboresha mishahara na maslahi yao na mazingira yao ya kufanyia kazi kwa kuwapatia vitendea kazi bora na vya kisasa.
Hii ni sehemu ya hotuba ya Rais John Pombe Magufuli wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 Novemba 20, 2015
Chanzo: Raia Mwema

Last edited by a moderator: