Pole mwenzangu pamoja na elimu yako jambo dogo lakushinda. Mie nilibambikiwa kesi na jamaa yangu Wa karibu kisa wivu Wa kibiashara. Akaenda kunifungulia kesi eti ni mmemtukana matusi na nimmemtishia kumtoa roho.
Kwenda polisi kachukua maelezo yangu mda wote huu, nimewasha iPhone yangu na chukua video taratibu Hana habari. Wazo langu ni kuwa akiteleza kutaka Rushwa ili asiniweke lockup, niwe na ushahidi.
Mwisho Wa siku Ana niuliza je umekuja na wadhamini maana ina bidi nikueke ndani ilikuwa ijumaa ili jumatatu nikupeleke mahakamani.
Ni kwamwambia nitajidhamini akakataa kwa sababu ya hasira ni kasema poa ni weke ndani hadi jumatatu.
Gafla si akatamka SIKILIZA RAFIKI MIMI NIKOTAYARI KUKUSAIDIA JE WEWE UTANISAIDIAJE. NIKAMWAMBIA WE NIPE TERMS. NIPE KITU KIDOGO RAFIKI KUMBUKA LEO IJUMAA UTAPATA SHIDA. JE ULITAKA KIASI GANI? KADAI LAKI MOJA NIKAMWAMBIA POA. Baada ya hapo banduku nikazima kamera. Nikaplay ile video na kuongeza sauti akawa anajisikia sauti yake akastuka vipi ni MIMI HUYO! Nikamwambia ndio subiri usikilize hadi mwisho. Ilivyokuja issue ya kuomba hela si aka shangaa Kama vile kapigwa shock ya Umeme.
Akanisihi nifute na pili niondoke nisije mwaribia kazi.
Sasa jamaa yangu akaenda jumatatu kujua kilicho jiri jamaa kamfokea anadai umeniletea mashushu waje ni haribia kazi hebu achana na Mimi.
HUO UKAWA MWISHO WA KESI YANGU.