Huyu mwanamke nilisoma naye shule ya msingi ila alikuwa nyuma yangu. Alinifahamu vizuri kwani nilikuwa vizuri darasani ila mimi sikuzoeana naye. Nilikutana naye miaka mitatu iliyopita baada ya kuachana kwa miaka mingi. Yeye ameshaolewa na sasa hivi anafanya biashara na mumewe. Tulibadilishana mawasiliano kama watu tunaofahamiana lakini kilichotokea mpaka leo kinanisumbua. Alianza kunitumia msg za mapenzi na kunipigia simu mara nyingi. Kuna siku alikuja kwangu bila taarifa. Nilipotoka kwenda kuoga nikarudi na kumkuta chumbani kwangu uchi. Kama binadamu niliingiwa na kuzidiwa na tamaa nikazini naye. Toka hapo amekuwa akiniambia anataka azae na mimi ili apate mtoto atakayekuwa na akili kama nilivyokuwa mimi. Niliamua kukata mawasiliano naye na kuhama pale nilipopanga mwanzo bila mafanikio.Nikimblock anatafuta laini nyingine na kunipigia. Nimebadili line mara tatu bila mafanikio. Anadai kwa nini namtesa namna hiyo? Ushauri wenu ndugu zangu!