Wakuu habari za mchana na
Wana was Mudi Asalam aleikhum......
Kama heading inavyosomeka mpaka mda huu nimefura kwa hasira natamani kila kitu nnachokiona mbele yangu nikipasue pasue.
Stori iko hivi;Jana majira ya sa tatu nilianza kuchati na kimwana mmoja niliyekutana nae Eid akanipa namba yake. kusema ukweli mtoto yule kajaaliwa uzuri ulitukuka ana bonge la msambwanda ni hatari yani kiujumla ni mrembo wangu wa dunia.
Toka anipe namba sikuwahi kumtafta ila ye Jana usiku kanitafta huku akinilaumu kwa nini sijamtafta toka anipe namba, (si unajua teknik za wakwere tukipewaga namba huwa tunakausha siku tatu afu ndo tunaanza mashambulizi)
Sasa baada ya kujitetea kidogo tukaendelea na maongezi mtoto nkamtia vokali(vocals) akajaa mzima mzima kidume nkashangilia kwa nguvu getoni kwangu nkachukua glass ya maji nkanywa kujipongeza kwa kumsajili nyota mahili ndani ya kikosi changu tena bila dau.
Tukaendelea na maongezi mtoto akadai anataka aje kwangu ili nimuone alivyojaaliwa make anadai huenda siku ile sikumuona vizuri basi nkamwambia ajifeel free kwanj mi ni bachelor naishi alone, basi mtoto akapendekeza tufanye kesho asubuhi maana wazazi wake wanaamkia safari ya mbali na watarudi baada ya siku mbili, basi nkasema haina noma maana toka juzi Niko off, nkamuelekeza mitaa nnayokaa akaielewa na akanisisitiza Nile ugali wa maan(nkajua kesho ni Eliclasico ya hatari).Mzee nkamwambia poa tukaishia hapo baada ya kumaliza nkaamua kulala huku nikiomba pakuche mapema.
Leo nimeamka sa 12 nkapanga geto langu likapendeza nkaenda kununua vitafunwa na madikodiko kibao ili mtoto akija akute kila kitu kiko poa.
Saa 2 mtoto akanipigia simu kuwa ameanza safari basi kidume nkafurahi nkaanza kuzunguka ndani huku napiga mluzi(furaha iliyoje). Mida ikazidi kwenda nkaona mtoto hafiki nkavumilia nkasema labda njiani kuna foleni nkamtext hajibu text nkampigia akapokea akasema anakaranakaribia kishuka, nkajipa hope.
Ikafika sa 5 mtoto hafiki nkapiga simu akikata nkajipa hope nkajua labda yupo kwenye kelele nkasubiri wapi, nkituma text hajibu ikaenda mpaka sa 7 basi ikawa kila nkipiga simu anakata.Mpaka mda huu hajapokea simu na sijui kinachoendelea yani mpaka naandika huu Uzi nmefura kwa hasira natamani kila kilicho mbele yangu nikivunje vuje .
Yani kati ya siku ambazo demu amecheza na akili yangu ni Leo.
Naomba kuwasilisha