Nimediriki kukataa Ndoa

Nimediriki kukataa Ndoa

Amos David Mathias

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2022
Posts
1,575
Reaction score
3,106
Ni siku chache zimepita baada ya kutoka Dubai matembezi ya kufurahisha macho kidogo.

Huku nyumbani nimekutana na Binti mmoja wa kingoni ambaye nilimpenda tokea Moyo ulipomwona Kwa mara ya kwanza.Nilihisi damu imechangamka ghafla na vipepeo wanatembea na kuruka ruka ndani ya tumbo baada ya kumwona Kwa mara ya kwanza.

Basi nikajisemea liwe liwalo ngoja nitupie nyavu.Nashukuru Sana mtoto wa watu kanikubalia japo Kwa mbinde.

Anadai amemaliza chuo ila anasubiri ajira sasa nilichoamua kumfanya ni kumweka ndani ya geto tuishi wote.Nachosikitika ni kuwa Anadai vitu vya gharama na anataka nimtreat kama Malkia.Namfanyia mengi lakini haridhiki.Nimeamua kujiengua haraka Sana kutoka kwake.Nimekataa kuwa mtumwa wake pamoja na kuwa mtumwa wa ndoa.

###KATAA NDOA

###NDOA NI UTAPELI
 
Oh boy!

Ulifahamiana naye kwa muda gani kabla hujamkaribisha kuishi naye ghetto? Pengine kosa lako lilianzia hapo.

Jaribu wengine watatu huku ukiepuka makosa ya waliotangulia. Hatimaye utampata mke mwema atakayekupa ndoa yenye furaha kama nawe uko tayari kupewa ndoa yenye furaha.

Umebwaga manyanga mapema sana kamanda
 
Hajakupenda kama unavyompenda wewe.

Tafuta mwanamke ambae amekupenda wewe zaidi ya unavyompenda yeye, ukimpata wa hivyo hata kukuomba pesa ndogo tu hua wanajishtukia.

Ukifanikiwa kumpata wa hivyo muheshimu na mtunze asipotee. Utakua umeyapatia maisha ya ndoa. Kinyume na hapo ni mateso tupu.
 
😀😀
Mnaingia kwa pigo za "akipendacho binti" matumizi yakizidi mnalia.
Kama hukiwezi kifukuze , tafuta mnayewezana
 
Uzi wa kitapeli sana.Umeshindwa kumnunulia alichotaka?Kwani ni bei gani?Haukurudi na mapesa?Au ulikuwa umeenda kufanya kazi za ndani huko ulipoenda?
 
Na hii kampeni ya KATAA NDOA inavyotrend mtu hata akinyimwa namba atakimbilia kuanzisha uzi huku!!
Au akijibiwa ambavyo hakupenda 😂😂😂 mbio Jamii Forum.
 
Ni siku chache zimepita baada ya kutoka Dubai matembezi ya kufurahisha macho kidogo.

Huku nyumbani nimekutana na Binti mmoja wa kingoni ambaye nilimpenda tokea Moyo ulipomwona Kwa mara ya kwanza.Nilihisi damu imechangamka ghafla na vipepeo wanatembea na kuruka ruka ndani ya tumbo baada ya kumwona Kwa mara ya kwanza.

Basi nikajisemea liwe liwalo ngoja nitupie nyavu.Nashukuru Sana mtoto wa watu kanikubalia japo Kwa mbinde.

Anadai amemaliza chuo ila anasubiri ajira sasa nilichoamua kumfanya ni kumweka ndani ya geto tuishi wote.Nachosikitika ni kuwa Anadai vitu vya gharama na anataka nimtreat kama Malkia.Namfanyia mengi lakini haridhiki.Nimeamua kujiengua haraka Sana kutoka kwake.Nimekataa kuwa mtumwa wake pamoja na kuwa mtumwa wa ndoa.

###KATAA NDOA

###NDOA NI UTAPELI
Sawasawa
 
Kuna mojawapo kati ya haya mawili; Aidha kuoa au kuolewa.
 
Mwanamke anayesema "nataka unitreat kama Malkia" ukimuoa amini ya kwamba atachakatwa na wajinga wajinga wengi sana
 
Hajakupenda kama unavyompenda wewe.

Tafuta mwanamke ambae amekupenda wewe zaidi ya unavyompenda yeye, ukimpata wa hivyo hata kukuomba pesa ndogo tu hua wanajishtukia.

Ukifanikiwa kumpata wa hivyo muheshimu na mtunze asipotee. Utakua umeyapatia maisha ya ndoa. Kinyume na hapo ni mateso tupu.
Utajuaje kuwa anakupenda kwa dhati? Mkuu hawa viumbe kwa kuigiza ni hatari.
 
Uzi wa kitapeli sana.Umeshindwa kumnunulia alichotaka?Kwani ni bei gani?Haukurudi na mapesa?Au ulikuwa umeenda kufanya kazi za ndani huko ulipoenda?
Mtu akiwa na pesa si kwa ajili ya mipango aliyonayo na kuishi anavyoweza? We unaijua chuma ulete ya wadada wa mujini au unasema tu? Atajikuta amebaki anamili p...u..mb....u tu
 
Kama hela yako haipo kwenye mipango ya akina dada,kaa utulie na ufanye mambo mengine.Kutaka vitu vya bure ni kuchanganyikiwa huku umevaa kwa kupendeza barabarani.
 
Ni siku chache zimepita baada ya kutoka Dubai matembezi ya kufurahisha macho kidogo.

Huku nyumbani nimekutana na Binti mmoja wa kingoni ambaye nilimpenda tokea Moyo ulipomwona Kwa mara ya kwanza.Nilihisi damu imechangamka ghafla na vipepeo wanatembea na kuruka ruka ndani ya tumbo baada ya kumwona Kwa mara ya kwanza.

Basi nikajisemea liwe liwalo ngoja nitupie nyavu.Nashukuru Sana mtoto wa watu kanikubalia japo Kwa mbinde.

Anadai amemaliza chuo ila anasubiri ajira sasa nilichoamua kumfanya ni kumweka ndani ya geto tuishi wote.Nachosikitika ni kuwa Anadai vitu vya gharama na anataka nimtreat kama Malkia.Namfanyia mengi lakini haridhiki.Nimeamua kujiengua haraka Sana kutoka kwake.Nimekataa kuwa mtumwa wake pamoja na kuwa mtumwa wa ndoa.

###KATAA NDOA

###NDOA NI UTAPELI
Dalili ya ushoga
 
Mama muuza lete chapati mbili, chai ipo tayari...
 
Back
Top Bottom