Nimebaini: Wengi hushiriki shughuli za kiimani ili wasikataliwe kuzikwa, ni ‘black mail’ fulani hivi

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,066
40,725
Katika udadisi wangu wa kina na wa muda mrefu, nimebaini kitu ambacho nimekuwa nikikihisi toka niko mdogo.

Zile mbinu za kutishia watu wazima nyau kwamba utaenda motoni au kwamba utaenda kunywa maziwa na asali pamoja na malaika zinaanza kukosa mashiko kwa sasa. Hata yale mawazo ya kipuuzi ya kwenda kupewa wanawake waremho mbinguni kama zawadi ya kufanya jambo flani la kiimani pia imeanza kukosa mashiko.

Kiufupi ushiriki wa wanaojiita waumini wa imani mbalimbali ni ili waweze kuzikwa siku watakapofariki. Na ili kuwatisha zaidi, uongozi wa imani zao umekuwa ukionyesha mifano ya kukataa kuwazika wale ambao wamekataa kuwa ‘extorted’ na mfumo husika wa kiimani, ila wao utasikia wakisema ‘hatumziki sababu alikuwa hashiriki......’, kumbe ukifuatilia utakuta walimuomba mchango wa kununua gari la kiongozi flani wa kiimani akakataa ndio inakuwa kama adhabu hiyo.

This is black mail.
 
haulazimishwi wala hautishiwi, wewe ndiyo una uamuzi wa kuyafuata au kutokuyafuata.

Wamekueleza ukiyafuata utapata faida hizi na usipofuata utapata hasara hizi then unaachwa ufanye uamuzi wako.

Hapo hakuna blackmail unless tuna uelewa tofauti juu ya maana ya hilo neno.
 
Sasa hiyo description uliyotoa hapo juu si ndio blackmail yenyewe, mwishowe wataanza kusema asiyeenda kupiga deki choo cha nani sijui hazikwi 😂😂😂
 
Sasa hiyo description uliyotoa hapo juu si ndio blackmail yenyewe, mwishowe wataanza kusema asiyeenda kupiga deki choo cha nani sijui hazikwi 😂😂😂
kwa maana yako hiyo, unapoambiwa kwa mfano ili uwe Rais lazima uchaguliwe kwa zaidi ya asilimia hamsini za kura napo unaona ni blackmail.

Kwamba ili upewe kazi fulani lazima uwe hivi na hivi na hivi nayo ni blackmail! Ili uwe mtu wa fani ya aina fulani unatakiwa usomee moja mbili tatu nayo ni blackmail! Mkuu rudia kutafakari uelewa wako juu ya hilo neno.

Ili uwe mwenzao lazima ufanane nao au at least uwe na sifa kama zao including common interests. Sasa kama wenzio wanataka lazima utoe michango na wewe hautaki automatically unakuwa siyo mmoja wao.

Na that being the case usiwalazimishe wakuzike, acha wawazike wenzao.
 
Mantiki na dhima nzima ninayoizungumzia ni ile ya kukomoana na kutoleana mifano ili kuwatisha walio hai, haiwezekani kila siku ni michango ya kununulia watu magari ya kifahari tu, na wanaong’ang’ania hiyo michango ndio hao hao viongozi walioshika mpini wa nani azikwe na nani asizikwe, sasa si blackmail hiyo, mgongano wa maslahi huo, hata ingekuwa mimi ningedai waninunulie helicopter, atakaekataa kunichangia, hakuna kumzika!! kwa mtindo huo wacha tuzikwe na watoto wetu tu, hii ifike mwisho!😂😂
 
Mantiki na dhima nzima ninayoizungumzia ni ile ya kukomoana na kutoleana mifano ili kuwatisha walio hai, haiwezekani kila siku ni michango ya kununulia watu magari ya kifahari tu, kwa mtindo huo wacha tuzikwe na watoto wetu tu, hii ifike mwisho!😂😂
Mungu ametupa akili na utashi wa kujua mema na mabaya ili tufanye maamuzi sahihi. Kwahiyo matumizi ya akili ni ya msingi sana katika imani.
 
Mungu ametupa akili na utashi wa kujua mema na mabaya ili tufanye maamuzi sahihi. Kwahiyo matumizi ya akili ni ya msingi sana katika imani.
Sawa, hakuna aliyebisha hilo. Ila tatizo ni mgongano wa kimaslahi unaopelekea blackmail kwa waamini. Unakuta mtu hataki ajengewe nyumba ya kawaida, anataka ajengewe rosheni moja ili awe juu karibu na Mungu, basi hapo inaanza kutangazwa michango minne kwa jumuiko moja, tena wakijua unachochote wanakutaja hadi jina ili utoe ahadi yako kabisa mapema, ukigoma unawekewa kinyongo, mwisho wa siku hata kwenda kwenye hiyo mijumuiko inakuwa shida na hapo ndio balaa la kutozikwa linakuangukia, tena wanapublicise kabisa ili iwe fundisho kwa wote wanaotaka kugomea unyonyaji wa aina yoyote ule, no way!!😝😝
 
Sijasoma thread yote
Lakini kwa kifupi ni Kwamba
WAISLAMU wanazika mtu yeyote Yule atakaekuja mbele yao hata kama Sio Muislam, hata kama Ni mlevi kupindukia, hata kama Ni Malaya,hata Kama ni Shoga, nk
Sababu Kujudge ni kazi ya Mungu, sio ya binadamu. kisa kakosa Nissan Patrol V8 new model, ndio wanawamalizia hasira wafu wasio jua hili wa lile
 
Sawa, hakuna aliyebisha hilo. Ila tatizo ni mgongano wa kimaslahi unaopelekea blackmail kwa waamini. Unakuta mtu hataki ajengewe nyumba ya kawaida, anataka ajengewe rosheni moja ili awe juu karibu na Mungu, basi hapo inaanza kutangazwa michango minne kwa jumuiko moja, tena wakijua unachochote wanakutaja hadi jina ili utoe ahadi yako kabisa mapema, ukigoma unawekewa kinyongo, mwisho wa siku hata kwenda kwenye hiyo mijumuiko inakuwa shida na hapo ndio balaa la kutozikwa linakuangukia, tena wanapublicise kabisa ili iwe fundisho kwa wote wanaotaka kugomea unyonyaji wa aina yoyote ule, no way!!😝😝
akili kumkichwa.
 
Kuna haja gani ya kuhofia kutokuzikwa wakati tayari umeshakufa yaani mzoga?

Kauli yako haina mashiko kwa kua kama suala ni kuzikwa na si kuzikwa kidini wapo wahuni wa kufukia chap chap kwa buku 20 mnamalizana au hata manispaa

Watu bado wana hofu ya dini, na wanaamini huo moto si propaganda ni ukweli kwa kua Mungu aliweza kuwaumba wao atashindwaje kuumba moto
 
Back
Top Bottom