Nimeamua nitafute mtoto kwanza

Chokochoko

JF-Expert Member
Oct 15, 2011
438
183
Heshima zenu wanajamvi wa mmu, bila shaka mnakumbuka post yangu ya nyuma kuhusu kuolewa nashukuru sana wengi wenu mlinitia moyo mkanifariji na mkanipa mawazo kemkem ya kusonga mbele, nilikua natafakari mambo mengi kwa muda wote ule na kuna jibu moja la maana nimelipata na litawafaidieni na nyie ni kwamba, upande juu ushuke chini KUNA KIPINDI MWANAMKE ANAHITAJI KUITWA MAMA usichana basi na anatamani jina lake libadilike si Sofia tena anatamani kusikia mama fulani, sasa basi nimeamu nitafute mtoto kwa udi na kwa uvumba bila kuwa na mume nimeamua kufungua ukurasa mpya wa maisha naenda zangu mbali nikiwa na maana ya kuama.

sitahiji uhusiano wowote na watu wa zamani wala comunucation wala rafiki wala shoga nabadilisha namba ya simu nafunga email yangu naenda kuanza upya marafiki na mashoga zangu mtanisamehe sana walio kuwa wapenzi wangu ndio kabisaaa hawatakaa wanisikia wala kuniona nimeamua ndio maisha mapya wa kuzaa nae nishampata kwa vile nimeona hana mwelekeo wa kuoa nikishabeba mimba tuu namtoroka hatakaa anisikie kwa chumvi wala kwa sukari ni mimi na mwanangu tuu, habari ndio hiyo
 
Well hongera!!
Hakikisha tu kwamba maisha ya umama utayaweza..being a good mother is not EASY!!
 
samahani sikusoma post yako labda utupe iyo link naweza changia vizuri zaidi...........
 
Kama umejifunga kisawasawa unaweza mtangulize mwenyezi mungu kwenye kila jambo lako na kila la kheir.....
 
mumeona iwanaume tulivyo 'miujiza' eeh? yaani mtu kukupa mimba yupo, mtu wa kukuondolea hamu yupo but mtu wa 'kukuoa' ndo hakuna.

Hakuna mwanamke 'anaekufa bikira'
fact...
 
mumeona iwanaume tulivyo 'miujiza' eeh?
yaani mtu kukupa mimba yupo..
mtu wa kukuondolea hamu yupo
but mtu wa 'kukuoa' ndo hakuna...
hakuna mwanamke 'anaekufa bikira'
fact...
wapo ndugu yangu,siku moja nilikwenda kumtembelea ndugu yangu pale katika hospital moja ya private,sasa katika kile chumba kilikuwa na wagonjwa wawili,baaada ya kumtambua hali bi dada ambaye alikuwa chumba kimoja na huyu mgonjwa niliyekwenda kumtembelea, huyu dada aliniomba nifanye naye mapenzi ili mradi asife na bikra yake, mie nikadhani ndio anaanza kuugua ukichaa,ila niligoma sikuafanya vile alivyotaka na yeye akaaga dunia.

Nalog off
 
wapo ndugu yangu,siku moja nilikwenda kumtembelea ndugu yangu pale katika hospital moja ya private,sasa katika kile chumba kilikuwa na wagonjwa wawili,baaada ya kumtambua hali bi dada ambaye alikuwa chumba kimoja na huyu mgonjwa niliyekwenda kumtembelea, huyu dada aliniomba nifanye naye mapenzi ili mradi asife na bikra yake,mie nikadhani ndio anaanza kuugua ukichaa,ila niligoma sikuafanya vile alivyotaka na yeye akaaga dunia.Nalog off

haya tuma salamu lol...
 
mmh! washawasha na ww lol!! ndo maana shangazi alikutembea mbovu kwa mkeo!!
lakini si inawezekana ikaharibika? mie ningemshauri asubiri mpaka atakapojifungua ndio aangalie ustaarabu mwengine.

shangazi kawa mtata sana sijui sababu ya uzee nimemuambia akakae hotelini,kagoma kasema haendi kokote na haondoki mpaka muda wake atakapokaribia kuisha ndio ataondoka.Nalog off
 
Sina uhakika sana kama staili hiyo ndiyo suluhisho, Maana huyo mtoto utakaye zaa still atakusumbua sana kuulizia baba yake kitendo ambacho kimsingi kitakurudisha kule kule ulikokukimbia.

Kukimbia tatizo si suluhu ya tatizo, unaweza kubaki na kufanya maamuzi magumu ya kubadili tabia na kutokuwachekea tena waliokutenda na bado ukawa na maisha mazuri ya kuheshimika huko baadaye.

Nashindwa kukushauri sana maana sikumbuki kisa chako cha mwanzo kilikuwa ni nini hasa ...
 
Angalia mbele kabla ya uamuzi wako maana iko siku utashndwa kujibu baadhi ya maswali toka kwa mwanao hadi ujutie huu uamuzi unaochukuwa leo.

Mfano akikuliza anataka amjue/kumwona baba yake sijui utamjibuje? Pili life is uncertain unaweza ukatangulia mbele ya haki wakati mwanao hajaweza kujitegemea huku hamjui baba huoni unajenga mazingira magumu kwa mwanao?

Tafakari kabla ya kutenda na kila unapoamua kufanya uamuzi fulani kumbuka lengo lako kwanza
 
Back
Top Bottom