Hapa ni kazi tu. Nimetumia utoto na ujana wanagu wote katika kupambana nikiwa mpinzani wa serikali iliyoko madarakani. Nakumbuka nilianza harakati nikiwa na umri wa miaka 16. Hiyo ilikuwa mwaka 1995. Hivi sasa mvi zimeanza kuniota. Pesa zimeniishia nikichangia katika kutafuta ukombozi feki. Ni mara nyingi nimekuwa katika hatihati ya kupoteza kazi yangu serikalini nikiwa natafuta ukombozi feki. Mapambano yetu yalikuwa ni kupinga ufisadi, Kutaa unyonaji wa watu wachache. Lengo kuu ya mapambano ilikuwa ni kuleta ukombo wa kiuchumi. Leo hii wakina Sumaye na Lowassa wanaotajwa kwenye kashfa nyingi za kujirimbikizia ardhi na ufisadi eti wamekuja kuungana na sisi kutafuta ukombozi. Hawa wanatuzuga hawa. Ngoja tupishane wao wanaingia na mimi ninatoka.
Leo hii CCM imetuletea Rais wa ndoto yangu. Rais mwenye kupinga unyonyaji. Mwenye kuwatetea masikini. Rais anayetaka kila mtanzania afaidike na nchi yake. Mtetezi wa wanyonge. Tunahitaji nini tena. Ni ukombozi wa namna gani tunahitaji watanzania wenzangu? Tunachopinga ni nini? Siwezi endelea kumpinga magufuli. Siwezi pinga maendeleo. Siwezi kuwa sehemu ya kurudisha nyuma maendeleo ya nchi yangu. Nitachapa kazi kwa bidii kumuunga mkono Rais wangu na chama changu kipya ccm. Kwani hata katika kupitia katiba nimeona ndicho chenye katiba bora kuliko vyama vingine vyote.
Kama upinzani ni kupinga kila kitu mimi sipo miongni mwenu. Narejea ccm. Wana ccm naomba mnipokee mimi mwana mpotevu. Sitorudi nyuma tena katika kuijenga nchi yetu na wala sitoibomoa. Nitafia ccm. Hapa ni kazi tu!!