Sukari Yenu
JF-Expert Member
- Dec 8, 2014
- 1,698
- 1,260
Habari wanajamii,
Nikiwa katika kutimiza majukumu yangu ya kazi nilifika katika nyumba za kanisa fulani. Shida yangu ilikua kufika nyumbani kwa mchungaji wa kanisa la mahali hapo.
Niliona mlango wa nyumba moja kati ya nyingi za mahali hapo upo wazi, nikasogea na kugonga. Nilisikia sauti za watu wakiongea lugha nisiyoielewa, nadhani kilikua Kitaliano.
Akatoka bint wa Kizungu age 15-17 hivi, wakati nawaza kumsalimia Kiinglish akaniwahi na "shikamoo" tena kwa unyenyekevu kama wafanyavyo wakwe zangu(wanyakyusa), kwa kubonyea kidogo.
I was surprised na nikaitikia kwa umaridadi kabisa. Ingekua hawa dada zetu wa kibantu (watoto wa mjini) asingeniamkia, kwa muonekano wangu.
Nikaeleza shida yangu akanielekeza nikamuuliza na jina akasema anaitwa Suzana.
My take,
Hawa watu wakija huku kwetu ni vema wafuate taratibu na mwenendo wetu na tuwafundishe norms and customs zetu. Sijui yule bint ana muda gani hapa Tz sababu anaongea Kiswahili kwa taabu kidogo. Kilichonifurahisha ni ile salam yake na niliona fahari ya Uafrika wangu kwa mara nyingine tena.