MR Kilimanjaro
JF-Expert Member
- May 5, 2019
- 249
- 364
Hata sipo mjini nipo kijijini mkuu na ni nyumbani piaFanya jitihada uhame uswahilini mkuu....
Wakuu salam
Leo asubuhi nimeamka vizuri nikawa nipo kijiweni tunapiga stori sababu mvua ilikua imenyesha hivyo nilikua sina kazi.
Nyumayangu akaja jaama ambae ni bubu na hasikii kama utani kanivua kofia ,na mm kama utani nikamtishia kumvua suruali na yeye akanianza kama kunipiga na mimi nikadhani utani, eh nikapata 1 nikakwepa ya 2 ahaaa nikaona hapa amna utani nikajibu mashambulizi sasa mimi namhurumia maana ni bubu na kiziwi watu wakamzuia mimi nikasogea kando maana sikutaka ugomvi nae bado akanifwata akanipiga ya sikio, dahh kaamsha mizuka yote nimempiga za uso za kutosha nikachukua na jiwe nikamwongeza la kichwa kazimia kama amekufa nimetimka hadi nyumbani nimefika nikajuta sana huu mkosi umenitokea wapi? Muda huo sijui kama nimeua au nitakamatwa?
Nilikosa majibu.
Nishanawa nimekaa eh mara namuona anakuja hado nyumbani nikajikoki nashangaa ananiomba msamaha
Kumbe wakati tunaparangana kule kijiweni majamaa wamenichomoa elfu 30 mfukoni
Wakamjaza upepo kua mimini mbaya nimeenda hom kuchukua panga, mara wanamwambia nimepoteza simu naenda kumshitaki
Ndio maana kaja kuniomba msamaha na ukicheki mimi mtaani ni mpole ila nikiwaga na hasira najulikana. Ila tumeyamaliza kiume tumekula pamoja na kunywa pamoja mambo yameisha ila kisirani nikibaya sana.
Sijui ningeua ingekuaje au ningefugwa.,
Mtu anaweza kukuletea balaa maisha yote
Hasa mazoea na utani kila mara
Inawezekana na wewe imesha wahi kukutokea tupe kisa tuzidi kuelimika na kuepuka mikosi kama hiyo.
Asante nashukuru mungu yamepita kila mtu anaugulia maumivu kivyakePole mzee ila nimejikuta nacheka sana. Kweli ni kisirani
Bado upo kwenye umri wa kupigana na watu ovyo kwa sababu za kijinga?????
Au huna kazi???
Kua uache
Mkuu nijifungie ndani kweli!Uache kwenda kukaa kijiweni
Unajua kupigana siku zote siyo jambo zuri. Jaribu kuepusha ugomvi kwa namna zote hata ukichokozwa. Hebu fikiria hilo jiwe kama lingempata sawasawa na akafariki! Wewe saa hizi ungekuwa unajuta na ingechukuwa muda mrefu sana kuja kuwa tena mtu huru (kama ungekuwa na bahati ya kupata hukumu ndogo). Kwa kifupi maisha yako yangekuwa kama yamefikia ukingoni. Nina uhakika ungejuta na kusema ''laiti ningekimbia japo alinianza yeye''.Mkuu mimi sipiganagi ila napiga na hadi nipige unakuta kweli ilibidi nifanye hivyo
Unajua kupigana siku zote siyo jambo zuri. Jaribu kuepusha ugomvi kwa namna zote hata ukichokozwa. Hebu fikiria hilo jiwe kama lingempata sawasawa na akafariki! Wewe saa hizi ungekuwa unajuta na ingechukuwa muda mrefu sana kuja kuwa tena mtu huru (kama ungekuwa na bahati ya kupata hukumu ndogo). Kwa kifupi maisha yako yangekuwa kama yamefikia ukingoni. Nina uhakika ungejuta na kusema ''laiti ningekimbia japo alinianza yeye''.
Tushamzoea kijiweni aliambiwa kwa ishara tu na nimwelewaNimecheka sana hapo ulipompiga na jiwe! Ila mzee alisikiaje hayo aliyoambiwa wakati ni kiziwi??
Sio kisirani mkuu huyo mtu kakuanza