X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,719
- 14,847
Duuh asee hakuna kitengo ninachokipenda na ninachokiona rahisi jeshini kama kwata huwa sielewi kwanini watu wanakichukia na kukiona kigumu
Yani mimi kwangu kwata ndio ilikuwa sehemu ya kupoozea machungu ya jeshi, maana mimi sipendi mabio wala mazoezi nakumbuka mwishoni mwa six weeks za kwanza, nilikosa kuwepo kwenye pass of square tu roho iliniuma sana
Nikasema kwenye graduu lazima niingie kitengo cha kwata, na kweli graduu nilikuwa kwata coy sema kimbembe kuweka silaha begani, hadi mfupa wa bega ukaanza kuuma nikawa naweka handkerchief
Yani mimi kiujumla jeshini vitu nilivyovipenda ni chenja, kwata, range (japo niliishia kulenga mijusi), syndicate na route march (kutembea tu), ila ukishaniambia nikimbie daah nilikuwa najionea tabu tu
Na yale maovyoovyo mengine nilikuwa siyapendi kabisa
Aisee na Numbisa ni mdada??JF warembo ni wengi sikuizi...Haha..
Mbona unachanganya jinsia zao?
Huyu naye siyo mzee, ni mrembo bro
Uandishi mzuri👍👍👍SEHEMU YA 7
Nashangaa muda unaenda mbona haturuhusiwi kwenda kulala?
Yule bakabaka akastopisha kwata akasema hivi sasa ni saa 2 usiku muda bado kabisaa! 😂
Kuruta tunaulizana muda bado kivipi akati tumetumia muda mwingi kombania.
kuruta wakisinzia wanapewa kazi ya kushindana kukimbia
Mimi sikua nasinzia nilikua najipa moyo muda simrefu tunaenda kulala ila wapiiiii.... kila muda bakabaka anasema ndo kwanza saa 2 kamili usiku.
Tunaimba chenja, mazoezi ya viungo kwenye mazoezi nilikua napenda viroba (squats) hata 100 nashuka tu nasihisi kuchoka. then bakabaka anasema hapohapo ulipo jilaze ulale! Basi watu fasta tunajilaza kwenye vumbi
Dakika 5 nyingi anasema inuka rukaruka kichura😄
Kuruta tulipata hasira hadi wengine wakaanza kusonya.
Hapa nilishangaa kitu! Kuruta anamsonya bakabaka halafu hafanywi kitu zaidi tu anasmile halafu anasema "kuruta fungua moyo huo"
Ila walikua wanaudhi fikiria mtu anakuambia lala ghafla ruka kichura anarudia mara nyingi zile hasira plus usingizi watoto wengine hawana adabu wanamsonya na yeye anablush tu.
Hamuwezi amini alfajiri ilifika tukishuhudia kwa macho! Sasa tunaulizana "mbona leo hatujaenda kulala?" Tutafanya nini ndo ishapita hiyoo😄
Tukapanga foleni mabio yakaanza, kama nilivyosema muda wa mabio niliupenda sana zile chenja ndo ugonjwa wangu nikawa nakimbia bila kutegea nafurahia kukimbia.
Tumerudi jogging uelekeo shambani, tukitoka shambani chai kuipata hadi ukimbie 2km, tukitoka chai uelekeo kwata
Sikupenda kwata nilikua nanga nimekula mabao mengi tu mpaka bakabaka akanichoka! Akaniambia labda utaweza vitu vingine kama ngoma coy, karate au kazi mchanganyiko.
Ratiba iliendelea mpaka wiki ikakata hatukurudi angani hatukulala wiki nzima!
Baada ya wiki sasa bila kulala! vituko vilianza mtu anachuma machungwa huku kafumba macho anaota kabisa😄
Mimi ile mabio nikawa nakimbia huku nasinzia, chenja naitikia miguu inaenda mbele lakini nimelala ila naota nakimbia.
Unaweza usiamini lakini hali ndio hiyo.
Bakabaka wakawa wanasema hawa itabidi leo wakalale wasije kutufia bure hapa!
Kitengo cha kuvuna machungwa tulikua tunapiga story sana na bakabaka.
Wiki ilipita bila kuoga.
Usiku ukafika mimi najua kabisa leo tunaenda kulala, nikawa na furaha , sasa muda unaenda ila haturuhusiwi, njaa ikawa inaniuma nikasema subiri nitoroke niende kunywa chai jikoni halafu nirudi fasta kombania nilihisi tulidanganywa leo tena tunakesha.
Lahaula nilijuta kwanini nilitoroka........
Itaendelea.
Aahh yani mimi kwata ndio my best na sijawahi kuwa nanga wa kwata zile steps kwangu zilikuwa very easy to capture, sasa mimi mwendo wa pole unaniboa mimi napenda goose march mwendo wa haraka halafu muwe mnapigiwa ngoma na matarumbeta bwana wee, mimi hata maadhimisho ya sherehe za kitaifa huwa napenda kuangalia lile gwaride la mwendo wa haraka wakifika pale kwenye heshima kulia wanavyochapa zile silaha aahhmimi nina mwili ambao mwalimu wa kwqta akiuona Lazima aniunge kwenye Bogi la kwata dakika 15 tu za mwanzo ata nichoka na kunitimua...
kwata ina watu wake mimi pia ni miongoni mwa watu ambao kwata imetu kataa[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Ruvu wengine tumerudi tumenenepa zetu life was good..... labda kuchakaa rangi ya mwili tuNimepita pita hamna jipya!!!!! Wanangu tuliopita ruvu tujuane hamna mateso makali lkn!
Kwahiyo kwenu mnafokewa sana.Hahaha mkuu umenichekesha sana aisee, mdogo wangu wa kiume alipangiwa maramba Tanga, Sasa yeye ni mweupe, siku amerudi ile wiki moja wanayopewa ya kuapply chuo na mkopo aisee kawa mweusi, kakondaa, mama alipomuona akamkumbatia tu huku machozi yanamlenga, kila saa tunampa mara matunda, mara supu, hafokewi yaani tulimhandle with care, baba na mama wote wamepita jkt ile mujibu ya mwaka mmoja na kaka etu mkubwa yupo jwtz wakampa mbinu mbinu na kumtia moyo hapo akarudi Tena.Ile program ilimtransform Sana dogo kwanza alirudi ile miezi mitatu ilipoisha ana furaha, self discipline ilikua juu sana, zamani kusafisha tu chumba chake mpaka mgombane, maji anaoga ya Moto lakini alipotoka kule anaoga mara 2 kwa siku bila kuambiwa Tena maji baridi anafanya mambo yake kwa wakati, yupo active, nilimfurahia Sana nikasema Jeshi kumbe linabadilisha watu.Mpaka leo anasoma MD mwaka wa 3 yeye ni mtu wa mazoezi tu , anacheza mpira wa miguu na kukimbia hizi mbio fupi, yupo kwenye timu ya chuo.Nilisema nikipata mtoto wa kiume lazima aende JKT mwaka mmoja.
Wenye trauma hawawezi kukuelewaHakika,, kuna vitoto viko hivyo. Lakini binafsi siioni katika kudeka, sijui ni mazoea ya makuzi.
Mfano mdogo, nimekulia kwenye nyumba ambayo haina ndoo za lita 20. Ni tank, majaba na vindoo vya lt 10.
Nimemaliza heka heka za kusoma, nikapata tempo mkoani. Mshua akagoma nisitoke nyumbani kwenda kuishi mwenyewe ama laa niende huo mkoa nikakae kwa ndugu flani, nikakubali kwenda kwa huyo ndugu.
Hilo eneo nikakuta maji kukatika week nzima ni kawaida tu na hawana tank. Wana madumu na mandoo kibao ya Lt20, mimi siwezi kuyabeba.. yule mtu anapiga simu home kunisemelea kwamba najifanyisha. Home wananitetea kidizain aendelee kunizoesha kidogo kidogo.
So hapo napo ni kudeka? Hapana ni mazoea ya makuzi.
Nachukia kuumwa, ile moment mwili unakuwa unconfortable uwa siipendi. So najikuta ndio nimeshalia.
Mazoea ya kusindikizana pia, sijui umeagizwa wapi unaenda na mdogo wako, ama unaenda wapi umeenda na mama. Haya yalinifikia mpaka huku utu uzimani.. nikitoka job imetokea ninaondoka mwenyewe, nashindwa kutembea mwenyewe, naangalia contact list nimpigie nani mpk nifike stand.
kuna mtu humu anaitwa Lenie, nimemsumbua sana. Nikitoka nampigia tustorike mpaka navyopanda hiace. 😂
So ni mazoea na sio madeko… mtoto kamzoea baba ake, akimuona lazima amgande gande. Nyie ndo mnaona madeko? Hapana 😂😂😂
Ujue nawasoma muda mrefu mpaka mnanikera kuita pitshort ile inaandikwa PT Short sio pitshortNi physical training shorts sema kikule ndio zinaitwa pitshot kufupisha.
Hahaha mkuu umenichekesha sana aisee, mdogo wangu wa kiume alipangiwa maramba Tanga, Sasa yeye ni mweupe, siku amerudi ile wiki moja wanayopewa ya kuapply chuo na mkopo aisee kawa mweusi, kakondaa, mama alipomuona akamkumbatia tu huku machozi yanamlenga, kila saa tunampa mara matunda, mara supu, hafokewi yaani tulimhandle with care, baba na mama wote wamepita jkt ile mujibu ya mwaka mmoja na kaka etu mkubwa yupo jwtz wakampa mbinu mbinu na kumtia moyo hapo akarudi Tena.Ile program ilimtransform Sana dogo kwanza alirudi ile miezi mitatu ilipoisha ana furaha, self discipline ilikua juu sana, zamani kusafisha tu chumba chake mpaka mgombane, maji anaoga ya Moto lakini alipotoka kule anaoga mara 2 kwa siku bila kuambiwa Tena maji baridi anafanya mambo yake kwa wakati, yupo active, nilimfurahia Sana nikasema Jeshi kumbe linabadilisha watu.Mpaka leo anasoma MD mwaka wa 3 yeye ni mtu wa mazoezi tu , anacheza mpira wa miguu na kukimbia hizi mbio fupi, yupo kwenye timu ya chuo.Nilisema nikipata mtoto wa kiume lazima aende JKT mwaka mmoja.
Sahihi kabisa.Lakini tofauti na majeshi ya nchi zilizoendelea huku kwetu bado tunachapana kama punda, kule kwa wenzetu ni matusi tu kama kawa lakini drill instructors hawaruhusiwi hata kumkunja recruit, huku kwetu afande anamnyuka kuruti utasema anapiga mtoto wake
Nanga maana yake ni Mjinga au mtu mwenye uelewa mzitoSisi Raia mnatuacha solemba!
hivi Nanga ndio nini Afandi
Yaani ukitaka tu shughuli uliyofanya naweza kujua wewe ni kuruti wa mwaka gani mfano wewe ulikuwa wa kujitolea op makaoKule kwenye kuku nlikuwa naenda mara Moja Moja, ile mwanzoni nlizozana na serviceman Moja aisee nkapangwaga kwenye ujenzi uwanjani hlo tofali kulinyanyua😁siku kama hakuna ujenzi tunaenda kuangalia ruvu shooting wakifanya mazoezi
Kujila ni kujitoa/kujituma kufanya kazi ambazo una uwezo wa kudoji/kuziachaHaha,, kuna wakati misemo yao ilikuwa imenikaa mpaka nilipo move on kwa kijana yule. Kwa sasa mengine naanza kusahau.
Kujila si kujipa utawala flani wa kuibia huku ukiwategea wenzako? Kama sijasahau. Kind of uvivu.
Kama ulipata kitengo mbn unang'aaa mapema tuRuvu wengine tumerudi tumenenepa zetu life was good..... labda kuchakaa rangi ya mwili tu
Mi ni mujibu wa sheria.... natamani nikurahisishie code ila naona umeanza mwenyewe! Haya endelea kijana wa Ngonyani baba lao😁Yaani ukitaka tu shughuli uliyofanya naweza kujua wewe ni kuruti wa mwaka gani mfano wewe ulikuwa wa kujitolea op makao
Mbuge aliondoka kipindi cha kati ya op magufuli na op mererani akaenda kusimamia ujenzi wa ukuta wa mererani kisha akaenda Dodoma akisimamia ujenzi mpaka alipopelekwa kwenye madaraka ya ukuu wa wilaya🤣🤣🤣🤣 nilijua tuuu utawataja wale wachina...enzi napita hapo kulikuwa na mbu wengi sana Kuruta tulisumbuliwa sana na maralia...ilikuwa ngumu pia kujongomea...porini kulikuwa na chatu wakubwa...harafu wewe kama ulipita enzi za Mbuge itakuwa ilikuwa OP Kikwete...? au miaka 55 ya uhuru...?
Mbunge licha ya kuaondoka alikua anarudi sana pale kambini Kuna kipind alikua anarudi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Ruvu jkt club, anaenda hadi shadidi kuleMbuge aliondoka kipindi cha kati ya op magufuli na op mererani akaenda kusimamia ujenzi wa ukuta wa mererani kisha akaenda Dodoma akisimamia ujenzi mpaka alipopelekwa kwenye madaraka ya ukuu wa wilaya
Yes nimejichanganya nlimaanisha wa mujibu, wa kujitolea walikuja nyinyi mkiwa mnakaribia Kumaliza lakini mlikuwa mnafoleni pamoja usiku ila mnatenganishwa ninyi na wao.Mi ni mujibu wa sheria.... natamani nikurahisishie code ila naona umeanza mwenyewe! Haya endelea kijana wa Ngonyani baba lao😁