Niliyoyaona Rwanda, yapo mengi ya kujifunza na kuiga

Msigazi Mkulu

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
4,137
3,323
Wiki mbili zilizopita nilipata fursa ya kutembelea nchi jirani kwa mwaliko wa ndugu yangu anayekaa huko katika Province flani, wilaya flani(samahani kwa kutokuweka wazi). Kiujumla hali ya hewa ya ni nzuri kuna ubaridiubaridi. Kijiografia, karibia nchi nzima ni vilima(hills) na mabonde. Karibia ardhi yote inatumika kwa shughuli za binadamu. Sio rahisi kuona mapori. Hivyo ardhi ni finyu.

Nitaongelea niliyoyaona katika vipengele vifuatavyo:

1. Usafirishaji na miundombinu. Nilitumia njia ya barabara. Vyombo vya usafiri baina ya mikoa na mikoa au wilaya na wilaya ni coaster. Barabara zote zina lami. Kilichonifurahisha hapa ukifika tu kituoni ukakata tiketi inaonesha na muda wa kuondoka na ukifika tu mnaondoka.wapiga debe hakuna.

2. Bihashara pamoja na ukusanyaji wa mapato. Maeneo ya kufanyia bihashara yako kwenye mpangilio mzuri. Hakuna vibanda vya hovyo mijini, wala machinga. Complex zao zimejengwa vizuri kila wilaya. Kuna masoko pia ya vyama vya ushirika kila kata. Usafi unazingatiwa sana kwenye hayo maeneo ya bihashara na bidhaa zao zinavutia sio kama bongo unaingia skononi unakuta ndizi zina matope. Kwenye kukusanya mapato, hapa jamaa wako mbali sana aisee, kila bihashara inayofanyika lazima ilipiwe kodi. Iwe saloon hata wakata tiketi za usafiri zinatolewa kweye mashine za EFD.

3. Suala la ulinzi na usalama. Hapa kidogo niliogopa maana muda wote mara polisi au wanajeshi wanapita pita tu. Ujambazi umeshasahulika kule. Ikifika saa 9 jioni, wanajeshi ndo wanaolinda taasisi zote za serikali na polisi wanaendelea na patrol. Hapa kuna cha kuiga Wanajeshi wetu pia wangekuwa wangepangiwa majukumu ya kusaidiana na polisi suala ujambazi lingedhibitiwa kwa kiwango kizuri. Nilishindwa kupiga hadi picha sababu ya hawa jamaa wanatanda sana barabarani huku wakiwa wamekoki mitutu yao. Suala la Rushwa na ufisadi pia limethibitiwa kwa 99%. Wafungwa pia wanatumika kufanya shughuli za kimaendeleo kama vile ujenzi na kilimo.

4. Siasa, hapa raia wa kule hawajishughulishi sana na mambo ya siasa. Wanachojivunia sasa ni amani na maendeleo ya nchi yao. Japo bado watu hawaaminiani miongoni mwao kutokana na athari za mauaji ya kimbari. Hawashirikiani sana kwenye shughuli za kijamii kama vile harusi. Na sio rahisi kuchangiwa kama wewe ni mhusika mkuu.

5.Uchumi na Hali ya maisha ya kwa mtu mmoja mmoja. Ni kama huku kwetu, wapo matajiri na masikini pia. Vijana wengi wa kule wanapata fursa za ajira zenye malipo mazuri kwenye mashirika binafsi yanayofadhiliwa na wazungu. Walimu wa kule pia wana hali ngumu ya maisha kama huku Tanzania, mishaara midogo. Hapa ndo nilihitimisha kuwa viongozi wa waafrika suala la elimu sio kipaumbele sana .Pesa zao pia zina thamani kuliko za Tanzania. Laki moja ya Tz ni sawa na elfu 35 za kule.

6. Elimu, Afya na lugha. Wamejitahidi kuwa na mashule mengi na vyuo vikuu. Shule nyingi ni za mashirika ya dini na watu binafsi lakini zinatoa ufadhili kwa watu wasiokuwa na uwezo hadi vyuo vikuu. Hospitali pia zipo kwa kiwa kiwango kizuri na hapa kila mwananchi lazima awe na bima ya afya. Kama hana anaweza kataliwa kutibiwa. Kumbe hapa bongo watu wanabembelezwa sana, mtu anashindwa kulipia elfu 50 kwa mwaka ili kupata bima?. Kwenye lugha, Rwanda ni multilingual Society. Lugha kuu ni kinyarwanda, vilevile wanajua vizuri lugha za kiingereza na kifaransa. Sikupata shida sana kwenye mawasiliano maana hata bar, mabarmaid wanatema vizuri yai. Hapa Tanzania sijuitunapata ugumu gani wa kutumia kiingereza kufundishia toka shule ya awali na kiswahili kibaki kama somo? Ona sasa wenyewe wameongeza hadi kiswahili. Maprofesa wakatili hapo UDSM wanataka kufanya ukatatili kwa watu maskini eti kiswahili kitumike kufundishia hadi vyuoni wakati watoto wao wapo shule nzuri au nje ya nchi.

Kwa kuhitimisha, mambo mengi nimewasifia hasa suala la kutokuwepo ubabaishaji kwenye uendeshaji wa shughuli zao. Suala ubabaishji ndo limetufanya tufike hapa tulipo. Ona suala la vyeti feki, watu hawasomi kwa bidii wenzao wanasoma kwa tabu alafu baadae wanakosa kazi. Kila idara hapa huwezi kuwa promoted bila kuwa na mtu wa kukubeba. Nilitembelea pia kwenye makumbusho yao ya mauaji ya kimbari. Skeretoni zipo kama maonesho na makaburi ya pamoja.

Pongezi kwa Raisi wetu kwa kuwa na dhamira ya dhati ya kuondoa ubabaishaji serikali, japo una shughuli pevu maana huku wilayani bado watu wanafanya wanavyotaka. Inawezekana hata na hili zoezi la vyeti wakakuhujumu, asilimia kubwa ya watu ambao hawakukamilisha uwasilishwaji wa vyeti vyao vina ukakasi.
 
Basi hamia huko, maake yaani utembelee sehemu ndani ya wiki mbili tayari ujue kila kitu cha sehem hiyo, kweli hii ni copy na paste kama mdau alivyosema hapo juu
 
Kwaio unafananisha mkoa wa kigoma hicho ni ki nchi kidogo sana vipi haukuulizia victoire ingabire kwanini bado amefungwa? kwa nini wanaiita tutsi genocide wakati wahutu nao waliuawa?
 
Huwa nashangaa sana kwa wanaolinganisha maendeleo ya Rwanda ambayo ni ndogo kama mkoa wa Tabora kuipambanisha na Tanzania ambayo ni kubwa kupita nchi zote za east afrika!
Hivi ukichukua lami zote za Tanzania ukazipeleka Rwanda je kuna Ardhi itakayoonekana?
Pengine niseme hivi,
Hata kama sisi tungekuwa tumeendelea kuliko Rwanda si sawa kwetu kujiringanisha na wao! Maana tuna rasirimali nyingi kuliko wao!
 
Even Congo ni nchi Kubwa africa na pia ndio nchi yenye Rasilimali Nyingi sana Africa lakini ndio Nchi maskini africa tena njaa kali udogo au ukubwa wa nchi sio Kipimo Tz ubabaishaji usio kua na tija.
 
We are running East and Central Africa kwa nini tukaige Rwanda hali tumeshatoka zamani kwenye awamu na zama za ''kuondoa umasikini,ujinga na maradhi'', ''zama za ruksa", "zama za utandalizi na tako la regina", "maisha bora kwa kila mdanganyika", na sasa tupo era nyingine ya "viwanda na uchumi wa kati" mbioni kabisa kuanza kutoa misaada kwa nchi za ulaya na amerika kabla ya 2030.~Nikiwa nimekaa pembeni tu ya dreva naona tayari keshawasha indicator ya kulia akiomba njia tu-overtake mbele ya SA kiuchumi
 
Wiki mbili zilizopita nilipata fursa ya kutembelea nchi jirani kwa mwaliko wa ndugu yangu anayekaa huko katika Province flani, wilaya flani(samahani kwa kutokuweka wazi). Kiujumla hali ya hewa ya ni nzuri kuna ubaridiubaridi. Kijiografia, karibia nchi nzima ni vilima(hills) na mabonde. Karibia ardhi yote inatumika kwa shughuli za binadamu. Sio rahisi kuona mapori. Hivyo ardhi ni finyu.

Nitaongelea niliyoyaona katika vipengele vifuatavyo:

1. Usafirishaji na miundombinu. Nilitumia njia ya barabara. Vyombo vya usafiri baina ya mikoa na mikoa au wilaya na wilaya ni coaster. Barabara zote zina lami. Kilichonifurahisha hapa ukifika tu kituoni ukakata tiketi inaonesha na muda wa kuondoka na ukifika tu mnaondoka.wapiga debe hakuna.

2. Bihashara pamoja na ukusanyaji wa mapato. Maeneo ya kufanyia bihashara yako kwenye mpangilio mzuri. Hakuna vibanda vya hovyo mijini, wala machinga. Complex zao zimejengwa vizuri kila wilaya. Kuna masoko pia ya vyama vya ushirika kila kata. Usafi unazingatiwa sana kwenye hayo maeneo ya bihashara na bidhaa zao zinavutia sio kama bongo unaingia skononi unakuta ndizi zina matope. Kwenye kukusanya mapato, hapa jamaa wako mbali sana aisee, kila bihashara inayofanyika lazima ilipiwe kodi. Iwe saloon hata wakata tiketi za usafiri zinatolewa kweye mashine za EFD.

3. Suala la ulinzi na usalama. Hapa kidogo niliogopa maana muda wote mara polisi au wanajeshi wanapita pita tu. Ujambazi umeshasahulika kule. Ikifika saa 9 jioni, wanajeshi ndo wanaolinda taasisi zote za serikali na polisi wanaendelea na patrol. Hapa kuna cha kuiga Wanajeshi wetu pia wangekuwa wangepangiwa majukumu ya kusaidiana na polisi suala ujambazi lingedhibitiwa kwa kiwango kizuri. Nilishindwa kupiga hadi picha sababu ya hawa jamaa wanatanda sana barabarani huku wakiwa wamekoki mitutu yao. Suala la Rushwa na ufisadi pia limethibitiwa kwa 99%. Wafungwa pia wanatumika kufanya shughuli za kimaendeleo kama vile ujenzi na kilimo.

4. Siasa, hapa raia wa kule hawajishughulishi sana na mambo ya siasa. Wanachojivunia sasa ni amani na maendeleo ya nchi yao. Japo bado watu hawaaminiani miongoni mwao kutokana na athari za mauaji ya kimbari. Hawashirikiani sana kwenye shughuli za kijamii kama vile harusi. Na sio rahisi kuchangiwa kama wewe ni mhusika mkuu.

5.Uchumi na Hali ya maisha ya kwa mtu mmoja mmoja. Ni kama huku kwetu, wapo matajiri na masikini pia. Vijana wengi wa kule wanapata fursa za ajira zenye malipo mazuri kwenye mashirika binafsi yanayofadhiliwa na wazungu. Walimu wa kule pia wana hali ngumu ya maisha kama huku Tanzania, mishaara midogo. Hapa ndo nilihitimisha kuwa viongozi wa waafrika suala la elimu sio kipaumbele sana .Pesa zao pia zina thamani kuliko za Tanzania. Laki moja ya Tz ni sawa na elfu 35 za kule.

6. Elimu, Afya na lugha. Wamejitahidi kuwa na mashule mengi na vyuo vikuu. Shule nyingi ni za mashirika ya dini na watu binafsi lakini zinatoa ufadhili kwa watu wasiokuwa na uwezo hadi vyuo vikuu. Hospitali pia zipo kwa kiwa kiwango kizuri na hapa kila mwananchi lazima awe na bima ya afya. Kama hana anaweza kataliwa kutibiwa. Kumbe hapa bongo watu wanabembelezwa sana, mtu anashindwa kulipia elfu 50 kwa mwaka ili kupata bima?. Kwenye lugha, Rwanda ni multilingual Society. Lugha kuu ni kinyarwanda, vilevile wanajua vizuri lugha za kiingereza na kifaransa. Sikupata shida sana kwenye mawasiliano maana hata bar, mabarmaid wanatema vizuri yai. Hapa Tanzania sijuitunapata ugumu gani wa kutumia kiingereza kufundishia toka shule ya awali na kiswahili kibaki kama somo? Ona sasa wenyewe wameongeza hadi kiswahili. Maprofesa wakatili hapo UDSM wanataka kufanya ukatatili kwa watu maskini eti kiswahili kitumike kufundishia hadi vyuoni wakati watoto wao wapo shule nzuri au nje ya nchi.

Kwa kuhitimisha, mambo mengi nimewasifia hasa suala la kutokuwepo ubabaishaji kwenye uendeshaji wa shughuli zao. Suala ubabaishji ndo limetufanya tufike hapa tulipo. Ona suala la vyeti feki, watu hawasomi kwa bidii wenzao wanasoma kwa tabu alafu baadae wanakosa kazi. Kila idara hapa huwezi kuwa promoted bila kuwa na mtu wa kukubeba. Nilitembelea pia kwenye makumbusho yao ya mauaji ya kimbari. Skeretoni zipo kama maonesho na makaburi ya pamoja.

Pongezi kwa Raisi wetu kwa kuwa na dhamira ya dhati ya kuondoa ubabaishaji serikali, japo una shughuli pevu maana huku wilayani bado watu wanafanya wanavyotaka. Inawezekana hata na hili zoezi la vyeti wakakuhujumu, asilimia kubwa ya watu ambao hawakukamilisha uwasilishwaji wa vyeti vyao vina ukakasi.
Yaani unafananisha wilaya na tanzania.Hiyo nchi sawa na wilaya moja tu ya rungwe mbeya.Afterlaw chakula chao si kizuri sana tena ungejua wanatamani sana kuishi tanzania.
Unaweza kuzunguka nchi nzima kwa pikipiki siku moja ukaimaliza na muda ukabaki.
Wabaguzi mwanzo mwisho wenye roho ya unafuu ni watusi.
 
Huwa nashangaa sana kwa wanaolinganisha maendeleo ya Rwanda ambayo ni ndogo kama mkoa wa Tabora kuipambanisha na Tanzania ambayo ni kubwa kupita nchi zote za east afrika!
Hivi ukichukua lami zote za Tanzania ukazipeleka Rwanda je kuna Ardhi itakayoonekana?
Pengine niseme hivi,
Hata kama sisi tungekuwa tumeendelea kuliko Rwanda si sawa kwetu kujiringanisha na wao! Maana tuna rasirimali nyingi kuliko wao!
Nchi Ndogo Rasilimali Ndogo..
Nchi kubwa Rasilimali Kubwa..

Mbona Nchi Kama France, UK zinashindanishwa Uchumi Na Ma nchi makubwa kijiografia kama RUSSIA, USA ,CHINA.?
 
Huwa nashangaa sana kwa wanaolinganisha maendeleo ya Rwanda ambayo ni ndogo kama mkoa wa Tabora kuipambanisha na Tanzania ambayo ni kubwa kupita nchi zote za east afrika!
Hivi ukichukua lami zote za Tanzania ukazipeleka Rwanda je kuna Ardhi itakayoonekana?
Pengine niseme hivi,
Hata kama sisi tungekuwa tumeendelea kuliko Rwanda si sawa kwetu kujiringanisha na wao! Maana tuna rasirimali nyingi kuliko wao!
Point yangu kubwa hapo ni kwamba watanzania sasa yatupasa kubadilika. Tuache ubabaishaji ili mambo yetu yaende sawa. Kingine pia raslimali watu zitumike ipasavyo kama nilivyosema hapo kwenye kipengele cha ulinzi na usalama.
 
Back
Top Bottom