Nilivyo ibiwa kimaajabu

Phenol 41

Member
Joined
Jul 20, 2022
Posts
22
Reaction score
55
Natumaini mko salama! Wenye changamoto poleni.

Leo napenda kushare na ninyi mkasa wa kuibiwa kimaajabu ulio nipata siku kadha zilizopita.
Baada ya kuhitimu chuo kimoja wapo jijini Dar es Salaam niliamua kubaki sikurudi nyumbani kwakua hakukua na inshu ya Kwenda kufanya, niliamua kukomaa nikifanya kazi ndogo ndogo za kuniingizia kipato (Ka mtaji nilikua nako na bimkubwa alinipush kimtindo) niliendelea na mishe mishe hadi mwezi wa kumi 2024 hiyo.

Nilikua na classmate wangu wa advance ambae aliniconnect na jamaa mwingine ambae alikua anafanya kazi kwenye shirika flani hivi la wazungu nikapata mchongo pale, kwakua sikua na cheti wala transcript (vilikua havijatoka) nilitumia provisional result na nikawa nafanya kwao kama nafanya internship (Nilitumia provisional result na jamaa pia alinisaidia sana maana jamaa walinikatalia), basi nikapiga kazi pale mpaka mwezi wa tatu 2025 mradi wao ukawa umekamilika wakarudi zao ulaya namm nikaamua nirudi kijijini kwetu kuwasalimia ndugu na jamaa, nilikaa nyumbani kwa wiki tatu kwa shinikizo la mama na baadae nikaondoka kurudi jijini kuendelea na mapambano ya kutafuta kazi na harakati nyingine za Maisha.

Nilipofika jijini nikapata email ya jamaa mmoja tumwite kimwaga (code) ambae alikua ni supervisor wa kitengo chetu wakati tupo kwenye lile shirika la wazungu alikua kanipatia mchongo flani hivi (Sitautaja kwa sababu za kiusalama), kimwaga nilikua karibu nae kiasi kwasababu alisoma chuo nlichosoma japokua yeye alimaliza chuo miaka 6 nyuma so kulikua na ka ukaribu flani hivi. Sasa baada ya kupokea email yake nilimjibu na kila kitu kikawa sawa na nikasafiri Kwenda mkoani njombe kwaajili ya mchongo alionipatia nilikaa kwa siku 10 na mchongo ukawa umekamilika, ofcourse kimwaga alinilipa vizuri baada ya kazi ile.

(Siyo kazi haramu ila siwezi itaja hapa) aliendelea kunipatia vi kazi vidogo vidogo na nilikua navifanya na ananilipa. Sasa mwishoni mwa mwezi wa sita nilipata tena email ya kimwaga akiniambia kuna inshu nyingine imepatikana nitafute milioni 8 tukapige kazi, (Kazi za mimi kuanda kiasi cha pesa nilikua nimefanya nae kazi mbili so haikua ajabu kwangu) pesa nloambiwa niandae ilikua kubwa kidogo ukilinganisha na nilizokua nikiandaa mwanzo na kwenye akiba zangu nilikua na milioni 3 pekee, hapo hatujawahi kuwasiliana kwa njia ya simu coz sikua hata na namba zake so kazi zote tulifanya bila kuongea directly, yeye alikua ananielekeza kwa jamaa mwingine ambae ndiye nilikua naongeanae).

Nikaanza mchakato wa kupata hiyo pesa nyingine kwani zile tulizolipwa kwa wazungu nilinunua mashamba kijijini kwetu na kuanza ujenzi wa kijumba kwenye ka kiwanja changu hukohuko kijijini.

Baada ya mchakato nikafanikiwa kufikisha milioni 7, hapo niliomba kwa mama (akiba yake na alinikopea VICOBA), kwa my ex-girlfriend pia alinikopesha (huyu ni wakishua sana niliachana nae kwa wema ila bado tunawasiliana) na niliamua kuuza pikipiki ambayo nilimpa mtu aipigie kazi na aliinunua jamaa mwenyewe aliekua anaiendesha. So baada ya kufika hicho kiasi nikamwambia kimwaga kua imefika hiyo pesa akasema haina shida tutafanya hivyo hivyo. Kimwaga kama kawaida akaniambia nitawasiliana na yule mshikaji kwa maelekezo zaidi na nilimpigia simu na tukaongea tu kwa kifupi sana na tulikubaliana kuonana maeneo ya Kinondoni studio kesho yake.

Siku iliyofuata asubuhi nilijiandaa na nikatoka magetoni kuelekea sehemu ya kukutania, nilipanda bajaji hadi kufika eneo la kukutania nikaelekea sehemu za chakula kupata soup wakati nikimsubiri mshkaj aje, wakati naendelea kupiga soup jamaa alinipigia na kusema kua amepata dharula so anamuagiza mtu mwingine aje, sikua na wasiwasi kwa sababu tayari nilikua nmefanya nae kazi zaidi ya nne so sikua na wasiwasi wowote ule, so alinambia kuna mtu atakuja hapo kwa niaba yake, kweli baada ya muda nilipokea simu kwa namba ngeni

Nikapokea alikua ni mdada akiniuliza mahali nilipo, nikamuelekeza na baada ya muda akawa amefika na kunielekeza kwenye gari flani hivi nikaenda na kumkuta mdada amekaa ndani ya gari akiwa na dereva wake, nikaingia na baada ya salamu tukaanza mazungumzo, kwenye yale mazungumzo kuna vitu vingi sikuvielewa na kwakweli sikua interested kabisa na ile kazi kwa sababu process zilikua ni ndefu sana na complications za kutosha, hivyo sikutaka kupoteza muda, nikamjibu tu kua sitaweza hiyo kazi atafute mtu mwingine. Yule dada alionekana kua disappointed kiasi ijapokua alijitahidi kua calm, basi tukaachana hapo na mimi nikaenda Kariakoo kuendelea na mihangaiko ya hapa na pale. Jioni wakati narudi nyumbani nikapokea simu ya yule jamaa wa kimwaga anaongea kwa ukali sana kua nimekua mshamba na nimeacha dili la pesa ndefu, mimi majibu yangu yalikua ni yaleyale kua sikuvutiwa na biashara ile nilishangaa jamaa akaanza kunitukana na kunipa vitisho vya hapa na pale mi nikakata simu nikaendelea na mishe nyingine.

Sasa siku kama tatu baada ya kukataa ile biashara, hiyo siku nilikua maeneo ya kawe kuna mtu nilikua namfanyia delivery ya bidhaa, nilipitia kwenye duka kuchukua maji ya kunywa maana jua lilikua ni kali mno, nilipotoka pale dukani nikasimama pembeni kunywa maji, badae akatokea mdada flani hivi akanambia kaka umedondosha hela akawa ananipa kuitazama ni elfu tano, lakini nikawaza mimi siku ana hiyo pesa kwa wakati huo, maana mfukoni nilikua na elfu 20 (Elfu kumi mbili) pamoja na mia tano nlonunulia maji, nikamwambia yule dada kua pesa ile sio yangu akasisitiza sana anipatie mkononi, wakati sipo tayari kuichukua akawa ameirusha mkononi

Nikaidaka na kuitazama, nilipoishika niliduwaa kama sekunde kumi hivi halafu nikashangaa naanza kumfuata yule dada, akaenda na kuingia kwenye gari namimi nikashangaa namfuata hadi kwenye gari na kuingia kisha gari ikaondoka, hapo nilikua naona kichwa changu ni Kizito lakini nilikua najihisi kuchangamka sana, hapo nikawa naongea sana kupita maelezo. Ndani ya gari kulikua na yule dada halafu na dereva ambaye alikua mwanamke pia (Nilisikia sauti yake akiwa anaongea na simu), kwenye gari yule dada akaniomba simu yangu nikampatia, akaniomba nitoe password lakini nikashangaa siikumbuki, nilijaribu kuingiza lakini nikawa sikumbuki, bahati nzuri kwake na mbaya kwangu simu ilikua na fingerprint, so akanambia niweke vidole na kweli ikafunguka, baada ya hapo akaniomba wallet yangu nikampatia ilikua na ile 20k na kitambilisho cha taifa pamoja na card ya Bank.

Baada ya mizunguko kadhaa tukawa tumefika Bank yule dada akanipatia card yangu ya bank na kitambulisho akaniambia nikatoe pesa yote iliyopo bank, basi nikaondoka na Kwenda na nikaingia ndani, nilipofika mle ndani nikawa sielewi niende wapi, ndipo Afande wa suma jkt (wale walinzi wanaokuepo ndani kutoa maelekezo kwa wateja) akaja na akawa ananielekeza kuandika form ya kutolea pesa sasa nilikua nashangaa vitu vingi sivikumbuki,

Lakini vingi nilijaza kwa kutumia card na kitambulisho, changamoto ikaja kwenye kiasi nilikua sikumbuki nina kiasi gani bank, so ikabidi nimuulize tena afande kua nina shingapi, yule dada alishtuka kdg na kuniuliza kama nipo sawa, nikamjibu nipo sawa, akanielekeza kwenye dirisha hivi nikaenda kuangalia salio kisha nikajaza kwenye ile form na kuipeleka kwa teller kwaajili ya kutoa pesa, teller alinipatia pesa yote milioni saba na laki mbili

(Niliiona kwenye bank statement baada ya tukio) nikaiweka kwenye kimfuko nilichopatiwa na yule dada wa kwenye gari baada ya hapo nikatoka nje ya bank nikawa najiuliza naenda wapi maana hata sielewi, baada kama dakika mbili za kushangaa shangaa nilimuona yule dada nlokua nae kwenye gari akinipungia mkono kwa mbali nikamfuata na nikampatia kile kimfuko cha pesa ila alinirudishia wallet yangu ikiwa na elfu kumi, nikaweka card yangu na kitambulisho kwenye wallet, hapo akawa ananiomba password ya M pesa akitaka nimtumie na pesa zilizoko huko, bahati nzuri kwangu nikawa sikumbuki password baadae ikaja gari na tukapanda na kuondoka, wakati tupo njiani huyu dada na dada dereva wakawa kama wanagombana hivi maana walikua wanaongeleshana kwa ukali flani hivi, mimi sikuwajali maana muda huo nilikua najiona kama naenda kufa hivi maana kichwa kilikua Kizito balaa na macho yalikua kama hayaoni vizuri na kusikia nilikua nasikia kwa shida sana. (Matukio hayo yote nilikuja kuyakumbuka baadae sana kwa sababu wakati yanatokea sikua najielewa).

Baadae sikumbuki tulifika wapi akaniambia nishuke nimfuatie vocha dukani akanipatia elfu mbili, nikashuka kwenye gari nikawa natembea lakini kwasababu ya uzito wa kichwa na kushindwa kuona vizuri niliamua kujipumzisha pembeni ya Barabara nipumzike kidogo.
Sikumbuki ni muda gani ulipita ila nilikuja kushtuka tayari kigiza kimeingia na nipo nimekaa chini ya mtu nikiwa nimeuegemea mti, niliamka baada ya mama muuza machungwa kunitikisa. Nilipo amka nikawa na mshangao mkubwa sana lakini hata hivyo kichwa kilikua bado ni Kizito sana yule mama akawa ananiongelesha lakini nikawa hata simuelewi nikawa nimeendelea kukaa pale na nikalala kabisa, nilikuja kushtuka nikiwa hospitali nikiwa na jamaa flani hivi na mkewe tumepanga nyumba moja.
Ndipo wakaanza kunisimulia kua walikua nyumbani hiyo jioni na mimi nilikua nimekaa kwenye mti ilikua ni karibu tu na ninapoishi so yule mama muuza machungwa aliponiamsha alinifahamu kwani anaishi nyumba ya Jirani na ninapoishi ndipo akaenda kuwaita watu nlokua naishi nao ndio jamaa na mkewe wakaja na kunipeleka hospitali kwani walinikuta natokwa na jasho mwilini kama mtu mahututi.
Baada ya matukio hayo nilienda polisi na uchunguzi ulifanyika ila nilichoambulia ni kufahamu tu kua kimwaga alifariki muda mrefu na niliekua nawasiliana nae hakua kimwaga. Na hata baada ya kuchunguza email yangu zile message zote hazikuepo zilikua zimefutwa na watuhumiwa hawakukamatwa na bado wanatafutwa.
Anyway, niishie hapo, ila kwasasa nimeamua kurudi nyumbani kwanza maana hali ni mbaya, nimepoteza pesa zote na kubakiwa na deni juu natakiwa sio tu kuanza upya ila kuanza kulipa kwanza madeni ya watu na sijui nitaanzaje. Usiku mwema
 
Mwaka 2016. -Posta. Mitaa ya Samora avenue. Jengo la jm mall. Nilipewa Dola 200 na boss wangu ili nikaichenji iwe hela ya madafu. Yeye alikuwa busy kidogo.

Nikasogea mpaka Benjamin mkapa tower, kuna bureau de change alinielekeza . Kabla sijafika kuna jamaa akanifuata na akaniambia direct" kama unaenda kuchange hela usiingie ndan sogea pemben nikuambie wap utapata kwa rate nzur" huku akinishika mkono.
(Sijui alijuaje naenda kuchange dollar)

Kitendo cha kunishika tu mkono nikasikia wenge moja balaa sana. Na nikazubaa sekund kadhaa , jama akawa ananivuta taratib. Ufaham wangu nadhan ulikuwa 5% wakat huo maana sielewi kitu. Ila nikajua nimepatwa na jini kwahiyo nikaanza kusema kimoyo moyo "Yesu Yesu Yesu" niokoe. Ndan ya sekund chache baadae nikaona ufaham unaanza kurud na nikawa namuangalia tu jamaa . This time ashaniachia mkono ametangulia mbele kidogo na ananiita kwa mkono.
Mm Nikazidi kusema ile "Yesu Yesu " na nikaona nguvu na ufahamu unarud taratibu.

Jamaa alivyoona simfuati . Akasepa zake.
Ndio pona Yangu. Kwahiyo sikuibiwa .

Ila nadhan wanatumia majini kupumbaza watu na hii ishu iko sana katikat ya jiji.
 
Hongera ulinusurika mkuu
 
Nimejifunza
 
Wizi wa kupambaza sio mara moja kuusikia. Kuna dada wakala wa pesa alikombwa akiba yote aliyokuwa anaenda ku deposit bank.

Pole sana chief. Siwezi kusema wewe ni mjinga kwa kuibiwa maana inaweza mkuta yeyote yule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…