Nilitegemea vikwazo kipindi cha EPA, ndege ya rais, rada, kusafiriswa twiga

chikambabatu

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
1,337
1,318
Naomba tutafakari kwa pamoja kuna watu tunahisi matukio kama hayo juu pamoja na ESCOW, RICHMOND yameumiza sana taifa hili lisisonge mbele, matukio mengi ya hayo yanaushirika na makampuni ya ulaya, hivyo wameona hakuna sababu ya vikwazo.

Kiukweli sababu wanazotoa kuhusu MCC kwa ulinganifu binafsi naona bado niliwataka waongeze zingine na si hivyo tu, kuwe na mizania. Walipaswa watuwekee vikwazo tu pale katiba ya Zanzibar ilipopitishwa, kwa kuwa inamyima raisi wa JMT kuingilia mswala ya Zanzbar.

Sasa tunashughulika na matokeo ya katiba badala ya sababu. MAGU kwa sasa wanamhujumu tu naamini kwa sababu ya kuwabana washirika wa wakubwa, wakubwa wa ulaya wanataka kufuata sheria na katiba kupiga vita rushwa ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka uzembe kazini na kumtaka kila mtu kufanya kazi (kiaina kama azimio la arusha) nae anatekeleza bila aibu.

Masuala ya sheria ya mtandao pia wakati wa mzee wa msoga, sio kipindi cha raisi ambae mgeni ofisi aendi kwao kunywa nao chai iwe sababu. Nasisi watanzania tunapitishi mikatiba ambayo aitekelezeki ni ubinafsi na kuhisi unamkomoa kundi/upande mwingine kumbe mwenyewe, haya ni matokeo ya kuoneana haya na kubemelezana yanatutia kitanzini hadi tunashindwa kuunda serikali inayoeleweka.

Naomba MAGU na SHENI huu muungano amwachie Mungu kama kuendelea au kukoma, asilazimishe mambo eti kwa kigezo cha kuulinda, kwangu binafsi sioni tofauti ya uwepo au la! nasi wengi huku bara hatuhuelewi wala kuhuhisi, mnapofanya sherehe Zanzibar na Dar bila kupeleka mikoa mingine ndio mnawapoteza watu kabisa, naomba tena tutafakari kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom