kuanzia la 4 hadi la 7 maksi zangu
za hesabu kwenye mitihani
zilikuwa zinacheza kwenye
03%hadi 08%.Matokeo yalikuwa
yanatangazwa mbele ya darasa!
yanapotangazwa mwalimu
anaanza kuwaita wanafunzi
kwakuanziamaksi za chini kwenda
juu (0-100), kwahiyo darasa lote
linajua makaratasi yakiletwa
lazima niitwe kama si wa kwanza
basi wa pili.Siku moja mwalimu
akaanza kuita majina,mpaka
akafikia kwenye maksi
30%,40%,50%,60%,70% bado tu mi
hajaniita. Watu wakaanza
kuniangalia waliokuwa karibu
wakaanza kuniuliza....""eeeh
umepasua hujaitwa, ilikwaje??"
Nilianza kuvimba kichwa, huku
mwalimu anaendelea kugawa tu
makaratasi. Yakabaki makaratasi
ya waliopata 80%-90% bado mi
sijaitwa tu. Mara akabaki na
karatasi moja mkononi, darasa
lote macho kwangu hawaamini
kinachotokea maana bado sijapata
karatasi. Mwishoni mwalimu
akaangalia juu,kishaakasema
"kuna ng'ombe hajaandika jina
kapata 0% aje achukue karatasi
lake"Nilienda kuchukua nikiwa
mpole...
SOMO GANI LILIKUWA LINAKUCHEMSHA ENZI ZILE..