Nilikuwa teja sasa ni mchungaji

Asante kwa ushauri mzuri ukweli nimeishi maisha hayo najua ubaya wake.

Napambana naomba Mungu anisaidie nipate hela ambayo itanisaidia mbali kutoa PDF nitoe vitabu kwenye sober house mbalimbali.

Ili wale wote wanao pata huduma kwenye hivyo vituo wawe na muda wa kusoma hizi shuhuda za kuwajenga
 
We sema unauza vitabu achana na mbwembwe za uchungaji,
 
Wengi tunafahamu, kwa maisha ya mjini inapofika kipindi cha sikukuu, kama vile ‘Christmass’ na Mwaka mpya watoto hufanyiwa mambo mengi mazuri na wazazi wao. Nikiwa mjini naishi kwa ndugu zangu, kipindi cha sikukuu kilikuwa ni kipindi ambacho nilikuwa naongezewa uchungu na chuki.

Watoto wenzangu wote walikuwa wananunuliwa nguo za sikukuu kasoro mimi. Zaidi ya yote, siku za sikukuu wao wanapelekwa matembezini wakiwa wamependeza, lakini mimi ninaachwa nyumbani kama mlinzi.

Mambo ya namna hii ni mazito sana kwa
mtoto kuyabeba.

Ni mambo ambayo kwa mzazi/mlezi anayeyafanya anaweza asione madhara yake, lakini ukweli ni kwamba yanasababisha majeraha makubwa sana ndani ya nafsi za watoto na yanaacha kumbukumbu hasi ambazo zitadumu maisha yake yote.

Hali ilikuwa vivyo hivyo inapofika wakati wa shule kufungua, baada ya likizo kuisha. Watoto wenzangu wote walikuwa wakifurahi kwenda shule, wakiwa na sare mpya zenye kupendeza.

Lakini kwangu mimi hali ilikuwa ni kinyume chake. Hakukuwa na dalili hata kidogo ya kwamba nitapelekwa shule.

Roho yangu ilikuwa inaniuma sana, ila sikuwa na la kufanya. Sababu kurudi kwetu nilikuwa siwezi mana baba ni kama alidhamiria kuniua,

Kosa kidogo tu alikuwa ananishika ananifunga kamba miguu na mikono ananipiga kwa mjeredi wa kuchapia ng'ombe hadi nikawa napoteza fahamu na masikio kuziba.

Siwezi sahau siku ambayo mama yangu mzazi aliamua kutoka kijijini kuja mjini. Lengo lake lilikuwa ni kuwashawishi baadhi ya ndugu wenye uwezo wanisomeshe, japo elimu ya msingi.

Mbele ya macho yangu, mama alijibiwa kwamba, “Ndugu, kama ni dhambi, basi leo hii Mungu na atuhesabie kuwa tumekataa kuishi na kumsomesha mtoto wa ndugu yetu.”

Tokea wakati huo, niliapa moyoni na kujisemea, ni heri kuishi maisha ya mtaani kama chokoraa lakini niwe na uhuru. kuliko kukaa nyumba moja na
ndugu au jamaa kama mtumwa nisiye na thamani yoyote Itaendelea...........
 
Pole na hongera kwa kuitikia mwito wa kuwa pastor, ila kwa ushauri ungeendeleza kisa chako kwa urefu kidogo hapa JF kabla ya kuhamishia wasomaji wako kwenye kitabu.nafikiri ingekusaidia kuvuta attention ya watu kabla ya kuwa direct kwenye kitabu chako.
Ila yote na yote..ubarikiwe sana na Bwana kwa kukubali wito wa kumtumikia.
 
Asante kwa ushauri [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Mchungaji ni vyema utoe ushuhuda wako hapa watu wasome wenyewe kule Mungu amekutoa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…