Nilichojifunza kuhusu mahusiano ya online

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,290
2,468
Wengi wanaoomba mahusiano ni wanaume. Si tatizo kwani hata katika dunia halisi hali ni hivyo. Mwanamke anapoomba mahusiano hupata mafuriko ya maombi. Ni tofauti na mwanaume anapoomba/hitaji.

Pale mwanaume anapoomba mahusiano basi hutokea wanawake kadha wa kadha na inakuwa ni ngumu kubaini uchomoke na yupi (hasa kwa sehemu kama JF).

Cha kufurahisha hapa ni pale kibao kinapogeuka na mwanaume kuonekana kumfukuzia yule aliyeleta maombi. Kiukweli inakuwa ni ngumu sana kuweka commitment kwa mtu ambaye hujui yukoje.

Hii ni rahisi sana kwa wanawake kwani wao inakuwa ni rahisi sana kwao kumuamini, kumpenda na kujiaminisha kwa mtu ambaye hata hamjui kwa vyovyote isipokuwa kwenye mawazo tu. Ni mbaya sana.

All in all ni adventure za watu, na watu wamekutana, pendana, oana na kujenga familia kwa njia kama hizi
 
Wengi wanaoomba mahusiano ni wanaume. Si tatizo kwani hata katika dunia halisi hali ni hivyo. Mwanamke anapoomba mahusiano hupata mafuriko ya maombi. Ni tofauti na mwanaume anapoomba/hitaji. Pale mwanaume anapoomba mahusiano basi hutokea wanawake kadha wa kadha na inakuwa ni ngumu kubaini uchomoke na yupi (hasa kwa sehemu kama jf). Cha kufurahisha hapa ni pale kibao kinapogeuka na mwanaume kuonekana kumfukuzia yule aliyeleta maombi. Kiukweli inakuwa ni ngumu sana kuweka commitment kwa mtu ambaye hujui yukoje. Hii ni rahisi sana kwa wanawake kwani wao inakuwa ni rahisi sana kwao kumuamini, kumpenda na kujiaminisha kwa mtu ambaye HATA hamjui kwa vyovyote isipokuwa kwenye mawazo tu. Ni mbaya sana. All in all ni adventure za watu, na watu wamekutana, pendana, oana na kujenga familia kwa njia kama hizi
100%
 
Wanawake ndio watu wenye imani kubwa zaidi Duniani !
Wanamuamini mtu from no where ni ujasiri wa ajabu sana
 
Na hzi relation za mtandaoni usipokuwa makini ni shda mno....Nakumbuka enzi hizo nilishafunguaga A/C mbili facebook zinazoonyesha ni mtu tofauti nikiwa najaribia kutongoza girlfrnd wangu na wale watu ninao wafahamu lakini wao hawajui ni nani majibu niliyoyapata...Hakika unaweza kata tamaa mno...Heri sheria hizi za mitandao zimebana kona mingi sana.
 
Na hzi relation za mtandaoni usipokuwa makini ni shda mno....Nakumbuka enzi hizo nilishafunguaga A/C mbili facebook zinazoonyesha ni mtu tofauti nikiwa najaribia kutongoza girlfrnd wangu na wale watu ninao wafahamu lakini wao hawajui ni nani majibu niliyoyapata...Hakika unaweza kata tamaa mno...Heri sheria hizi za mitandao zimebana kona mingi sana.
Ulipomtongoza g'friend wako nini kilitokea?
 
Nakumbuka enzi za tamthilia ya Second chance niliwahi kupewa jina la Salvador na mwanamke ambaye hata hatukuwahi kuonana. Nashukuru hatukuwahi kuja kuonana.
 
Wengine wamepata watu wazuri sana wa kufanya nao maisha na wengine wamejibebesha matatizo .
 
Mkuu nimefungua huu uzi kwa mawazo makubwa sana nikijua kuna jambo kubwaaaaa umejifunza juu ya online dating

Kumbe ni hili??...usiku mwema aisee
 
Back
Top Bottom