Nikufundishe nini mwanangu kuhusu wanawake?

Nikufundishe nini mwanangu kuhusu wanawake?

Peculiar

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
821
Reaction score
689
Mwanangu!
Baba yako nimezeeka sasa, nikiwa na ufahamu mdogo,na mwanangu umeshakua kiasi cha kuhitaji elimu hii adhimu,nikupe neno gani? Labda hivi...

1.KUHUSU TAMAA ZAO. Mwanamke yeyote anaweza kukutamani kimapenzi isipokuwa mama yako.
2.KUHUSU HULKA ZAO.wanawake wote huonesha upendo wao wazi wazi isipokuwa wale waliotendwa kabla.
3.KUHUSU KUACHANA.mwanaume kumuacha mwanamke anayempenda ni kama simba kuacha kula swala,mwanamke kumuacha mwanaume ni rahisi kama swala kumkimbia simba mzee.
4.KUHUSU TABIA.jihadhari na maneno ya vijiweni kwamba wanawake wote wapo sawa kitabia,No! Lakini kumbuka "hakuna mwanamke asiye mwanamke".
5.KUHUSU MKE/MPENZI WA ZAMANI.kujaribu kumsahau mtu uliyempenda ni kama kujaribu kumkumbuka mtu usiyemjua.ni ngumu!
6.KUHUSU KUOA.ni sharti na ni muhimu kuoa,lakini ni vigumu kumtambua mke mwema kabla ya kuoa.ni waigizaji wazuri sana! Ukimpata mke mwema utakuwa na furaha ila ukimpata mke muovu utakua mwanafalsafa.
7.KUHUSU USALITI.
Omba sana yasikukute! Ila ni vizuri kujiandaa kisaikolojia kusalitiwa.maana usipojiandaa unaweza kuua mtu au kujiua mwenyewe.ukiua mtu maisha yako yatakosa furaha siku zote.na ukijiua mwenyewe hao waliokusaliti wanaweza kuishi kwa furaha zaidi ya ulipokua hai.
8.KUHUSU PESA NA MAPENZI.mapenzi bila pesa yanapatikana kwa wingi sana huko mbinguni kwa watenda mema,hapa duniani ni ngumu mno.lakini usihofu sana,kuna makubaliano bila pesa.omba mungu!
9.KUHUSU UONGO.wahenga walisema ukweli "unauma".nami nakwambia uongo "unaua".
10.KUHUSU KUWAJUA WANAWAKE.
Ewe mwanangu! Kutaka kumjua mwanamke unahitaji miaka mingi sana ya kuishi kuliko idadi ya nywele zao.usihangaike na vitabu,mjarida,filamu,nyimbo wala hotuba za wanaofundisha mandhari ya wanawake.kuna kanuni moja tu ya kupenda. "ILI UBAKI SALAMA KATIKA KUPENDA SHARTI UJIPENDE KWANZA"

Basi mwanangu,hayo ndiyo machache naweza kukuhusia.nawe una nafasi ya kujifunza zaidi na kufundisha kwa ufanisi kuliko Mimi... Hekima zangu ziwe kama msingi na zitumie kujijenga.
 
asante kwa maneno mazuri haya mkuu
 
miss chagga usiku mwema.

Japo umerudia hii kitu maana ilishawahi kuwekwa hapa lakini bado ni tamu kama shairi la INSIDE VEROSSA la Mpwa wangu Mentor
 
Last edited by a moderator:
kuna wasichana wako addicted na chapaa aisee..nadhani hata mbinguni wataendelea kupiga mizinga
 
Anyway shairi zuri ila huu mchanganyiko wa limao na chunvi kuponda upande mmoja ni zaidi ya unyanyasaji.
 
Back
Top Bottom