Nina mpenzi wangu ambayenimekuwa na mahusiano naye kwa muda wa miaka miwili na miezi kadhaa, tulipendana sana nakuheshimiana na kusaidiana katika hali na mali,
Kwa muda wa mwezi sasaalikuwa na tabia ambazo zilikuwa hazieleweki,kwa kuwa yeye anafanya kazi Arushanilifunga safari mpaka kwenda kule kumsalimia nilikuta kila kitu kimebadilika,alikuwa hanijali tukienda out hanijalihata tukiwa barabarani tunatembea alikuwaanathubutu kuniacha nyuma yeye anakuwa mbele yangu, kuna siku tulienda Clubaliniacha peke yangu akaenda kucheza na wasichana wengine akanidanganya kua niwafanyakazi wenzake, lakini nikamwuliza mbona hujanitambulisha? Akawa ananizungushahakunipa jibu la kueleweka sikumwambia chochote.
Nilirudizangu Dar esSalaam maisha yakaendelea kusonga mbele niliendelea kumpigia simu kumtumiamessage na kumtumia zawadi kila mara nilipopata muda wa kufanya hivyo.
Tumeendelea kuwasilianakila mara na nimeendelea kumwonyesha upendo wangu wa dhati maana sikujua nakufahamu nini kinaendelea. Leo nimempigia simu kumwambia sina pesa nahitajikama laki tatu, haraka haraka kanitumia, amenipigia simu nyingi sana naameniandikia sms akinitaka niende arusha kumtembelea amenisihi sana lakininikamwambia "nilikuja hukunichangamkia wala hukionesha kunijali kweli sijisikiikuja"amenisihi sana lakini nikamwambia kwa sasa sina muda kuna mambo yamebanasana labda Holiday za Xmass na mwaka mpya. Akawa amenielewa tukaongea na mambomengine.
Baada ya muda akanitumiamessage ananiambia kuna kitu anataka aniambie ila nisikasirike nikamwambiahamna noma.
Amenitumia ujumbe huu......
Baby sorry najua nitakuumiza please haikuwa dhamira yangukufanya hivyo but nimejikuta tu imetokea nikawaq na mahusiano ya kimapenzi namsichana hapa Arusha anaitwa Rachel nilimu approach akanikubalia ingawasikutaka kuachana na wewe directly but ikatokea nikawa sikupendi kabisa nanikawa najisikia kero hata kupokea simu yako, ingawa nilifikiria kuachana nawewe lakini nikaona sio vizuri sikufanya nae mapenzi zaidi ya romance, nanilichana picha zako zawadi zako zote ulizonitumia nilichoma moto. Lakini juzinimeachana na. nae nahitaji kuendelea na wewe naomba unisamehe na usichukuehatua mbaya kumbuka tumetoka mbali.
Jamani naomba mnishaurinifanyaje yaani hapa nilipo simu zangu zote nimeziweka kwenye flight mode nanyingine Offline sitaki pokea simu zake, please nahitaji ushauri wenu
lola
Endelea nae tu,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,kama kashaachana na huyo Rachel, what is the problem then? Granted he was and has been up to no good but rarely you will find men with such honesty! My advise is jimwage nae ila usiache kumpa joto ya jiwe so he can learn that you are not his to use and dump when he pleases to!!!
anapima uvumilivu wako. kwani angekuwa mjeuri asingepoteza muda kukupa hiyo stori, ukizingatia mlikuwa hamjaachana. na hujawai mjua huyo mtu anaemsema
kwa uzoefu, ni kuwa anamtu mwingine ambae amewekwa kwenye mzani na wewe. na huyo mtu sio huyo aliyemtaja. anawaona wote mnafaa kwa kila namna. hapa anaangalia reaction yako. kama uki react vibaya ujue ndo mwisho. ukimwonyesha uelewa basi it ticks the boxes
sasa kidume kimefunguka na kukueleza ukweli
na kimeomba msamaha....na wewe unauliza ufanyaje?
ukimsamehe si ndo poa?
mnatufanya tushindwe 'kukiri' na kuomba msamaha
kwa sababu mnatumia 'kukiri na kuomba msamaha' kama silaha ya kutuadhibu...
wanaume wengi wakisoma hii post watasema huyo jamaa yako
'alikosea mno' kukueleza ukweli
angejirudisha kimya kimya bila wewe kujua kilichotokea....
Kweli kabisa, huyo kaka ni wa kusamehewa manake ameamua kuwa mkweli mwenyewe, mwingine angeamua kunyamaza na maisha yangesonga mbele bila mdada kujua kilichokuwepo nyuma ya pazia. Lola hajawahi kukutana na mwanaume unamfumania live na bado anakataa, hakiri hata kwa mtutu wa bunduki, mie ntamshangaa sana kama atashindwa kumsamehe mwenzi wake!sasa kidume kimefunguka na kukueleza ukweli
na kimeomba msamaha....na wewe unauliza ufanyaje?
ukimsamehe si ndo poa?
mnatufanya tushindwe 'kukiri' na kuomba msamaha
kwa sababu mnatumia 'kukiri na kuomba msamaha' kama silaha ya kutuadhibu...
wanaume wengi wakisoma hii post watasema huyo jamaa yako
'alikosea mno' kukueleza ukweli
angejirudisha kimya kimya bila wewe kujua kilichotokea....
Good, nafurahi kusikia umefunguka mpendwa.asnte Boss wangu kwa kunifungua, i appreciate you...
Kweli kabisa, huyo kaka ni wa kusamehewa manake ameamua kuwa mkweli mwenyewe, mwingine angeamua kunyamaza na maisha yangesonga mbele bila mdada kujua kilichokuwepo nyuma ya pazia. Lola hajawahi kukutana na mwanaume unamfumania live na bado anakataa, hakiri hata kwa mtutu wa bunduki, mie ntamshangaa sana kama atashindwa kumsamehe mwenzi wake!
Kweli kabisa, huyo kaka ni wa kusamehewa manake ameamua kuwa mkweli mwenyewe, mwingine angeamua kunyamaza na maisha yangesonga mbele bila mdada kujua kilichokuwepo nyuma ya pazia. Lola hajawahi kukutana na mwanaume unamfumania live na bado anakataa, hakiri hata kwa mtutu wa bunduki, mie ntamshangaa sana kama atashindwa kumsamehe mwenzi wake!
Huyo jamaa nae ni zuzu,kwa nin asingerudi kimya kimya tu?
Umeonae!halafu yeye mwenyewe anasema 'anampenda' bf wake
sasa ushauri wa nini tena?