Nikiwa DC au RC, nitawaacha Mrema na chama chake wakusanyike lakini sio kwa UKAWA

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,738
22,466
Habari mnaolalamika,

Hata atawale nani wa chama gani atafanya hivihivi tu, tatizo ni mfumo, DC na RC ni wasimamizi wakuu wa serikali/ ni amri jeshi wa maeneo yao, hawa huteuliwa na rais na wapo pale kwa matakwa ya chama tawala, wanauwezo wa kuamuru jeshi watakavyo.

Hivi mnategemea mimi kada niliyepewa mamlaka kusimamia ilani ya chama changu nikuruhusu wewe chama pinzani ujijenge nikiwa nakuona, nitakuzuia tu kwakuwa natambua utanisumbua nikikuacha ujipange.

Hata ingekuwa ni mimi ningekuwa DC au RC nisingeruhusu chama pinzani kuchukua point kwa wao kukutana maana jeshi lipo chini yangu nitashindwaje kupiga marufuku wakati uwezo ninao? Bora Mrema na chama chake watembee inchi nzima lakini UKAWA sitathubutu kuwaruhusu wasahau.

Updates;
Jeshi la police wapo sawa kabisa, police hufanya kazi kwa amri/order kutoka juu, sasa nashangaa wanaowalaumu, police ni watu wazuri sana lakini pamoja na hayo utii ndiyo kitu kikubwa kwako, unapoamuriwa kuwa piga, hupaswi kukataa hata awe babako mzazi, vinginevyo upige hewani kuzuga kumkosa lakini lengo nikupiga.

Naombeni msilaumu jeshi kamwe.
 
Ndiyo! Lazima nitakupiga pin tu! Maana siwezi kuruhusu ujijenge aisee!
Sasa kuna haja gani ya kuwa na uwepo wa vyama vingi vya siasa..? .
Maana ukitaka kufanya haya unayoyataka usiruhusu uwepo wa vyama vingi..
Nenda shule dogo acha ushabiki wa kitoto..
 
Sasa kuna haja gani ya kuwa na uwepo wa vyama vingi vya siasa..? .
Maana ukitaka kufanya haya unayoyataka usiruhusu uwepo wa vyama vingi..
Nenda shule dogo acha ushabiki wa kitoto..
Kwa akili yako unafikilia kuna vyama vingi hapa? Yaani wewe ndo uende shule nazani; kungekuwa na vyama vingi basi tungekuwa tushapata rais toka upinzani! Jiulize kwanini viongozi Wa vyama huvurugana kila uchaguzi unapokaribia, hivi vi saccos ni Vya ushahidi tu na kuzuga lakini kaa ukijuwa tunacho kimoja tu
 
Are u sure,..?
Unafahamu kuwa ipo sheria ya uanzishaji wa vyama vingi nchini..? Na ipo kikatiba.
 
Haukurudishwa ila uliwekwa ili nchi tajiri ziweze kutoa misaada na kusifia utawala bora. Ni mkutano gani wa CCM ulishapigwa mabomu? ni kiongozi gani wa CCM alishaswekwa lupango? Ni mfuasi gani wa CCM alishakamatwa kwa kuandamana au kudai haki fulani? Ni mfuasi gani wa CCM alishauawa kwa bomu mbele ya kamanda wa polisi wa mkoa akiangalia? Tangu nizaliwe mpaka nitakufa hakuna vyama vingi vitaonekana nchi hii as long as tunachukua chetu mapema.
 
Wambie maana kuna watu wanapenda kulaumu tyuuuuuuuuh wakati ukweli ndo huo
 
Back
Top Bottom