Samboko
JF-Expert Member
- Oct 30, 2011
- 5,420
- 7,775
Habari wana JF,
Niwatakie mkesha mwema wa pasaka,
Tatizo lipo hivi, kuna binti mmoja nilikua na mahusiano nae kwa kipindi cha mwaka hivi akiwa anafanya kazi hapa Dar, tukiwa kwenye mahusiano akawa anadai anatamani kua na mtoto na anataka azae na mimi, nikamwambia wewe bado mdogo pia sio vizuri kuzaa na mme wa mtu subiri ukipata atakaekuoa uzaenae lakini akawa king'ang'anizi.
Baada ya miezi kadhaa hali yake kua tofauti nikagundua ana mimba, akanieleza jinsi alivyoipata kwa kunidanganya hayupo siku mbaya tukafanya bila kuchukua tahadhari yoyote, Mimba ikiwa na miezi mitano akaacha kazi akarudi kijijini kwao tukawa tunawasiliana kama kawaida, tunatoka kijiji kimoja, nikaenda kijijini mwezi wa 12 tukaonana na mimba imekua kiasi.
Baada ya kurudi Dar kama wiki 2 hivi akaniambia mimba ilitoka na sababu ni kua siku tulifanya kule kijijini nilimsababishia matatizo ndio maana ikatoka, akawa anasumbua mara kwa mara nimtumie ela za matibabu nikawa namtumia kiasi maana alikua anadai hakusafishwa kizazi vizuri akawa anadai kuumwa mara kwa mara.
Sasa juzi kanitumia SMS nimpigie lakini sikupiga nikajua anasumbua kama kawaida yake, baadae akatuma SMS kua amezaa mtoto wa kiume na ni wangu huku akitaka nimpe mtoto jina na langu pia la kuandika kwenye kadi la mtoto.
Nilibaki nimeshangaa na nikimuuliza kwanini alificha anadai alijisikia tuu kufanya hivyo ili aje kunishtukiza akishazaa, nimempigia simu mara kadhaa kutaka kudhibitisha bila yeye kujua kama ana mtoto kweli na mara kadhaa nasikia katoto kachanga kanalia kweli, nimeshindwa kumkubalia kua mtoto ni wangu kwa sababu alinificha yeye kang'ang'ania ni wangu nifanye chochote ninachoweza kudhibitisha kama ni wangu yupo tayari, lakini moyo wangu bado unasita kwa kweli.
Nitakua na kosa nikimkataa huyo mtoto?
Nipeni ushauri kidogo wana JF.