Nijuavyo mimi...

ikhlas

JF-Expert Member
Jun 25, 2015
1,045
1,296
As alkm wana jukwaa,

Poleni kwa kazi ya kufikiri na kuumiza kichwa kila siku katika kutafuta ufumbuzi na majibu ya changamoto mbali mbali zinazotukabili...

Na leo basi naomba mlifkirie na hili (kwa mwenye muda),Lina husu kampeni iliokuwa na inayoendelea kusimamiwa na kuendeshwa na Shirika la kudhibiti mawasiliano (TCRA).
Kampeni hii ni ile ya kuzima simu zote zenye IMEI FEKI.yaani simu bandia au simu hewa kwa kile kinacho elezwa kama kutunza na kulindwa afya za wa TANZANIA(sina shaka na sababu hizi).

Japo ni mapema kutoa criticism au kuwa jadili TCRA mara baada ya cku iliotangazwa kuwa simu hizi zingezimwa kupita....lakini nachelea kusema kuwa hii kampeni ilifanywa na kuratibiwa kwa uhodari mkubwa kama AGENDA SETTING kama lengo kuu,halafu hili la kulinda afya lilifanywa kama PRETIX,(KISINGIZIO TU).
Wadau, ninapo sema agenda setting namaanisha kuwa kuwa kampeni hii imepewa air time na promo ya kutosha ili iwe gumzo huku nyuma ya pazia kuna mambo mazito aidha yanafanyika au yana zikwa(yasijadiliwe) na badala yake wa TANZANIA WOTE TUJADILI SIMU FEKI badala ya mambo ya msingi yanayo lisumbua taifa..
Kama kichwa changu cha habari kinavyo jieleza,kuwa ni fikra zangu tu hivyo wadau (great thinker hebu liangalieni)
Kilicho nipelekea ni fikirie hivyo ni kutokana na sababu zifuatazo:
1- Kwa mujibu wa habari nyingi za kimtandao na kimazingira hakuna simu ilio zimwa,na ushahidi upo wazi hapa mtaani kwangu watu wengi wana simu za mchina tena zina tumia laini 3 mpaka 4 wala hazijazimwa na zinapiga kazi kama kawaida.

2-Viongozi wa TCRA hadi siku ya mwisho ya jana tarehe 16/6/2016 (kupitia vyombo vya habari) wameonekana waki sisitiza kuzimwa simu hizo,lakini badala yake wamekuwa wakuwa rushia mikwara mafundi simu kuwa atakae fanya utundu watamchukulia hatua(maana ya kauli hizi ni kuwa TCRA wanatafuta visingizio kwa wananchi ili itakapo onekana simu feki zina fanya kazi wao waseme mafundi simu WAMEZIFLASHI) lakini ki uhalisia hawajazima..

3- Wadau wengi wa simu ikiwemo baadhi ya wataalamu wa kutengeneza mifumo ya simu wanadai TCRA hawana uwezo(ki system) kuzima simu za wananchi ambazo ni feki,hio teknolijia hata kama ipo wao TCRA hawana(na TCRA hawaja jitokeza kufafanunua mfumo utakao zima simu feke..)

4-Kuna mgongano mkubwa wa kimaslahi kati ya TCRA na makampuni ya simu za mikononi...TCRA wakizima baadhi ya simu maana yake mapato au faida kwa makampni haya yatapungua,swali je TIGO .AIRTEL,ZANTEL.HALOTEL NA VODA wataichukuliaje kampeni hii? Hasa ukizingatia wao makampuni wamekaliwa kooni na Magufuli kuhusu ulipaji kodi?Je watakubali wazidishiwe kodi ilhali wateja (tena wengi wao) wamepigwa panga na TCRA?

Kutokana na sababu hizo hapo juu na nyengine nyingi,ndo ni kafikiria kuwa TCRA HAWAKUZIMA NA HAWATO ZIMA NA WALA HAWAWEZI KUZIMA SIMU FEKI...
Bali kampeni hii imepewa PROMO ili iwe agenda ya kuzizima/kiziua agenda nyengine zisijadliwe na wananchi wala wapinzani,yaana wakati wapinzani wanaikosoa serikali basi wakose sapoti kutoka kwa wananchi kwa kuwa ATTENTION NA MAWZO YA WANANCHI YATAKUWA YAPO KWENYE SIMU FEKI,na muda huo huo serikali wanaendelea na YAO..

Hebu fikiria masuala ya msingi yaliyio wekwa pending kwa sababu ya HABARI/KAMPENI YA KUZIMA SIMU FEKI..

1-SUKARI
2-SAKATA LA UPINZANI KUTOKA BUNGENI
3-SERIKALI KUIDHAMINI IPTL kuchange mtambo wao kuwa wa gesi wakati IPTL ni mali ya watu binafsi chini ya mwamvuli wa PAP
4-Sakata na hatma ya wanafunzi wa DODOMA,
5-Muelekeo wa AWAMU YA 5 CHINI YA JEMEDARI MAGUFULI
6-UFISADI KWA UJUMLA..


Pamoja na mengine meeeeeeeeeengiii...hayo nilio yaoredheshwa yote yamezidiwa nguvu na kampeni ya KUZIMA SIMU FEKI...je ni AJALI AU IMEPANGILIWA?

Mimi nafikiri imepangwa ili kuzima hoja zenye maslahi mapana na taifa..(naomba ieleweke hata mimi naunga mkono zoezi la kuzima simu feke)
Lakini kwa nini hakuna simu hata moja ilio ripotiwa kuzimika au bado mapema?


NIONAVYO NI AGENDA SETTING......

ahsanteni.....
 
Kamati ya ubongo wako inakushauri mambo mengi ya uongo research yako imejaa asilimia nyingi element za uwongo kuliko ukweli hata hivyo zoezi la kuzima simu halijafanikiwa sana na halitafanikiwa kivile lakini si kwa sababu ulizosema
 
Kamati ya ubongo wako inakushauri mambo mengi ya uongo research yako imejaa asilimia nyingi element za uwongo kuliko ukweli hata hivyo zoezi la kuzima simu halijafanikiwa sana na halitafanikiwa kivile lakini si kwa sababu ulizosema

Nipe za kwako zilizo fanya zoezi lisifanikiwe
 
Back
Top Bottom